Huduma ya Bima Mkononi kupitia Tigo Pesa, ni ushindi mawazo tunayotoa humu yanawezekana na pia yanatekelezeka Serikali ikidhamiria

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Tarehe 9/10/2020 kupitia Jukwaa la Siasa hapa JamiiForums, nilitoa pendekezo /ushauri kwa serikali juu ya namna gani wanaweza kutumia simu za mkononi kuanzisha Bima ya Afya na hata kugharamia elimu ya juu.

Serikali kupitia simu za mkononi, inaweza kukusanya fedha na kuanzisha Mfuko(Fund) wa kugharamia Bima ya Afya na Elimu ya Juu kwa Watanzania wote

Nilitoa hill wazo nikiamini ni jambo linalowezeka iwapo litafanyiwa kazi na wahusika. Takribani miezi miwili baadae (December mwaka jana), nilipokea sms kutoka Tigo juu ya huduma ya Bima Mkononi inayojulikana kama Bimamkononi Faraja Yako, ambapo baadae walinipia simu na kunipa maelekezo juu ya huduma husika na nikaridhika nikajiunga.

Wakati mimi nilipendekeza huduma hii itolewe kwa gharama ya shilingi 500 kwa mwezi, wao wanatoza shilling 4,000 kwa mwezi ambapo hukata kiasi hicho katika akaunti yako ya Tigopesa mara moja kila mwezi huku huduma hii ikidhaminiwa na MO na Resolution.

Huduma wanazotoa ni pamoja na Bima ya Maisha ambayo ni shilingi 1,000,000/=,Bima ya Ajali ambayo ni shilingi 3,000,000/= na Bima ya Matibabu ukilzwa ambayo ni shilingi 40,000/= kwa siku. Unaweza ku-access menu yao kwa kupiga *148*15 kupata maelezo zaidi.

Kwa maelezo yao, hata kama una Bima nyingine,wao watakulipa mradi tu uwasilishe vielelezo vinavyotakiwa kutoka hospitali uiolazwa.

Wakati mimi natoa hili wazo, sikujua kama huduma hii ilikuwepo au ilianza baadae ila nachotaka kusema hapa ni kuwa, mawazo tunayoyatoa humu yakifanyiwa kazi, tunaweza kabisa kutatuta baadhi ya matatizo makubwa ya hii nchi kama hili la watanzania wengi kutokuwa na Bima ya Afya na hili la kugharamia elimu ya juu.

Mimi nilieleza kwa kirefu sana na ilikuwa jukumu la wataalamu kupitia na kuboresha wazo lile na kulifanyia kazi. Sasa tuache wajanja wanaojua kutumia fursa kufanya biashaara, wapige pesa na sisi tukibaki kutegemea misaada na kukamuana kwenye kodi za kila aina kuendesha nchi.

Hata hivyo, natoa angalizo kuwa wakati wengine tumeamua kujiunga na huduma hii, serikali kama ina jambo iliweke wazi mapema tusije kuchangia kila mwezi alafu tukaja kuambiwa huduma hiyo haitambulika na vitu vingine vya aina hiyo na pia wanaotoa hii huduma tunawaasa kutimiza ahadi za kwa vitendo pale mwanachama atapohitaji kulipwa kulingana na makubaliono yaliyopo.

Vile vile napenda kuwashauri hawa watoa huduma hii waanzishe website maalamu kuhusu huduma hii ya Bima Mkononi kupitia Tigopesa, site itayotumika kutoa maelezo juu ya huduma hii, kujiunga online na hata kujibu maswali ambayo ni common badala ya kutegemea mawasiliano ya simu kusajili wanachana na kuelimisha wateja /wanachama.

Hongereni kwa ubunifu.
 
Mkuu, mbona ina vionjo kama vya QNET?!
 
Kumbe ni ya muda mrefu hivyo.Swala ni wao kuboresha ila bado ni jambo jema tu unless sio wasikivu na hawataki kubadika.
 
Kumbe ni ya muda mrefu hivyo.Swala ni wao kuboresha ila bado ni jambo jema tu unless sio wasikivu na hawataki kubadika.
Hapa nina madai kwao niliwasilisha vielelezo wavitakavyo lakini hawajanilipa kwa madai kuwa vina mapungufu.

1. Fomu ya kutoka hospitali haina nembo (alama/mchoro) ila ina jina la hospitali - wao wanataka yenye nembo. Hospitali (kituo cha afya) wanasema hiyo ndio fou yao rasmi, hawawezi kufuata sharti la mgonjwa na kumpa fomu tofauti

2. Wanataka fomu ya bima ya afya (NHIF) iwe na muhuri - hospitali wanasema muhuri wanaupiga pale wanapowasilisha madai kwa BIMA. Matumizi ya muhuri ni kwa ajili ya wao kuwasilisha madai NHIF sio kwa mgonjwa.

