Baada ya kuangalia posts nyingi hapa naona kuna tatizo.Kuna makundi makubwa mawili ambayo yamejitokeza,
Hadi hapo tunakubaliana!
Kundi moja linalojiita la watanzania safi au la watu ambao kama sikosei pia linalojiita siyo lawabaguzi
1: Kosa la kwanza. Hakuna mtu aliyejiita "mtanzania safi" au watu wanaojiita "siyo wabaguzi" Tupo watanzania tunaojiita watanzania period, no extensions, no abbreviations!
(kundi hilo) linasema kuwa Richa ni safi kama theluji na hakuna EVIDENCE au ushahidi wowote kuonyesha kuwa kuna connection yoyote ile ya upendeleo au ubaguzi katika ushindi wa Richa na kwa jamii yetu!.
2. Kosa la Pili: Hakuna mtu aliyesema kuwa "Richa ni safi kama theluji" hayo ni maneno yako. Ila ni kweli tumehitimisha kuwa "hakuna evidence au ushahidi wowote kuonesha kuwa kuna connection yoyote ile ya upendeleo au ubaguzi katika ushindi wa Richa na kwa jamii yetu! Hapo umepatia. Je kuna ushahidi kuwa Hoyce Temu alikuwa anatumiwa na wafanyibiashara weusi na washindani weusi ili kumpigia debe mshindi ambaye atakuwa ni Mtanzania mweusi ili kumkomoa Richa na kutoa funzo? Hakuna mtu aliyetoa ushahidi huo zaidi ya maneno yaliyokuja baadaye!
Kundi hili limeamua kufumbia macho na kuwanyamazisha wote ambao wanatoa malalamiko yao juu ya kuwepo kwa upendeleo wa makusudi kwenye ushindi miss TZ
Hadi hivi sasa hakuna mtu aliyethibisha hata kimantiki kuwa kulikuwa na upendeleo. Madai kuwa Lugha ya Kiingereza ilitumika kumpa edge Richa hayana msingi. Ni upendeleo gani basi ambao Richa alipewa? Je alipewa mafunzo peke yake, je aliitwa chemba na mtu yeyote kwenye mashindano hayo na kupewa majibu kabla? Je Richa alilala walikolala wengine na kula walichokula wengine au yeye kwa vile alikuwa ni Mhindi alipewa treatment ya tofauti? Hadi hivi sasa hakuna aliyekuja na chembe ya ushahidi hata wa kimazingira kuwa Richa alipendelewa. Na hakuna mtu aliyenyamazishwa kutoa hoja zake, isipokuwa hoja hizo zimepingwa na zitaendelea kupingwa! kwa sababu ni hoja za kibaguzi.
Kundi la pili linasema kuwa ushindi ule haukuwa wa haki na kuna matatizo ya kibaguzi katika jamii yetu ya Kitanzania na mara nyingi kuna upendeleo wa makusudi hasa kati ya jamii ya wahindi juu ya ile ya watanzani weusi.
Bahati mbaya sana hukuangalia ili kundi limejipa majina gani! Kundi hili au sahihi zaidi baadhi ya watetezi wa ubaguzi dhidi ya Richa wamejipachika majina kama "Watanzania Halisi", "Watanzania Wazawa", "Watanzania Asilia" na "Watanzania WAzalendo"
Na kwamba mara nyingi watanzania weusi wamekuwa victims wa sera hizi za kibaguzi za wahindi kwa MUDA MREFU TU na kuwa haijawahi kusikika hata siku moja mtu kutoka kwenye kundi la kwanza au kiongozi wa serikali akiwasahihisha au japo kuwakemea wahindi hao kwa sera zao za kibaguzi.
Kwa mara nyingine tena watu wa kundi hilo la pili, wanaendelea kumtumia Richa kuwaadhibu Wahindi! Hakuna hata mmoja wao aliyeonesha mahali popote hata kwa mbali kuwa Richa amehusika kwa namna yoyote ile na ubaguzi au vitendo vya kiudhalilishaji vilivyowahi kufanywa na baadhi ya wahindi! Watu hawa wa kundi la pili wanataka tuamini kuwa ubaguzi ni mbaya unapofanywa na wahindi isipokuwa weusi wakibaguana na kudhalilishana hilo ni sawa! Kama watu wa "kundi la kwanza" hawakuwasahihisha au kuwakemea wahindi hilo linahusiana vipi na ushindi wa Richa? Hakuna uhusiano! Kama kiongozi angesema "wahindi acheni ubaguzi wa watanzania weusi" hilo litamhusu vipi Richa?
