Huduma ya polisi ku-trace simu ni hisani, kiofisi au bure?

Huduma ya polisi ku-trace simu ni hisani, kiofisi au bure?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kuna hii huduma ya ku trace simu hutolewa na polisi wapelelezi. Kama umepoteza simu au unamtafuta mtu fulani namba yake inakiwa traced kujua yupo wapi.

Utaratibu wa utoaji wa hii huduma umekaa kiwizi wizi sana. Hakuna utaratibu rasmi wa kiserikali. Ni kama mradi wa mtu binafsi au wa serikali iliyoparanganyika.

Yaani mnamalizana wewe na askari, hakuna invoice/bill wala EFD. Bei maelewano.

Nawataka jeshi la polisi na wizara ya mapolisi wanijibu kupitia vyombo mbalimbali vya habari;

1. Hii huduma ni bure? Kutokana na kwamba victim amepeleka jambo polisi apate msaada.

2. Hii huduma ni utashi wa polisi mpelelezi? Mnaelewana tu bei na kupeana pesa vichochoroni?

3. Wekeni wazi taratibu wa kupata hii huduma.

Haya maswali yajibiwe ndani ya masaa 72
 
Kuna hii huduma ya ku trace simu hutolewa na polisi wapelelezi. Kama umepoteza simu au unamtafuta mtu fulani namba yake inakiwa traced kujua yupo wapi...
Mimi nina shauri mwaka wa pili sasa. Nilipoeda kureport, nikamkuta mwanamama mmoja polisi akasema sis hatufanyagi tracking ya simu. Tutakupa loss report upate SIM Card nyingine, yaani urudishe namba yako.

Nilipomuwliza utaratibu ni upi maana nahitaji simu yangu, alisema basi andikia maelezo. Hadi leo hakuan kitu kimefanyika. na uwezo wa kutoa Rushwa sina.
 
Wizi tu huo na wabunge tunao wa kuhoji haya Bungeni ila wametulia tu watu wanapigwa
 
Na niaba ya jeshi letu, napenda kutoa taarifa hii kutokana na kijana mmoja anayejiita Okwi Bobani sunzu aliyeandika akituhumu jeshi letu pendwa kitengo cha intelligensia na cyber.

Mtu huyu hatujui kama ni kijana au mzee aliandika huko jamii forum, ila kwa kifupi natoa maelezo haya, ukiibiwa simu yako na kutoa taarifa kituo chochote ukionyesha vielelezo vyote muhimu, jeshi la polisi kupitia kitengo tajwa hapo juu kitakupa ushirikiano kuipata simu yako.

Tafadhali nenda kituo chochote kwa msaada zaidi ukiwa na vielelezo vyako vyote.

Asante kwa niaba.
 
Polisi inaendeshwa unprofessionally,sio hilo tu la ku_trace simu,ukipeleka kesi yako ukachukuliwa maelezo mlalamikaji, ikafunguliwa file,hata km suspects umewatajia,kinachofuata hapo ni utoe hela ndio washughulike na jambo lako.

Mgambo kufuata mtuhumiwa 10k.

Polisi kufuata mtuhumiwa na gari yao 20k+

Bora hz taratibu za mlalamika kujigharamia zikawekwa bayana,vinginevyo rushwa haitakoma.
 
vitu km hivi vilitakiwa kuwekwa wazi jamii inajua sio mtu unafahamu taratibu baada ya kupata tatizo, pia ukiweka wazi taratibu unapunguza mianya ya rushwa...wahusika wachukue hio km ushauri na si lawama au ukosoaji itasaidia kujenga imani, imani hujengwa kwa matendo banah sio kuhubiriana au kutishana
 
Kuna hii huduma ya ku trace simu hutolewa na polisi wapelelezi. Kama umepoteza simu au unamtafuta mtu fulani namba yake inakiwa traced kujua yupo wap...

Utafikiri hata watafutaji ni wao basi?

Aliimba jabali la Muziki

Dunia sasa imekwisha:
"si wanawake si wanaume" 🎼🎼

Angekuwapo leo angeimba:

"Si majambazi, si ma polisi" 🎼🎼
 
Hii issue imelalamikiwa na wengi sana ni kichochoro cha polisi kupiga hela.
 
