Siku moja ( ilikuwa usiku ) katika mtaa wa Jamhuri, karibu na mgahawa wa Chef Pride nikiwa pamoja na rafiki yangu mwenye asili ya ulaya, tukiwa katika bar moja ambayo iko karibu sana na mgahawa huo, pia kulikuwepo na kundi la watalii wenye asili ya ulaya pia wakipata kinywaji. Alijitokeza jamaa mmoja mwenye ASILI ya Asia ( simkumbuki vizuri jina lake ) lakini alijiunga pamoja na sisi na tulimkaribisha, lakini kilichofuatia alianza kuwaponda wazi wazi wale watalii ama wageni huku akisema " Sisi ndio watu sio hawa! " akiongeza " Go to your own Country! " kilichofuata baada ya hapo wale watalii walijiengua katika eneo hilo na kushika zao, sikufahishwa na jambo hilo ila nachotaka kusema ni kwamba hata kama wahindi watakuwa wabaya ki namna fulani itakuwa si wote, na hii inalingana na madaraja waliyonayo. mhindi ni binadamu kamili na ana ukamilifu na mapungufu kama niliyonayo mimi,nina Imani Mahatma Gandhi ( R.I.P ) hakuwa na Sera tofauti kama alizokuwa nazo Martin Luther II ( R.I.P ), wote walipenda na walitaka kuwe na usawa ndani ya Jamii, hivyo wahindi ni watu wazuri tu! nitawapa mfano wa jamaa yule aliyejitolea kupigania usawa wa Elimu Nchini na ana Asili ya Ki Asia, huyo naye Vipi? nadhani ni kutokana na mapenzi yake aliyo nayo katika jamii ya ki Tanzania ujitoaji katika kushirikiana na Jamii , kuna misemo kama "kunapokuwa na UPENDO chuki hujitenga, yote haya yamekwenda Wapi?
kuna wahindi ambao wanachanganyikana kabisa na jamii yetu ya kibantu katika nyanja mbalimbali mpaka kwenye misiba na inapendeza kweli kweli, pia kuna ndoa za wahindi na weusi ingawa ni chache na hii inatokana na tetesi kwamba wenzetu wahindi hawapendi mali itoke nje ya Familia!, that is Why Kaka kamuoa Dada na vitu kama hivyo! , na kuna wale ambao wao hujifungia majumbani mwao asubuhi mpaka jioni, unategemea mtu kama huyu atajifunza nini toka kwa jamii inayomzunguka? wanajitenga wao wenyewe! na cha mno wana sehemu zao maalumu za jamii yao kukutana na kujadili yanayowahusu wao, nina hakika hii ni katika kulinda na kutetea TAMADUNI zao lakini hapo hapo hakuna mtu ambaye hapendi na kujali tamaduni zake lakini wenzetu wamezidi ( ninaweza kusema hivyo! ) kwa kujipenda kuzidi kiasi ( SELFISHNESS ) mpaka kufikia hatua za kuoana wao kwa wao.
nilipata kwenda kwenye mgahawa mwingine unaomilikiwa na Mtanzania ( sidhani! ) mwenye Asili ya Asia uliopo mtaa ule ule nikiwa nimeongozana na rafiki yangu yuleyule kilichotokea alihudumiwa mwenzangu mwenye rangi nyeupe na mimi sikupata huduma yeyote ingawa wote pamoja tuliweka order at the same time! hapo sijui tuseme nini?
Kwa ufupi ukiangalia maisha wanayoishi hawa wenzetu utagundua wamejitenga wenyewe, tena kwa manufaa yao, Tazama Wana sehemu za special za kuishi, ( tembelea mikoa yote utaona ) Shule maalumu ( kwa ajili ya watoto wao! ) na sehemu maalumu za mikutano wenyewe wanaziita Tempo ( kama sikosei! )huko wanakaa na kujadili wanayoyajua wenyewe, pia na hili suala pesa zao wanazopata kupitia migongo yetu kuziwekeza katika sehemu maalumu, shortly the whole systems ama TAMADUNI walizojiwekea ndiyo zinazowafanya watuone sisi wabaguzi! ( hawaamini mtu ! ) na hapo hapo mimi ninasema kutokuwa na IMANI na Mwenzako huo ni ubaguzi tosha!, halafu wanasema wanatoa mchango wao katika taifa!!! upi? wa kupiga picha na ma Rais wetu na kutundika katika Maduka yao ! na kama wanajiona wao wana upendo wa dhati na nchi yao ya Tanzania kwa nini wanajinyima haki wao wenyewe kwa kuongoza kutoa Rushwa!? huu ndio unaoitwa ukosefu wa IMANI baina ya Jamii yetu.
Mimi ninachowaomba hawa jamaa ni wapunguze kutoa Rushwa huko TRA, UHAMIAJI na Taasisi nyingine za kijamii, wapunguze pia maisha ya kujionyesha( Showing off ) na tabia zingine zisizo muhimu, badala yake washirikiane na jamii inayowazunguka! USHAURI WA BURE!