atuambie! wote wanatumia kiingereza wakati wa kujibu maswali? si kweli! kama sikosei mashindano ya 2005 au 2006 kuna mrembo alikuwa na mfasiri wake na nadhani alikuwa kwenye top 5, mnaokumbuka vizuri naomba mnisaidie. Kuhusu wahindi kuwa wabaguzi mi nina experience yangu mwenyewe, mdosi yule sintomsahau and i really hate indians kwa jinsi a(wa)livyonitendea, tena nikiwa ndani ya nchi yangu!ieleweke kuwa wahindi ni wabaguzi na kinachompata Richa sasa ni payback time, anadeserve - wahindi wote wanadeserve! kama wana akili safi waanze kujisahihisha/kujisafisha or else ..... i dont care about legacy ya Nyerere! its too much and we wont mouth it anymore ..... Hoyce kawasha moto! hata kama kakanusha kuwa hakuwa akipinga rangi(more precisely tabia chafu iliyojificha ndani ya rangi ya kihindi), nahisi alikuwa akifanya hivyo, mimi na jamii nyingine yenye mtazamo huo au inayoonja ubaguzi na maudhi ya wahindi tunamtaka asikanushe wala kuomba radhi ... yupo sahihi! tena mumwacheni!
hakuna cha nini wala nini, hakuna cha kujifanya ati "miye walinibagua basi na miye nawabagua".. ubaguzi hauna sababu! Ubaguzi asili yake ni hisia ya kujiona bora kuliko mtu mwingine hata kama mtu yule mwingine hajakufanyia wewe jambo lolote lile baya! Angalau mnajitokeza ili tujue kuwa wabaguzi wapo hata wa rangi nyeusi! Na sumu yenu tutaendelea kuipinga kwa nguvu zote. Wabaguzi kama nyinyi ni hatari kabisa kwani hamuishii kwenye kuchukia tu, ubaguzi hauokomi na hasa ukipata nafasi ya kulipiza kisasi! Tunawapinga nyinyi wabaguzi mambo leo, hamna nafasi katika Tanzania na mawazo yenu ni ya hatari kama ukoma! Tutaendelea kuwapinga nyinyi wabaguzi ambao mnataka kutumia ushindi wa Richa kama kichocheo cha itikadi zenu potovu na za kibabe! Tunawapinga nyinyi wabaguzi mambo leo, ambao licha ya kukosa hata sababu moja ya msingi mnataka kumuadhibu binti huyu wa kitanzania kwa vile hafanani nanyi na kwa vile ati "wahindi walininyanyasa!".. Tunawapinga, tunaendelea kuwapinga, na tutazidi kuwapinga hadi pale mtakapotambua kuwa "binadamu wote ni sawa" na kila mtu "ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"!
Tanzania tutakayoijenga ni Tanzania ile ambapo wana na mabinti wake wote bila ya kujali hali zao za kimaisha, rangi zao, dini zao, au mahali wanakotoka, au asili yao ya kitaifa, watakuwa na haki sawa, na nafasi sawa. Tuliupinga ubaguzi wa mtu mweupe dhidi ya watu weusi, tukaonesha makosa yake, na hatimaye ukaporomoka katika himaya yake ya mwisho kule Afrika ya Kusini, na sasa tumeanza mapambano mapya ya kuupinga ubaguzi wa watu weupe unaofanywa na watu weusi, hadi na wenyewe uporomoke kama vipande vya biskuti na uwe umesagika na kuwa tikitiki kama tikiti maji lililoangushwa kwenye mwamba!
Fikra zenu na vitendo si za kupuuzwa bali za kubezwa na si za kutweza! Kama vile wabaguzi wa Marekani walipata msemaji wao ndani ya Gavana Wallace, na wale wa Afrika ya kusini kupata msemaji wao kwenye P. W Botha, na nyinyi wa Tanzania inaonekana mmepata msemaji wenu kwenye Hoyce Temu, na waandishi ambao wanajifanya wanatetea usawa kumbe wanashiriki katika kupenyeza sumu yao ya kibaguzi! tunawapinga, tunaendelea kuwapinga na tutazidi kuwapinga!
Sumu yenu ya kibaguzi huwa haikomi, na hupenya kama mshale wa mwindaji, na kuwadunga wasiokuwa tayari na kuwafanya mateka wa fikra hizo mbovu!! Kwa ngao ya utambuzi wa usawa wa binadamu, tukisimama kidete kama majemedari wale waliopinga ubaguzi kwenye vilima vya Wamatumbi, na wale waliosimama kumwaga damu zao kulinda heshima ya mtu mweusi na haki ya watu weusi kuwa na haki sawa na binadamu mwingine yoyote! Tunawapinga kwa majina ya mababu zetu ambao walipigana kwa nguvu zote kupata nafasi ya kuishi kama binadamu wengine na kutambuliwa kama binadamu wengine na siyo kupigana ili wao wawe juu ya binadamu wengine! Kwa majina ya Mkwawa, na Ihunyo, kwa majina ya Songea na Mirambo! Tunawapinga, tunaendela kuwapinga, na tutaendelea kuwapinga!
Katika Tanzania hii kila Mtanzania atakuwa na haki sawa na nafasi sawa! Hata wabaguzi wetu na wenyewe wataheshimiwa na kuthaminiwa utu wao licha ya kwamba fikra zao mbovu zitapingwa kwa nguvu zote na hadi kwa masilio ya matone ya damu itiririkayo katika mishipa ya wale wapigania usawa na haki!
Tunawatangazia kuwa hamna nafasi ya kushinda, hoja zenu ni dhaifu, na mifano yenu ya kibaguzi imeporonyoka kama ndege aliyeruka mtego! Ni ninyi wenyewe mliotega mtego huo na mmnaswa wenyewe!