Kwa mtazamo wa kundi la kwanza hawa ni wabaguzi weusi! na ubaguzi kwao ni pale tu kundi la pili linapotoa malalamiko juu ya wahindi! hapo ndipo mlolongo wa neno EVIDENCE unapotakiwa!
Hapana si kwa sababu hiyo! Wanakuwa wabaguzi weusi pale wanapochagua mtu asiyehusika na kitendo kibaya chochote kile dhidi yao na kumbagua huyo kama ishara ya kuipinga jamii anayotoka mtu huyo. Ubaguzi wao unadhihirika zaidi pale ambapo binti ambaye wazazi wake wamezaliwa TAnzania, yeye amezaliwa TAnzania, hana nchi nyingine isipokuwa TAnzania, na yeye kama mabinti wengine akatamani kugombea taji la Miss TAnzania (nchi yake kwa kuzaliwa), wabaguzi wetu mambo leo wanasema "hapana hastahili mbona asili yake ni mhindi"! Wanampinga na kumkataa na kumkejeli si kwa sababu nyingine ya msingi, la hasha ni kwa sababu yeye ni Mhindi na anatoka jamii inayotuhumiwa kuwa na ubaguzi na hivyo na yeye ni mbaguzi kwa hiyo na yeye abaguliwe! Ndio maana hawa tunawaita wabaguzi weusi!
na kwao ni haki na ni sheria mtu mweusi akibaguliwa!
3. Kosa la tatu: Si kweli, tumekataa na tumepinga mtu mweusi kubaguliwa na hatuko tayari kuona mtu mweusi anambagua mtu mwingine ambaye si mweusi kwa kisingio kuwa ati na yeye alibaguliwa kwa hiyo na yeye anabagua! Tunaupinga ubaguzi regardless nani anabagua!
na nikosa la jinai mhindi kukosolewa au kuhojiwa pindi kunapotokea malalamiko ya kibaguzi au upendeleo wa namna fulani! hii ni double standard!
4. Kosa la nne, ukisoma makala yangu ya kwanza utaona nimetumia nafasi hiyo pia kutoa dukuduku langu kuhusu jamii ya Wahindi na ni jinsi gani watajionesha kuwa ni sehemu ya Watanzania wengine zaidi. Hakuna mtu aliyesema kuwakosoa wahindi ni kosa! Tatizo hamuwakosoi wahindi, mmeamua kumbagua binti mmoja mwenye asili ya kihindi na kumkosoa si kwa kitendo/vitendo alivyofanya vya kibaguzi (kitu ambacho ningekiunga mkono kumkosoa) hapana, nyinyi mnamkosoa ati kwa vile yeye ni Mhindi! kuna tofauti kubwa hapo!
ubaguzi hauji tu kutoka upande mmoja!na kuhalalishwa upande mwingine!sisi wengine tunapinga ubaguzi au upendeleo kwa pande zote!
Kwa nje maneno hayo yamejaa hekima kwa ndani yanajipinga! Mnakataa kubaguliwa kwa mtu mweusi lakini mnakubali Richa abaguliwe kwa vile ni mhindi! kwenu ubaguzi ni mbaya ukifanywa na mhindi, ili ukifanywa na mweusi basi "unavumilika" na "ni halali". Kama mngekuwa mnapinga ubaguzi pande zote mngekuwa upande wetu!!
tunataka haki itendeke bila ya kujali rangi.Na pale inapotokea malalamiko tunakuwa mstari wa mbele kuchunguza,kuchambua,na kukemea kwa nguvu zote ubaguzi au upendeleo wa aina yoyote ile.
Hapana sir, mnajali rangi! kwenu nihalali kabisa kumbagua na kumkatalia Richa kuwa Miss TAnzania kwa vile tu yeye ni Mhindi! Kwa bahati mbaya hamkukemea maneno ya kibaguzi ya Hoyce Temu, mmeyatetea na kuyahalalisha, hamjawakemea wabaguzi mambo leo ambao hawataki kusikia lolote kwani "Richa sura yake si ya Kitanzania" na ya kuwa "hawezi kuiwakilisha Tanzania sawasawa"!
