Hubiri la tatu na la mwisho: Twendeni mpaka Gilgali(Oktoba) ili tuuimarishe ufalme(Urais) huko mara ya pili

Barnabas Mashamba

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2020
Posts
1,154
Reaction score
3,144
Andiko kuu: 1 Samweli 11:14

1 Samweli 11:14
Kisha Samweli akawaambia watu, Haya! Na twendeni mpaka Gilgali, ili tuuimarishe ufalme huko mara ya pili.

Usuli (Background)
Sura ya 9 na ya 10 ya kitabu cha kwanza cha Samweli (1 Samweli), inatutambulisha juu ya kupatikana mfalme wa kwanza kwa taifa la Israeli.

Mfalme huyo aliitwa mfalme Sauli. Na wakati harakati za kumpaka mafuta ya ufalme zikiwa zinaendelea, yeye mwenyewe hata alijiona kama mtu duni sana.
1 Samweli 9:21
[21]Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila ya Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?

Katika sura ya kumi (10), ndipo tunaona Sauli akitambulishwa rasmi kwa Waisraeli na kisha kusimikwa rasmi kama mfalme.

Kama ilivyo ada, huwezi kukubalika kwa watu wote, hata kwa Sauli punde baada ya kusimikwa rasmi kama mfalme, walipatikana watu waliokuwa hawamkubali na wanaotajwa hivi;
1 Samweli 10:27
[27]Walakini wengine wasiofaa kitu wakasema, Huyu je! Atatuokoaje? Nao wakamdharau, wasimletee zawadi.

Sura ya 11
Inaanza kwa tatizo katika Israeli Nahashi mwamoni alikwea ili apigane na Israeli hasa eneo la Yabesh-gileadi; na habari zilipomfikia mfalme Sauli, ili kuwakusanya waisraeli wote wawezao kwenda vitani, alifanya kama ifuatavyo.

1 Samweli 11:6-8
[6]Na roho ya Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana.

[7]Naye akatwaa jozi ya ng’ombe, akawakata-kata vipande, kisha akavipeleka vile vipande mipakani mwote mwa Israeli kwa mikono ya wajumbe, kusema, Ye yote asiyetoka nyuma ya Sauli na Samweli, ng’ombe zake watatendwa vivi hivi. Basi utisho wa BWANA ukawaangukia wale watu, wakatoka kama mtu mmoja.

[8]Naye akawahesabu huko Bezeki; Waisraeli walikuwa mia tatu elfu, na Wayuda thelathini elfu.


Kwa hiyo alipata uungwaji mkono wa watu 330 elfu

Baada ya kutembeza mkong'oto mkali kwa Waamoni.

[11]Ikawa, kesho yake, Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu; nao wakaingia katikati ya marago kwenye zamu ya asubuhi, wakawapiga Waamoni hata wakati wa jua kali; kisha ikawa wale waliosalia wakatawanyika, hata wasiachwe wawili wao pamoja.

Baada ya kichapo kikali, kuna watu bado walikuwa wanakumbuka siku ile ya kusimikwa rasmi kama mfalme namna watu walivyomdharau. Walipendekeza adhabu ifuatayo kwa waliomdisi mfalme Sauli siku ya kuapishwa kwake.

1 Samweli 11:12
[12]Ndipo watu walipomwambia Samweli, Ni nani yule aliyesema, Je! Huyo Sauli atatutawala? Walete watu hao, ili tuwaue.

Ilibidi Samweli aingilie kati kwa kusema
1 Samweli 11:13-14
[13]Lakini Sauli akasema, Hakuna mtu atakayeuawa leo, maana leo BWANA amefanya wokovu katika Israeli.

[14]Kisha Samweli akawaambia watu, Haya! Na twendeni mpaka Gilgali, ili tuuimarishe ufalme huko mara ya pili.



Hivyo kuelekea uchaguzi wa 2025, neno hili linatukumbusha mambo matatu:

(a) Uchaguzi ni nafasi ya upya wa agano

Israeli walikwenda Gilgali si tu kwa ajili ya kumthibitisha Sauli, bali pia kwa ajili ya kuonyesha utii wao kwa Mungu. Tanzania inapofanya uchaguzi wake, ni nafasi ya kutafakari: je, tumeishi kwa amani? Je, tumetenda haki? Je, tumemheshimu Mungu katika maisha ya kitaifa?

(b) Uongozi ni wito, si heshima binafsi

Sauli hakujiteua; alichaguliwa kwa mapenzi ya Mungu kupitia watu. Viongozi wetu pia hawaji kwa nguvu zao pekee, bali ni Mungu anayeinua. Ikiwa Rais Samia Suluhu Hassan ataendelea kupewa nafasi ya kuongoza awamu ya pili, ni kwa sababu Mungu amemwona anafaa katika wakati huu kwa ajili ya taifa.

(c) Amani ni ushindi wa pamoja

Baada ya Sauli kushinda vita, taifa lote lilikusanyika pamoja kwa furaha na mshikamano. Vivyo hivyo, baada ya uchaguzi, taifa letu linapaswa kusimama pamoja bila kujali tofauti za kisiasa. Ushindi wa kiongozi yeyote ni ushindi wa taifa, ikiwa tunaweka mbele haki, upendo, na mshikamano wa kitaifa.


Hitimisho

Wakuu, 1 Samweli 11:14 inatufundisha kwamba uchaguzi ni tendo la kiroho na la kijamii. Waisraeli walithibitisha uongozi wao kwa umoja na sherehe kwa Mungu. Tanzania pia ikifanya uchaguzi wake kwa haki na amani, tutaona baraka na mshikamano.


Maombi ya Kufunga

“Bwana, bariki Tanzania katika uchaguzi huu. Lete mshikamano na uongozi wenye hekima. Ikiwa ni mapenzi yako, mruhusu Rais Samia Suluhu Hassan aendelee kwa awamu ya pili. Utupe amani na mshikamano kwa jina la Yesu Kristo. Amina.”

Fahamu kuwa
Leo ndiyo mwisho wa majukumu yangu ya uhubiri mkuu wa taifa. Ninawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mlionipatia kipindi chote cha majukumu yangu hayo.

Mungu aendelee kuwabariki.

Barnabas Mashamba
Mhubiri mkuu wa taifa (mstaafu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…