Ni rural area mkuu maeneo ambayo makampuni ya simu na Fiber hayawezi fika.
Si Ethiopia tu hata ujerumani wametangaza Ku subsidize Satelite Connection kwenye Vijiji vyao.
Sikatai satelite ni njia Bora ya kutoa coverage Nchi ama bara zima Sababu ina cover eneo kubwa, ila sio replacement ya mobile data ama Fiber internet Sababu hizo zinakupa speed zaidi. Fiber ya zuku ina ping 2ms tu, mobile data kama Voda na Tigo most of time ping ni chini ya 20ms, voda napata 17ms local ping.
Low orbit satelite ni kubwa kushinda 4g, ping zake zipo baina ya 3g na 4g, advertised ping ni 20ms mpaka 40ms na pia Sababu unabadili satelite mara kwa mara kunakuwa na lag fulani sometime disconnection, early beta users wanareport wifi calling, gaming zinapata disconnection kila baada ya dakika kadhaa.
Hivyo wale wazee wa kudownload, kuangalia YouTube, kuchat, na mambo mengine ya kawaida kwao haitawasumbua.
Ila kama unaangalia mpira online, wazee wa Voip, Skype na viber, kubrowse internet, unacheza games online ama kitu chochote kinachohitajika real time response satelite inazingua.