Hoyce Temu na Wabaguzi Mamboleo!

Hoyce Temu na Wabaguzi Mamboleo!

Sijui kama unakumbuka nilimuuliza kuhusu "magabachori" alikuwa na maana gani?

...glad uko against this ignorance na cha ajabu mtu kama Hoyce amekaa States miaka yote na ameona dhambi zote za kibaguzi na jinsi watu walivyopigana kuondoa huo upuuzi na akaweza kukaa neighobhood moja na mzungu bila wasiwasi lakini at the end ujinga ni MZIGO...nimeamini ujinga hauna subsitute!
 
Ndiyo maana walisema "if you think education is expensive try ignorance"..
 
that is funny.. mtu anaweza kuingia darasani, bila darasa kumuingia kichwani!
 
Hii issue ipo deep sana wasee....inabidi kuzungumziwa kwa staili nyingine.
 
hivyo huyo HOYCE huko University America alisomea nini maana naonekana naye ni kichwa maji tuuu
 
.

...ninatoa wito kwa Watanzania kuwapinga wabaguzi hawa mahali popote wanapojitokeza, kwani sumu yao inatia ganzi fikra, inapumbaza akili, na inasababisha mtindio wa mawazo. Wabaguzi hawa mamboleo hawana nafasi, hawakubaliki, na wasipewe nafasi wala kukubalika, tumeanza kuwapinga, na tutaendelea kuwapinga! Hadi pale watakapotambua kuwa raia wote wa Tanzania ni sawa na wanastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wao. Vinginevyo tutaanza kuwabagua wao kwa ubaguzi wao hadi tuwe na taifa la wabaguzi wenye kubaguana ambao kila kukicha wanatafuta wa kumbagua.

...kama wanaosema RA ni muirani, mwenzenu mnanichanganya,!!!
 
RA kama anahusika na ubovu wowote ni yeye atahukumiwa na niyeye ndiye atawajibishwa. Hata hivyo haiwezekani aje atokee binti wa Kitanzania ambaye ameshinda fair and square mashindano ya urembo na kwa vile tu ati wazazi wake wana asili ya Shirazi basi abaguliwe kisa RA? It DOES NOT MAKE ANY SENSE! Mimi sitaki nihukumiwe kwa makosa ya Idi Amini!
 
Khadija Kalili


MWISHONI mwa wiki iliyopita, Jumamosi Septemba mosi, ndipo alipopatikana malkia wa urembo nchini, yaani Miss Tanzania 2007, naye si mwingine ila ni Richa Adhia, binti mwenye asili ya Kiasia ‘Mhindi', ambaye tangu azaliwe hajawahi kufika bara Hindi.
Kutokana na ushindi huo wa Richa, Watanzania wengi walionekana kugawanyika, mara baada ya kutangazwa mshindi.

Tanzania Daima ambayo ilikuwepo katika shindano hilo, iliweza kushuhudia mambo mengi yaliyojiri pale Leaders Club na kwa wakati huohuo iliweza kuzungumza na wadau mbalimbali wa urembo, ambao kila mmoja alikuwa akibwatuka kivyake.

Kwa mtazamo tu, shindano la mwaka huu lilipendeza, hasa jukwaa ambalo lilivutia wengi waliofika pale.

Kumbe kila kitu kinawezekana, yaani kwa wale ambao hawakufika, jukwaa lilikuwa zuri mno na taa za kutosha zilikuwepo, jambo ambalo liliwawezesha mashuhuda kuweza kuona hata pini endapo ingedondoka!

Akizungumza na Tanzania Daima, shabiki mmoja ambaye alikataa kutajwa jina lake gazetini, alisema kwamba, wakati sasa umefika wa kukemea rushwa, hata katika mashindano ya urembo na watakaoikemea na kuifichua si wengine, bali ni warembo wenyewe.

"Kama kweli hatutaki kuwakilishwa na watu wenye asili za nje kama ilivyotokea kwa Richa, itabidi wadau wa urembo na Watanzania kwa ujumla kupambana ili kusiwepo na mchezo mchafu," alisema.

