Jamani ningeshauri kuanzishwa kwa thread nyingine inayozungumzia Ubaguzi rangi na Ukabila Tanzania.Kwa nini ninashauri hivyo?
1)Tanzania tunayo matatizo ya ubaguzi wa rangi hasa
kati ya waasia hasa jamii ya wahindi na ile ya watanzania
weusi.Suala la Richa ni punje tu juu ya mambo yanavyosokota
chini kwa chini katika jamii yetu na wote tumeshuhudia
hilo!.Kwa hiyo naona si vibaya kuwa na thread nyingine
ambayo itaweza kulijadili na kulitafutia
ufumbuzi au kupendekeza majibu.
2)Tuichukulie Tanzania kama Tanzania na siyo nchi kama
Marekani au South Africa na kwingineko.Nchi yetu ina
utamaduni na historia tofauti na nchi nyingine. Kwa mfano
Nchini Marekani suala hili walilijadili na kulitafutia
ufumbuzi karibu miaka arobaini iliyopita ingawa nao haikuwa
rahisi,ilibidi wamwage damu ndipo kieleweke!na mpaka leo
bado wanaendelea kuondoa kasoro zilizobaki ingawa bado kuna
maeneo mengi ya kuyafanyia kazi.Nchini Afrika kusini ni
kweli kwa nadharia tu kuwa ubaguzi umekwisha ila nao bado
mambo si shwari.
3) Kuna baadhi ya wenzetu ambao wanatumia suala la Richa ili kutaka kuondoa au kuipumbaza jamii kuwa hakuna ubaguzi ambao waasia hasa wa jamii ya wahindi wanaoufanya kwa wenzao weusi.Kila mara watu wanapotaka kujadili suala la ubaguzi wa rangi,hawa wenzetu wanalipotosha na kuweka lile la ukabila au la weusi juu ya wahindi.Sasa nadhani thread hiyo inaweza kuyachambua mambo hayo kwa KINA ingawa yote yanaelekea kuwa na dhana moja.
4) Tanzania bado ina matatizo ya ukabila,ingawa mambo haya yanaendelea kupungua siku hadi siku kutokana na jinsi watu wa makabila mbalimbali yanavyojichanganya pamoja na kujiona ni taifa moja.Hali hii si hivyo kwa ndugu zetu wahindi,bado ni taifa la wahindi ndani ya taifa lingine likiwa na passport ya Tanzania. Hii ni tofauti na wahindi walioko marekani ambao hujichanganya na wengine bila ya matatizo yoyote!! mifano tunayo.
5)Mzee wetu Mwl.Nyerere alipambana sana na ukabila na ubaguzi, ingawa naye alielekea kuwaadhibu weusi kuliko wahindi pindi wanapofanya makosa hayo.Karibu hotuba zake zote tangu miaka ya sitini alifokea sana weusi walipotaka kubaguana wenyewe kwa wenyewe au kuwabagua wahindi au waasia lakini sijawahi kuona pale alipodiriki kusema kuwa jamii ya wahindi inakosea inapoamua kujitenga au kuwabagau au kuwanyanyasa wenzao weusi!.Tafadhali mwenye mifano naomba awasilishe hapa tuone!
Ninaomba tu kuwasilisha!
Wembe.