Richa ameibua malalamiko mengi kuwa hakustahili! na vigezo vilivyotumika havikuweza kuhalalishwa kushindwa kwa wale wengine.Sasa sisi kama wapenda haki tunaungana na wote kudai haki!hata kama tutaitwa wabaguzi.
4. Kosa la Nne. Richa hakuibua malalamiko yoyote! Aliyeibua malalamiko ni Hoyce na mashabiki wake wanakubaliana na mawazo yake ya kibaguzi! Vigezo vilikuwa sawasawa isipokuwa aliposhinda Richa, ila kama angeshinda binti mweusi siku ile wote mngefurahia! NI nani yuko tayari kusema kuwa kungekuwa na malalamiko kama aliyeshinda angekuwa Mtanzania mweusi!? Unafikiri HOyce angeangusha kilio kupinga!? Tatizo vigezo ni vizuri akishinda mtu wenu, ila akishinda msiyemtaka "vigezo vilipindwa". Ni sawa sawa na watu wanaocheza soka, ambapo refa akipendelea timu yenu na kumezea off side mkapachika bao, hamlalamiki, ila akiwageuka na kuwapa bao wapinzani wenu kwa kuruhusu "goli la mkono wa Mungu" mnalalamika! By the way, hakuna kigezo kilichobadilishwa au ambacho mabinti wote hawakujua kabla yake! Walijua lugha ya kiingereza itatumika siyo kwamba walishtukizwa!
Mpaka sasa tunao victims wengi weusi kwenye jamii yetu kuanzia majumbani,kwenye siasa,mahakamani,mahospitalini,mashuleni, madukani,michezoni,mitaani na hata kwenye huo Umiss Tanzania! na kwa miaka mingi watanzania hawa wamelazimishwa au kunyamazishwa kuwa hakuna ubaguzi wowote au upendeleo wowote kwa wahindi juu ya wale weusi.Watanzania hawa hawana mtetezi yeyote yule! wengi wao ama wameshazulumiwa haki zao za msingi au hata kubakwa! na kuitwa majina yasiyoweza hata kutamkwa na mtu mwenye akili timamu! hili pia kwa mtazamo wa kundi la kwanza ni sawa, nani haki mbele ya sheria! na ni makosa na ubaguzi pale tu watu kama akina Hoyce wanaposema jamani hebu tuangalie jinsi muenendo mzima wa ushindi wa huyu binti kama kweli alistahili au la? na kama ni kweli wale wengine walistahili kushindwa!!
whattt!! NI wangapi wamewahi kutukanwa kwa Kichagga ni wangapi wamewahi kuitwa "wapumbavu", "wajinga", "mbwa mkubwa" n.k na watu weusi wenzao! NI kina nani wamewahi kuitwa na wazazi wao au wakubwa zao "nyani kasoro mkia"? Hivi ni nani huyu anayetaka tuamaini kuwa wahindi ni watu tofauti kweli wasiojua matusi, wasiotukana na wasiotaka kudhalilisha watu wengine waliochini yao au watumishi wao? Nimeshaona kwa macho yangu mwenyewe Daktari wa Wilaya akimtelekeza mtumishi wake wa ndani hospitali ya Bugando na kumuacha afe kwa vile tu hakutaka kumhumdumia, na wote wawili walikuwa ni watu weusi! (soma kisa cha Mama Ngaiza)
Kundi la kwanza (linalojiita la watanzania safi au ambalo kama sikosei linajiita pia si la wabaguzi)
rejea kosa lako la kwanza!
kwa sababu ambazo hazijulikani limeshawahukumu na kuwashutumu vikali kundi la pili na kuwabatiza jina la wabaguzi weusi
Sababu za kuwaita wabaguzi zinajulikana, itanichukua muda tena kuzirudia. Simply put, ni wabaguzi kwa vile wameamua kumbagua binti wa Kitanzania na kupinga ushindi wake kwa vile tu anatoka jamii ya Watanzania wenye asili ya kihindi! Nikirudia tena nitaumwa na kichwa!
ati tu kwa sababu kundi la pili limeamua kufichua sera za ubaguzi na upendeleo juu ya tabaka moja juu ya jingine katika jamii yetu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Umiss Tanzania.