Alidai kwamba inaonekana wazi kuwa Richa alikuwa na watu wengi ambao waliamua kumwongezea nguvu ili ashinde na ushindi wake si tu kwamba aliwazidi uzuri na urembo warembo wengine 25, bali kulikuwa na hila.

Aliyekuwa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, naye aliibuka kivyake ambapo alilia hadharani na kusema kwamba yeye analilia haki ya taji la Miss Tanzania kuwa limekwenda kwa mrembo ambaye hakustahili.

"Mimi sisemi kwamba yeye ni Mhindi hivyo hastahili kushinda, la hasha, ila tatizo ni vigezo. Hivi wale majaji walitumia vigezo vipi katika kumchagua mrembo wa taifa?" alihoji.

Hoyce alishindwa kujizuia na kutangaza hadharani kwamba anapingana na matokeo ya mrembo wa mwaka huu na kusema kwamba hastahili.

"Nalia kwa uchungu, hivi hawa majaji wamechagua nini? Vigezo vya urembo ni vipi? Mbona wanaipa kipaumbele lugha ya Kiingereza? Mimi sikubali na ninalipinga hilo, katika hili majaji wamechemsha," alisema Hoyce huku akibubujikwa machozi.

Pamoja na hayo, Hoyce alihoji kwanini mataji mengine yawe yanatolewa siku ya kilele cha kumsaka Miss Tanzania na kwa nini yasitolewe siku inayofuata kama ilivyokuwa hapo awali.

"Wale warembo wako pale kwa ajili ya taji moja tu la Miss Tanzania, na hawako pale kwa ajili ya kumtangaza Miss Redd's.

"Yatupasa kuuenzi utamaduni wa Mtanzania, siku ile pale mimi sikuuona, na hasa ukizingatia kwamba hadi leo bado tunasaka vazi la taifa, warembo wetu hawakuvaa vazi la ubunifu, sasa utamaduni wa Mtanzania uko wapi?" alisema na kuhoji.

Pia alihoji iweje warembo walioingia katika kumi bora ndiyo wawe na haki ya kuvaa vazi la ubunifu, tena katika sare moja?

"Je, waliwatambua kabla ya shindano? Kama jibu waliwatambua, basi hakuna haja ya kuita halaiki ya watu na kuwaonyesha mambo ambayo walikwishayapanga," alisema.

Alisema vazi la ubunifu, lilipaswa kuwepo kwa kuwa hata katika mashindano ya dunia kila mshiriki hutakiwa kuonyesha utamaduni wa kwao.

"Sasa kama mrembo hakuvaa vazi hilo, ataeleza utamaduni gani akiwa huko kwenye shindano la dunia siku ya ‘Culture Day'?" alihoji.

Aliendelea kusema kuwa katika mashindano ya Miss Tanzania, sifa kubwa ni uzuri na kusema kwamba Richa alizidiwa uzuri na warembo wengine walioingia katika tano bora na hata wengine ambao hawakubahatika.

"Sisi tuko hapa kueleweshana ili jambo kama hili lisije kutokea tena, haya ni makosa, tulitakiwa tumtumie Nancy kama dira ya kutuelekeza wapi tulikosea kidogo kuchukua taji la ‘Miss World' kwa kuwa alitufikisha mbali ambako hatukuwahi kufika, mwaka jana walifanya makosa kwa kumchagua Wema Sepetu na sasa wameyarudia tena, bora tuache," alisema.

Lakini, waandaaji wa shindano hilo ambao huongozwa na Kamati ya Miss Tanzania chini ya Mratibu Hashim Lundenga, wameunga mkono ushindi wa Richa, wakisema kwamba alistahili.

Lundenga alisema kwamba Richa alistahili na kwamba hivi sasa kamati inamuandaa ili akaliwakilishe taifa kwenye shindano la kumsaka mrembo wa dunia litakalofanyika Sanya, China, Desemba, mwaka huu.

Kufuatia ushindi wa Richa, wapo wanaodai kwamba kuna mazingira ya kuwepo rushwa ambayo ndizyo ilikuwa ngome kuu ya kumsaidia kushinda.

