Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #121
Mheshimiwa mwanakijiji,
Mimi nafahamu unaelewa tofauti ya mtanzania asilia na yule mzawa.
No i don't! na maneno hayo hayamo kwenye misamiati yangu. Raia wa Tanzania wanaitwa "Watanzania" hawa raia wengine wanaoitwa "Asilia na Wazawa" mimi sijui uwepo wao ndio maana nimeuliza maana.
Richa ni mtanzania mwenye asili ya Asia (Mtanzania Nusu??? M.M.) lakini kazaliwa Tanzania(uki-trace babu zake wako Asia) na mwingine anajulikana bila ubishi ni mtanzania wa kuzaliwa na kwa asili (uki-trace babu zake asili ni Tanzania).
Hawa mababu tunaenda nyuma kiasi gani? Babu wa Babu? Babu babu yake na Babu? Wairaqw wa Mbulu mababu zao wanatoka mashariki ya kati au pembezoni mwa Pembe ya Afrika, hawa ni Watanzania? Wanyakyusa asili yao ni Kusini mwa Sudan toka ufalme wa Malkia wa Kinubi hawa ni Watanzania licha ya kuwa mababu zao wanatoka Nubia? Wasukuma asili yao ni sehemu za Magharibi ya Uganda, na walihamia eneo la sasa la Tanzania miaka kama 700 hivi iliyopita, je hawa ni Watanzania nao? Wacchaga asili yao ni Niger-Congo, Wahaya nao ni hivyo hivyo! Wadigo nao ni hivyo hivyo, wahamiaji wa Tanzania, Wangoni kila mtu anajua hilo (tena Wangoni hawana hata miaka mia tatu Tanzania!), ! Na makabila mengi yote ni wahamiaji na wa eneo hilo!
Sasa mnaposema "Mzawa" ina maana ya aliyezaliwa Tanzania kitu ambacho Richa anacho, na mkisema "Asilia" ina maana ambaye wazazi wake na babu zake wamezaliwa Tanzania, Richa hata hicho anacho! Sasa, kama Richa ni Mzawa na Asilia, kwanini bado anapingwa?
Ukweli ni kuwa hamjawa na ujasiri wa kusema kile mnachotaka kusema na mnatuzungusha tu kwa euphemisms za "Mzawa na Asilia". Mnapotumia maneno hayo mna maana ya "mweusi". Kama ni hiyo maana yenu kwanini msiseme tu kuwa ushindi ungemuendea Mtanzania Mweusi, Mwafrika Mweusi? Mkisema hivyo hoja yenu inaweza kuwa na nguvu na itathibitisha tunachokisema sisi wengine kuwa tatizo lenu siyo uzawa wala asilia, tatizo lenu ni rangi!