[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwan hoyce hajasoma? Uwiiiih
Sent using
Jamii Forums mobile app
Suala SIO kusoma Tuu. Kuna hulka ya MTU kuwa Kiongozi na kuiwakilisha nchi. Makuzi yake , mtizamo wake , style yake ya maisha,Maono yake. Anatitanguliza nafsi yake au ya Wengine?
MTU anayejiona kuwa ni mzuri wa sura kuliko Wengine huwezi Kumpa uongozi Wa umma ni kujilisha Upepo? Unampa MTU mbinafsi ofisi ya umma ukiwa Unajua wazi kuwa Hana uwezo Wa kuiwakilisha nchi maskini katikati ya nchi Tajiri Duniani. Hao hua wanaajiriwa kwenye mataasisi makubwa ya kibeberu ambayo mishahara yake ni kuanzia mil. 30 na kuendelea. Ukimpa ofisi ya umma ni Sawa na kumkabidhi Paka Chumba Chenye Unga Wa sembe alale Ili Hali Unajua wazi kuwa akitaka kunya atakunya kwenye Unga mana anapenda usafi Wa kunya na kufukia Ili asisikie harufu ya kinyesi chake.
Waafrika tusidanganywe na vyeti vya Shule bila kuangalia Maono na Tabia na uadilifu Wa MTU.
Wazungu walikua wajanja sana. Walipoona waafrika wanadai Uhuru walianza kuwaandaa Watoto Wa Machifu kuwa Mawakala Wa Ukoloni na Kisha kuwakabidhi nchi baada ya kuwasomesha kwenye Shule maalumu Ili wasije wakawa na ujasiri kama ule Wa Machifu . Waliwapa elimu iliyowafanya wajione kuwa wao ni watu Wa maana sana na kuwadharau waafrika wenzao na Kila kitu Cha Mwafrika na kukiona kuwa ni cha kishenzi. Waliudharau mpaka uafrika na Bara la Afrika na kuona kuwa Ulaya ni Kama Peponi na Afrika ni Jehanam .
Wasomi wengi SIO wazalendo. Wanapaswa kulazimishwa kuwa wazalendo na SIO kubembelezwa kama ilivyo Sasa . MTU ni profesa lakini hawezi KUFANYA utafiti Kwa ajili ya nchi yake. Anachotaka ni kulipwa posho na maraurupu makubwa Lakini hakuna alichoufanyia nchi . Anakimbilia miradi na tafiti za Wazungu Kwa manufaa Yao. Bila kujua wazungu wamefikia walipo Kwa sababu ya wasomi waliotangulia ambao WENGINE walikufa Katika tafiti Kwa manufaa ya nchi ZAO. Mfano Stigler aiyekufa Wakati Wa KUFANYA utafiti Wa BWAWA la Nyerere Karne ya 20. Leo tuna maDr. waPhD na mapropesa Wa tafiti za mitandaoni lakini wanapenda kusifiwa Kwa vyao vyao SIO Kwa waliyoyafanya?
Afrika safari ni ndefu sana kuwafikia wanadamu Wenzetu wenye ngozi nyeupe na nywele ndefu .
Tuna wasomi kama wao , tuna vitabu kama wao, tuna vyuo vikuu kama wao ,tuna serikali kama wao ,tuna watu kama wao wanaume Kwa wanawake . Tunazaana kama wao ,tunakula kama wao,tunakunya kama wao ila tuna Rasilimali nyingi kuliko wao . Chaajabu tuna umaskini mkubwa kuliko wao.
Tatizo ni kuwa wasomi wao na watawala wao wanapatikama Kwa lengo la kusasidia jamii na umaarufu wao haulazimishwi Bali unatokana na kile wanachokifanya kwenye jamii Kwa uzalendo Mkubwa na kujitoa. Kwetu Jamii inagharamika na kujitoa sana kuwabeba na kuwahurumia Wasomi na Watawala. Watawala na Wasomi Afrika wanajiona ni miungu watu wenye bahati kuwanajiona ni watu wenye bahati kubwa ya kutoka majalalani na kwenda kula na kuvimbiwa kwenye ofisi za umma bila Kutoa Majibu ya MATATIZO ya nchi Kwa vizazi na vizazi.
Wamezalisha vizazi HIVYO Kila sehemu na Sasa wanazalisha wasomi Chawa.