Bondpost
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 7,019
- 10,455
Waajiri wamekuwa wabinafsi sana, ni kweli vijana wanamaliza vyuoni wakiwa na distinction kwenye vyeti ila vichwani hawana ubunifu lakini ni mwajiri gani ametumia muda kumoatia induction course hata ya wiki mbili mwajiriwa mpya? Policy zao zinatoa hiyo nafasi?HR flani alilalamika wahitimu wengi Ni weupe vichwani na kuuliza Nini kifanyike
Nilikuwa na haya yakujibu!
Ushauri chakufanya Ni kwanza wakufunzi hasa wa vyuo vikuu waanze kufundishwa maarifa ya kisasa
Pili tujaribu kuchukua wakufunzi kutoka vyuo Bora vya nje inaweza kuwa kwa mpango wa kubadilishana.
Tatu : tuangalie tunapokwama kwenye mitaala yetu
Nne: Muda wa mafunzo ya vitendo angalau uwe muda mrefu kuliko ule wa kusoma darasani ,, badala ya mtu kwenda field miezi 3 mwanafunzi aende mafunzo ya vitendo angalau miaka miwili.
Tano : ipo mifumo inayomruhusu mwanafunzi kujifunza zaidi ya kile anachopewa darasani Yani maswali yanayochochea upimaji na sio yanayomlazimisha mwanafunzi kukariri kitini Cha notes
Wakati mwingine ndio maana vijana wanaona mwajiri mzuri ni serikali maana wanalea watu kwa vikozi kadhaa mara kwa mara kuongeza ujuzi ila waajiri binafsi anataka mfanyakazi mzuri ila ambaye hajamtengeneza no wonder hauwezi kupata mtu mwenye uzoefu kazini.