This one could go down in JF history as the best spin ever attempted! Tunawaita wabaguzi wanaombagua Richa si kwa sababu ya matabaka bali kwa sababu wanambagua mtu kwa rangi yake na asili na kumtenga ati si "mtanzania asilia"! Kichwa kimeanza kuniuma!
Kwa mtazamo wangu hawa nadhani wanachuki binafsi na Hoyce na kwa kweli ninaweza kuwaweka kwenye kundi la watu wenye ubaguzi wakibinafsi!
5. Kosa la Tano. Hatuna chuki binafsi na Hoyce tunachuki na mitazamo yake ya kiubinafsi yenye kutukuza rangi ya mtu na kujaribu kumfanya duni Mtanzania mwingine kwa sababu ya rangi yake au tofauti yake katika jamii! Tunachokibagua sisi ni sera ya ubaguzi ambayo iliwakilishwa hadharani na Hoyce, tutaibagua sera hiyo na tutaendelea kuimbua na kuwatambua wale wowote watetezi wa ubaguzi katika Tanzania, bila kujali wao ni nani au nafasi zao katika jamii!
Tanzania kama nchi nyingi za kiafrika ina matatizo ya kibaguzi.Wapo wale ambao wanataka tuamini kuwa Tanzania ni safi na iliyotukuka! na kwamba hatuna victims wa ubaguzi wa Tabaka moja juu ya jingine.
Nusura upatie! Tatizo lililoko Tanzania ni baadhi ya watu ambao wanajiona wao ni bora kuliko wengine kwa vile tu wao ni watu weusi! Hakuna mtu anayedai kuwa Tanzania ni "safi na iliyotukuka". Tunasema kuwa Tanzania ilijengwa kwa misingi ya usawa, umoja, undugu, na haki. Misingi hiyo wapo watu wanaoivunja (wahindi, waarabu na watu weusi) Wakati wale wahindi wa kampuni fulani walipowafungia watu weusi kwenye container or something.. tulisimama kupinga na kutaka sheria ifuate mkondo na tukawakemea! Hakuna mhindi ambaye anaweza kuniita mimi mbwa au jina lolote baya na mimi nikainama nikakubali! Siyo mhindi, siyo mzungu, siyo mchina! NItampinga papo hapo! Na kwa hakika hata mtu mweusi mwenzangu haniiti hivyo! Ndio maana sikubali kuitwa "nigger" na mtu yeyote, for I ain't no nigger! Watanzania weusi na wenyewe badala ya kuendelea kukubali au kuinama kichwa na kusema hewala wakati umefika na wenyewe kusimamia na kuutetea utu wao! Kama Richa angeoneshwa mahali popote kuwa amefanya kitendo chochote cha kibaguzi au kutoa kauli yoyote yenye chembe ya ubaguzi, ningempinga kama ninavyompinga HOyce na mashabiki wake.
Mimi kwa sauti KUU NA YA JUU NINALIPINGA HILO! NANIKO TAYARI KUTETEA HAKI NA KUHAKIKISHA KUWA KAMWE HATURUDI KWENYE ZAMA ZA UKOLONI ambapo mtu mweusi alionekana kama bidhaa tu!
Unachopinga ndicho unachofanya, so it doesn't count! PInga kubaguliwa RIcha, kubali kuwa kama ameshinda kihalali basi anastahili kuwa Miss Tanzania! Ukikubali hilo basi utaonesha mfano! Lakini huwezi kukubali hata kama utaoneshwa kwa magnifying glass kuwa kashinda fair and square huwezi kukubali, kwani bado Richa atabakia kuwa ni Mhindi, na wewe na mashabiki wenzako hamko tayari kuona Mtanzania mwenye asili ya Uhindi analiwakilisha taifa letu! Kupinga peke yake hakutoshi! Chukua msimamo!
Ubaguzi unauwa na unauma na kamwe hauna nafasi katika jamii yetu.
Again, almost you got it.. isipokuwa kauli yako inakuw negated na attitude yako na ya wale wenye mawazo kama ya kwako kuwa kumbagua Richa ni sawa!
Na ubaguzi hauwezi kuhalalishwa tu pale kundi moja hasa la wahindi linapoachwa kuwabagua wale wa tabaka lingine yaani weusi na kushutumiwa vikali pale kundi la weusi linapoamua kueleza tatizo hili katika jamii yetu.