Sawa, Richa ameshakuwa Miss Tanzania, hakuna mjadala na hata Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), hawawezi kubatilisha na hii sasa inatuonyesha kwa nini katika soka uamuzi ni dakika tisini, na kule ni ubabe ubabe, ukileta ubabaishaji unachapwa, mtu anafungiwa, lakini sasa kilichobaki hapa kwenye urembo ni ya Kaisari mpe Kaisari.

Ina maana kwamba watoto ambao baba zao hawana uwezo wa kupita njia za panya, hawawezi kupewa funguo ya gari lenye thamani ya sh milioni 45, huo ndiyo ukweli.

Jambo hili sasa liko wazi, tena halina kificho, hivyo machozi ya waliolia na kusononeka Inshallah Mola awapoze ila wakati umefika sasa kwa wazazi ambao wana mabinti zao wawapeleke shule za Kihindi, Kichina, Kijapan na hata Kirusi ili mradi tu mwanao aweze kutwaa taji la Miss Tanzania kwakuwa akizungumza Kiswanglish anaonekana mshamba, mwenye ukurutu usiotibika, hana sura ya kuonekana mbele ya watu na kuweza kuielezea nchi yake ambayo babu na mababu zake walizaliwa na kufia hapa, ama kweli waswahili walisema mdharau kwao au chake ni mtumwa, nimeamini.

Kumbe zile shepu za namba nane na mahips hazitakiwi ‘Miss World', nasema hivyo kutokana na kwamba warembo walioshindana mwaka huu walikuwa mashallah, walijaaliwa, tulio kizani tukadhani kwamba taji litaenda Kanda ya Ziwa na kwingineko, lakini wapi, wenye nguvu na wajanja wa mjini wamelinyakua, tena kwa kutumia kisu butu chenye kutu na kuwaachia warembo wetu ukurutu wenye kutu.

Hivyo basi, kilio kile kile kilichomwagwa hadharani na Hoyce, si cha bure, na nina hofu kwamba huenda ikawa sawa na sauti ya mtu aliae nyikani, akiomba msaada huku wengine wakimkebehi na kumwona kama hana jipya.

Ikumbukwe kwamba, huyu aliwahi kuwa mrembo wa taifa na kuiwakilisha nchi, hivyo anafahamu nini huwa kinafanyika kule, hasa wanapokuwa kambini kuanzia kambi ya Miss Tanzania na ‘Miss World' kwa ujumla.

Hivyo basi, Watanzania wote sasa tusisikitike sana, kwani huo ndiyo utandawazi, sasa shime kwa kila dada akajilengeshe kwa Mchina na Mhindi kama kweli atadiriki kuchafua damu yake na Msukuma wa Bariadi, ambapo atakapopata mtoto mwenye asili ya Kichina, Kihindi, Kithailand au Kirusi, itakuwa umemjengea mazingira mazuri ya kusafishiwa njia na kukosa ukurutu ambao ni wenye asili ya mtu mweusi!

Sasa nimegundua kwamba kumbe wapo warembo wazuri ambao Lundenga huwalilia siku zote, lakini hawajitokezi kushiriki katika mashindano na matokeo yake wao huja kama mashabiki.

Kamati ya Miss Tanzania ikumbuke kwamba, hao warembo waling'amua hilo ndiyo maana wako nyuma ya pazia siku zote na hawataki kuja huko wakishindwa muwadhihaki, haipendezi kuona kiongozi wa juu akiwatusi warembo walioacha kukaa majumbani kwao na kujiunga na kambi eti wana ukurutu usiotibika.

Hoyce ambaye alionekana akitembea huku na kule akilia na kuweweseka kutokana na maamuzi ya kumchagua Richa, alisema wazi kwamba majaji walinunuliwa na vigogo.

Tunakumbuka hata Miss Tanzania 2005, Nancy Sumari, ambaye aliibuka kidedea katika shindano la kumsaka mrembo wa dunia na kuwa ‘Miss World Africa', hakuwa chaguo la kamati na hata waandaaji wake wa awali, lakini alishinda.

Hivyo hata huyo naye ni mwenye asili hiyo hiyo ya warembo wenye ngozi ya ukurutu na aliposhinda tuliwaona kila mtu akimpiga kumbo mwingine, haya sasa macho na masikio yetu ni kwa huyo aliye chaguo la kamati.

