Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
- #221
stonetown.. maneno ya hekima hayo... Kuna sifa nyingine si za kujivunia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata hivyo, watetezi hawa wa ubaguzi mamboleo wanashindwa kutuambia ni nani Mtanzania ambaye ana asili ya ardhi hii. Wangoni wanatoka wapi? Wachagga wanatoka wapi? Wamakonde je? Na Wahaya asili yao wapi? Tutawauliza hawa wabaguzi mamboleo (neo-segregationists) je, kama Richa wazazi wake wangekuwa ni Watanzania ambao asili yao ni Nigeria, nao ni weusi, ingekuwa sawa kwa binti huyo kushinda?
Vipi kama ingekuwa ni mtoto wa Wamarekani weusi waliohamia Tanzania miaka ya 60 na licha ya kuwa ni weusi, lakini familia zao zimekaa miaka mia tatu huko Marekani, angestahili kushinda?
Wanasema si hilo tu la wapi anatoka, wanatuambia kuwa Richa hawakilishi rangi ya Watanzania. Kwa hawa wabaguzi mamboleo, rangi ya Watanzania wote ni nyeusi na kama wewe si mweusi, basi Utanzania wako ni robo au theluthi (kutegemea na weusi wako).
Sasa anapotokea binti ambaye ni Mtanzania (kiuraia), lakini si mweusi, wabaguzi wetu wanataka tumtenge kwa vile si Mtanzania kamili? Watu hawa wanashindwa kwa moyo mweupe kuelezea mbona tuna wabunge wenye asili ya Uhindi, tunawafadhili wa klabu wenye asili ya Uhindi, tuna madaktari wa Kihindi, n.k ambao ni Watanzania kwa kuzaliwa.
Jamani mkiangalia tatizo sio rangi. Tatizi liko katika mgawanyo wa mali. Wanaolalamika majority ni walalahoi. wanaona wahindi kama Gabacholi(Mtikila version). Kwa hiyo wana wa Tnzania weusi wanaona wamebanwa kila nyanja ya maisha na wahindi. Chuki inaanzia hapo. wahindi wankuwa treated vipi na a kina maganga wanakuwa teated vipi. Weusi ni indegneous more than wahindi. wanaonaona nchi inaondoka. Pili watu wengi wanaamini wahindi wengi wana dual au tripple citizeship. Tanzania plus Canada au UK, usa AU India au USA. Kwa hiyo wanaonekana kama si wazalendo halisi. Huyo miss Tanzania ahana Passport ya nchi ingine? tusione matokeo ya watu kulaumu bali chunguza source. Ukifika hapo then you can propose a good mitigating ways kuondoa hali hiyo.
HUU NI UBAGUZI!
Bango la nafasi za kazi ya muuzaji kwenye famasia lililobandikwa katika moja ya maduka ya Shoppers Plaza, Dar es Salaam, likionesha sifa mojawapo ya mwombaji ni kuwa Mtanzania mwenye asili ya Asia. (Picha na Emmanuel Kwitema)
![]()
Hili Tangazo la kibaguzi la ajira linapaswa kulaaniwa na kila Mtanzania
Chanzo, Majira 18/01/72007
Watanzania hawana ubaguzi kiasi hicho, ukitaka kujua ona watu wanavyowachangamkia wageni kutoka sehemu mbali mbali.Wahindi wanataka kula keki yao halafu ibaki.Wanataka uraia wa Tanzania lakini hawapo kwenye majeshi ya ulinzi, hawataki kuchanganyika na Watanzania wengine, hawataki kujifunza Kiswahili.
hii lugha ambayo inavunjwa vunjwa Bungeni? Haionekani tutawabagua "waswahili" wenzetu ambao lugha ya Kiswahili kwao bado ni ya kigeni...?