Hakuna mtu aliyesema hivyo. Hakuna anayekubali kubaguliwa mtu yeyote at least not me, ila wapo hapa ambao mnakubali kuwa ubaguzi ni mbaya, kuwa kumbagua mtu mweusi ni kumbaya, ila kumbagua mhindi kunakubalika! So, you can't have it both ways!
Hoyce Temu ameelezea tatizo kubwa kwenye jamii yetu! na chakushangaza ameshahukumiwa na kubatizwa majina ya kila aina!
Hapana hakuelezea, ameonesha tatizo kubwa katika jamii yetu kuwa watu weusi wameanza kushabikia ubaguzi wa watu wengine! Watu ambao walipinga ubaguzi wa rangi hata kumwaga damu, leo hii wanatetea ubaguzi wa rangi katika nchi yao! Kusema tatizo kubwa labda hakuoneshi uzito wa kugeuka huko!
Hivi kweli tujiulize sisi wenyewe jamii yetu ya kitanzania ni safi? ni kweli hakuna ubaguzi ambao wahindi wanaufanya juu ya wale weusi? au ni kweli kuwa hakuna upendeleo wowote kweye mambo mbalimbali inapofika kwenye suala la wahindi? au ni sawa watu weusi kubaguliwa na ni nikosa na dhambi kuu wahindi kusahihishwa au kuchukuliwa hatua pindi wanapobagua au kupendelewa?
6. Kosa la Sita: Richa amekosea wapi hadi asahihishwe? NI wapi Richa amebagua!? Ni wapi Richa amependelewa?
wale wanaotaka EVIDENCE walikuwa wapi miaka yote hiyo ambapo watanzania weusi wamekuwa wakibaguliwa??? wakitanzania weusi ambao kwa miaka nenda rudi wamekuwa wakinyanyaswa katika jamii yetu na wahindi, wamekuwa wakiachwa wao peke yao bila ya mtetezi yeyote na hakukuwa na mtu yeyote yule aliyejitokeza kumea ubaguzi huu au kutamka neno EVIDENCE! mambo yakibaguzi yako wazi kwenye jamii yetu!na victims tunao!
Richa anahusika vipi na hili!? Tunaweza kuzungumzia ubaguzi wa kila aina unaoendelea Tanzania, lakini hakuna hata mara moja umeonesha ni Richa anahusika na ubaguzi huo!
na cha kushangaza hawa ambao wako kwenye kundi la kwanza walikuwa kimya kama maji mtungini! kana kwamba mambo yanayofanyika ni sawa! leo hii watanzania wanapotaka kujua ukweli kundi hili linaamka na kuwabatiza kila aina ya majina na kuweka neno EVIDENCE!
Wembe.
Hakuna haja ya evidence, onesheni japo kwa mbali ni wapi Richa amekosea, amebagua, au amefanya jambo lolote la kibaguzi kwa mtu yeyote mweusi, mtumishi wa nyumbani (kama wanao), mwanafunzi mwenzake? n.k Mkionesha hilo mtakuwa na kesi ya kumbagua Richa lakini kwa vile hamna mnajaribu kila aina ya hoja kuonesha kuwa Richa hastahili kuwa Miss Tanzania. Kwa bahati mbaya mmeshindwa kwa hoja, na hoja zenu za kibaguzi mamboleo tutaendelea kuziumbua na kuwazindua mtoke katika usingizi wa kujiona bora na victims! Tunataka mtambue kuwa "binadamu wote ni sawa" hata wahindi! Tunataka mtambue kuwa kila mtu (hata wahindi) wanastahili haki ya kuthaminiwa na kutambuliwa utu wao. Vivyo hivyo watu weusi wanahaki hiyo hiyo siyo zaidi siyo kidogo! Ni katika kutambua misingi hiyo ndipo tutaweza kuupinga ubaguzi popote utakapojitokeza. Tutaupinga ukifanywa na wahindi, tutaupinga ukifanywa na wazungu, tutaupinga ukifanywa na waarabu na TUTAUPINGA ukifanywa na weusi! Hatujali nani anayefanya! Laiti ungetambua hilo, ungejua ni jinsi gani hamumtendei haki Richa Adhi, Vodacom Miss Tanzania 2007!!