MSHINO
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,069
- 713
Napenda kuishauri serikali kuu kuzuia taasisi zake kuacha biashara ndogo ndogo kwani kufanya hivyo ni kuzuia kukua kwa biashara na wajasiliamali kwa ujumla hivyo kupunguza mzunguko wa pesa na kuikosesha serikali kodi. Mfano shirika la kusambaza maji Morogoro MOROWASA linalazimisha wananchi kununua vifaa vya kuunganishia maji yaani mabomba na viunganishi vyake kutoka MOROWASA.Iwapo mwananchi atafanya hivyo MOROWASA hawamuunganishi mteja maji japokuwa atakuwa amepewa ruhisa na michilo na MOROWASA. Imekuwa ikisababisha ukiritimba ambao unasababisha wananchi kuchelewa kupata huduma ya kuunganishiwa maji.
Kwa sasa ili mwananchi aweze kuunganishiwa maji anatakiwa kulipa gharama zifuatazo au Zaidi kulingana na umbali kutoka bomba kubwa:
- Vifaa 250,000.00
- Ada 50,000.00
- Ufundi 20,000.00
- Jumla 320,000.00
MOROWASA wameshindwa kusambaza maji sasa wameamua kufungua biashara ya hardware na kuuza vifaa vya ujenzi. Sehemu nyingi maji hayatoki. Mfano Kihonda, kiyegea, mkundi na nk. hakuna hudima za amaji japo morowasa wanaendelea na huduma ya kuuza vifaa.