Hata Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu hakuwa chaguo la kamati hilo liko wazi.

Warembo wengine 13 ambao waliwahi kutwaa taji la Miss Tanzania katika miaka tofauti ni Aina Maeda mwaka 1994, Emily Adolph (1995), Saida Kessy (1997), Basila Mwanukuzi (1998), Hoyce Temu (1999), Jaqueline Ntuyabaliwe (2000), Happiness Magesse (2001), Angela Damas (2002), Sylvia Bahame (2003), Faraja Kotta (2004), Nancy Sumari (2005) ambaye ni mrembo pekee aliyeweza kuiwakilisha nchi vyema kwenye mashindano, aliyeibuka kuwa mrembo bora kutoka Kanda ya Afrika ‘Miss World Africa' na Wema Sepetu Vodacom Miss Tanzania 2006 ambaye atavua taji leo.


Source*Tanzania Daima.

Je haya yana ukweli?Inawezekana alishinda kwa kutumia manoti au?
 
Article ya Khadija Kalili haina jipya zaidi ya kujificha nyuma ya Hoyce Temu katika kuendeleza ubaguzi. Hivi huyu Hoyce Temu anajua zaidi ya Majaji?Is she the authority in beauty? Mwandishi anajikanyagakanyaga huku akiongelea maswala kama "kuchafua damu" ambapo inaelekea wazi yeye ni mbaguzi.
Huyo Hoyce Temu kama anajua sana mbona hakutwaa taji hilo kama alivyofanya Nancy Sumari ambaye simsikii akibwabwaja kama hiki kituko...
 
..hao tanzania daima ni gazeti la udaku au mipasho? hiyo story credibility ni zero!
 
Kada mbona havina uhusiano??

Anyway Mwnakjj nakupa tano, sioni tofauti sana kati yako na watu kama martin L King, Mz madiba, mahatma gandh na Mwalimu JK.

havina uhusiano eeh, just watch out, lakini wahindi wenzako wajanja washajimwaga kwenye siasa, serikali, vyama vya siasa, utamaduni, wewe mtz halisi utabaki na nini ? just watch out am telling you !
 
Richa amefanya yapi kati ya hayo? Na hawa Watanzania Asilia ni wapi?

Kama nilivyomuuliza mtu mwingine hapo juu niwaulize hivi Mtanzania Asilia = Mtanzania Mzawa?



hizi zote ni Bla Bla Bla... Miye nashauri huyu Binti ajiuzulu ili wampe mtu mweusi!

itakuwa vizuri ukiheshimu hoja za watu mzee !
 
mbaguzi hoja zake hazistahili kuheshimiwa! zinastahili kuoneshwa ni jinsi gani zimekosa heshima na hazistahili heshima. Hoja za kibaguzi haziheshimiwi!!
 
ahhh mie nakushangaa Mwanakijiji ambaye wewe unajua fika kuwa mamabo yote yako BRAZIL sasa unahangaika nini?
 
Ubaguzi ni hisia ya mtu kujiona bora kuliko mtu mwingine kwa kulinganisha vitu ambavyo mtu huyo mwingine au anavyo au na hana uwezo wa kuvibadilisha au hayuko tayari kuvibadilisha. Mara nyingi ubaguzi huelekezwa kwa kundi la walio wachache kwenye jamii na hufanywa na walio wengi, au sehemu nyingine hufanywa na kundi la wachache wenye nguvu na mamlaka dhidi ya wengi.
 
Nimesikia kwamba hoyce temu alilia kwa sababu ya kulewa pombe siku ile sio kwamba alilia richa kupewa ushindi ule
 
wandugu UBAGUZI ni ishara ya udhaifu! udhaifu waweza kuwa wa aina nyingi.

Lakini cha msingi hao wanaong'ang'ania miss tz lazma awe mweusi nini hoja yao? kwani kule miss wed wanaenda kucheza dogoli? Utamaduni wa mtz na sanaa ya urembo ya kimagharibi wapi na wapi? alaa!

Ni aibu kwa JF sinia member kama Kada mpinzani na Babu ataka kusema kushabikia ubaguzi.
 
Back
Top Bottom