Mimi nina shauri mwaka wa pili sasa. Nilipoeda kureport, nikamkuta mwanamama mmoja polisi akasema sis hatufanyagi tracking ya simu. Tutakupa loss report upate SIM Card nyingine, yaani urudishe namba yako. Nilipomuwliza utaratibu ni upi maana nahitaji simu yangu, alisema basi andikia maelezo. Hadi leo hakuan kitu kimefanyika. na uwezo wa kutoa Rushwa sina.
Niko na experience ya hizi kesi mara 2

Kikawaida ukiitaji simu yako basi utafungua shauri, ambapo utaandika maelezo utapewa RB na kupangiwa mpelelezi

Simu yangu ya 1 iliibiwa 2017 siku ipata mpaka leo na simu ya pili iliibiwa 2021 process ilikuwa ni ivyo ivyo pia sijaipata mpaka leo na mpelelez hajawah kunicheki kunipa mrejesho ....

My Note;

Tz hamnaga izi mambo za ku track simu zilizoibiwa binafsi naona ni kutupiga changa la macho tu wa Tz
 
Yaani mnamalizana wewe na askari, hakuna invoice/bill wala EFD. Bei maelewano.

Nawataka jeshi la polisi na wizara ya mapolisi wanijibu kupitia vyombo mbalimbali vya habari...
Mkuu huu ni mradi wa watu ndiyo maana watu wanasema kufanya kazi na form four failures ni shida, nitakupa mfano mmoja, kuna rafiki yangu aliibiwa simu maeneo ya Shoppers Plaza, Samsung S7 akaenda polisi wakasema wataifuatilia, siku moja wakampigia simu kuwa imeonekana kwenye mfumo inatumika Mlandizi, wakaomba pesa 50K akawapa, baada ya wiki wakampigia tena kuwa inatumika Mikumi awape fedha waende, akawapa, baada ya wiki akawapigia wakamwambia ameizima haipatikani, mmoja kati yao akavujisha siri kuwa kama simu ni ya thamani kubwa wakiikamata huwa wanaichukua inakuwa yao.
 
Unaona sasa,daah
 
Usitegemee kupata simu yako kwa hao jamaa.
Hii huduma ya kutrace kweli ipo nilishawahi shuhudia hapo oysterbay wana track simu.

Ila utaliwa hela sana ya mafuta na nauli hata wakiipata hawakupi bali wanaanza kula hela kwa yule aliyekamatwa ili wamalize kesi.

Polisi ni wezi na janja janja nyingi.
 
Kuna hii huduma ya ku trace simu hutolewa na polisi wapelelezi. Kama umepoteza simu au unamtafuta mtu fulani namba yake inakiwa traced kujua yupo wapi.

Utaratibu wa utoaji wa hii huduma umekaa kiwizi wizi sana. Hakuna utaratibu rasmi wa kiserikali. Ni kama mradi wa mtu binafsi au wa serikali iliyoparanganyika.

Yaani mnamalizana wewe na askari, hakuna invoice/bill wala EFD. Bei maelewano.

Nawataka jeshi la polisi na wizara ya mapolisi wanijibu kupitia vyombo mbalimbali vya habari;

1. Hii huduma ni bure? Kutokana na kwamba victim amepeleka jambo polisi apate msaada.

2. Hii huduma ni utashi wa polisi mpelelezi? Mnaelewana tu bei na kupeana pesa vichochoroni?

3. Wekeni wazi taratibu wa kupata hii huduma.

Haya maswali yajibiwe ndani ya masaa 72
Ni bure ila kumbuka kuna tujiviatu kupata vumbi kutokana na mitaa yetu kukosa tujilami.
 
Mkuu huu ni mradi wa watu ndiyo maana watu wanasema kufanya kazi na form four failures ni shida, nitakupa mfano mmoja, kuna rafiki yangu aliibiwa simu maeneo ya Shoppers Plaza, Samsung S7 akaenda polisi wakasema wataifuatilia, siku moja wakampigia simu kuwa imeonekana kwenye mfumo inatumika Mlandizi, wakaomba pesa 50K akawapa, baada ya wiki wakampigia tena kuwa inatumika Mikumi awape fedha waende, akawapa, baada ya wiki akawapigia wakamwambia ameizima haipatikani, mmoja kati yao akavujisha siri kuwa kama simu ni ya thamani kubwa wakiikamata huwa wanaichukua inakuwa yao.
Jamaa yangu wa karibu walimfanyia hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom