Bondpost
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 7,019
- 10,455
Ilinikuta mie mwaka juzi niliibiwa iPhone yangu nikareport nilijua wataitrace sababu niliactivate huduma ya "find my iPhone".Kuna hii huduma ya ku trace simu hutolewa na polisi wapelelezi. Kama umepoteza simu au unamtafuta mtu fulani namba yake inakiwa traced kujua yupo wapi.
Utaratibu wa utoaji wa hii huduma umekaa kiwizi wizi sana. Hakuna utaratibu rasmi wa kiserikali. Ni kama mradi wa mtu binafsi au wa serikali iliyoparanganyika.
Yaani mnamalizana wewe na askari, hakuna invoice/bill wala EFD. Bei maelewano.
Nawataka jeshi la polisi na wizara ya mapolisi wanijibu kupitia vyombo mbalimbali vya habari;
1. Hii huduma ni bure? Kutokana na kwamba victim amepeleka jambo polisi apate msaada.
2. Hii huduma ni utashi wa polisi mpelelezi? Mnaelewana tu bei na kupeana pesa vichochoroni?
3. Wekeni wazi taratibu wa kupata hii huduma.
Haya maswali yajibiwe ndani ya masaa 72
Jamaa ananiambia nimpe laki afanye hiyo kazi nikamwambia basi aache tu maana niliona atanibabaisha na mambo ya kitoto wakati unakuta alisomeshwa kozi ya wiki tu namna ya kutrace simu kimtandao Ila yeye anajiona Kama amekuwa IT guru.
Nilichofanya nikaanza kuitrace kwa laptop na jamaa wakajichanganya kutaka kuingiza password mpya ikaniletea namba ya jamaa ni Fundi Kariakoo.
Nikampigia nikamwambia naiona simu ipo hapo maeneo ya Tandamti street kwenye wauza simu na namba yako ninayo nikampiga biti jamaa akasema yeye ni Fundi ameletewa tu simu .
Nikapanga mtego tikakamata mwizi wangu kilaini sana dogo alikuja akijua simu imeshafunguliwa akaja tukamdaka kwakweli walinilipa gharama zangu na nusu ya pesa ya simu kwa usumbufu ndio tukamwachia dogo sio Fundi Ila Fundi polisi walimnywa hela mie nilikomaa na dogo.
Hakuna maajabu kwenye kutrace simu sema no muda tu inahitajika Ila polisi wamegeuza ni dili siku hizi na wanawajua wezi wa simu wakiiona wanaweza kukausha halafu anampigia ampe hela .
Polisi bana.