3. Nimetibiwa na Clinical Officer (CO). Kwenye fomu ya NHIF kuna mahali pa kujaza MCT namba, CO hawana hizo namba, hawajazi mahali hapo. tiGO Bima hawataki kukubali na wanataka pajazwe.

Kwa kifupi, ni wasumbufu na wenye konakona kulipa madai ilhali wako fasta kukata mkwanja. Unapotibiwa unahudumiwa kama wagonjwa wengine na sio kama mgonjwa mwenye tiGO bima kuwa utapata nyaraka tofauti na wagonjwa wengine katika hospitali hiyo.
 
Hapa nina madai kwao niliwasilisha vielelezo wavitakavyo lakini hawajanilipa kwa madai kuwa vina mapungufu...
Mimi binafsi nilijiunga nayo Bima Mkononi, lakini sikuwahi kupata uzoefu kutoka kwa mwenye bima hii aliyelazwa akaomba madai. Taarifa hii itanisaidia kuwauliza maswali ili nifanye maamuzi ya kuendelea au kusitisha
 
Je serekali haiwezi kulazimisha kila mwananchi kuchangia 1000 kwa mwezi kupitia huduma za kifedha kwa mitandao yote halafu huduma za afya zikawa bureeeeeee kabisa
Inaweza kabisa. Ni bora tukilazimishwa (kinyang'anyi kama hivyo) kuchangia vitu vitavyotusaidia moja kwa moja. Kwa mwezi serikali inaweza kukusanya shilingi Bilioni 20 kutoka kwa wananchi milioni 20.

Kama tunachangia kwa lazima REA na SGR ambazo hatufaidiki nazo moja kwa moja, tunaweza tu kuchangia hiyo 1000 kwa mwezi tukapata huduma na wao wakawa wametekeleza ilani zao.
 
Inaweza kabisa. Ni bora tukilazimishwa (kinyang'anyi kama hivyo) kuchangia vitu vitavyotusaidia moja kwa moja. Kwa mwezi serikali inaweza kukusanya shilingi Bilioni 20 kutoka kwa wananchi milioni 20..
Binafsi naliona kama hili ni jema kabisa kuliko kwenda kukata mabima yao unaambiwa 1.5ml mnyonge atapata wapi pesa hii uundwe mfumo ambao utalazimisha tu kukatwa fedha utake usitake hata ukiweka vocha tu kama ujalipa ikatwe tu. 1000*APROXIMATE lines mil 15 is a huge enough money na za maendeleo tutazipatia hapa hapa binafsi huuwa nalia sana na huduma za afya ni aghali sana kwa wanyonge
 
Hili wazo ni zuri sana. Viongozi wa Serikali wanaopita humu na hata watumishi wa kawaida wa Serikali walifikishe hili kwa wahusika, Wizara ya Fedha na Wizara ya Afya Tanzania lifanyiwe kazi.

Bilioni 15 kwa mwezi ni fedha nyingi, na vile wananchi wote hatuumwi kwa mara moja, nina imani wagonjwa watapata huduma safi kabisa za viwango vya kimataifa bila ya wananchi kuumia sana kifedha na kujenga chuki kwa serikali yao, vifaa tiba vitanunuliwa kwa wingi nk.

Viongozi chukueni mawazo haya na kuyaweka kwenye uhalisia, tutasogea sana.
 
Hapa nina madai kwao niliwasilisha vielelezo wavitakavyo lakini hawajanilipa kwa madai kuwa vina mapungufu....
Huu ndio upuuzi na urasimu usiotakiwa.Serikali iwamulike na ikiwezekana ichukue hatua vinginevyo bora kujitoa.
 
Moderator tunaomba hii mada muirudishe jukwaa la siasa wanakopita wanasiasa na ambao ndio decision makers wakubwa wa nchi.

Watu kukosa Bima ya afya ni tatizo kubwa sana nchi hii.Tulipe uzito jambo hili.
 
Wezi tu hawana tofauti na wale wa bima za magari ambao ni wasumbufu tu
Ni wasumbufu kwasababu serikali imewaacha wafanye watakavyo ila ikiwabana na kuwawekea sheria na taratibu za kuwabana zaidi, haya mambo yataisha.
 
Hii mada ingebaki jukwaa la siasa ingekuwa bora zaidi kwani ni rahisi kwa wanasiasa kuiona katika hilo jukwaa.
Hivi jukwaa la siasa linapatikanaje? Maana mimi toka baada ya marekebisho ya mwisho ya tovuti kufanyika, jukwaa hilo nimekuwa silipati na baada ya uchaguzi niliona limerejea lakini baadae tena nikawa silioni. Natumia browser sio application
 
Hivi jukwaa la siasa linapatikanaje? Maana mimi toka baada ya marekebisho ya mwisho ya tovuti kufanyika, jukwaa hilo nimekuwa silipati na baada ya uchaguzi niliona limerejea lakini baadae tena nikawa silioni. Natumia browser sio application
Mbona hata mini natumia browser(chrome) na ninaipata kama kawaida tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…