Huduma ya polisi ku-trace simu ni hisani, kiofisi au bure?

Kuna hii huduma ya ku trace simu hutolewa na polisi wapelelezi. Kama umepoteza simu au unamtafuta mtu fulani namba yake inakiwa traced kujua yupo wapi.

Utaratibu wa utoaji wa hii huduma umekaa kiwizi wizi sana. Hakuna utaratibu rasmi wa kiserikali. Ni kama mradi wa mtu binafsi au wa serikali iliyoparanganyika.

Yaani mnamalizana wewe na askari, hakuna invoice/bill wala EFD. Bei maelewano.

Nawataka jeshi la polisi na wizara ya mapolisi wanijibu kupitia vyombo mbalimbali vya habari;

1. Hii huduma ni bure? Kutokana na kwamba victim amepeleka jambo polisi apate msaada.

2. Hii huduma ni utashi wa polisi mpelelezi? Mnaelewana tu bei na kupeana pesa vichochoroni?

3. Wekeni wazi taratibu wa kupata hii huduma.

Haya maswali yajibiwe ndani ya masaa 72
Jamaa umeweka na masaa.Tusaidiane kujuwa mawili matatu,mimi si askari ni mwananchi ila kuna jamaa yangu alipotelewa na cmu akaenda kituoni akaambiwa tutaitrace lakini cku2 hakuna kuanza hatua wakat huo cm inazid kusonga mbele.Hatimaye jamaa akaamuwa kumchek jamaa kitaa akaitrace ikajulikana maeneo ilipo.Ishu kubwa kitengo kama kimekuwa chanzo cha mapato cha watu fulani.Umeibiwa cmu ili uipate uwe na hela na aliyeiba anaambiwa toa hela msala usiwe mkubwa mnajikuta wote mwizi na muibiwa mumempa askari hela.Ushaur jeshi la polisi liboreshe kitengo na kukisimamia kimaadili.
 
Kitaa gani hicho ulitrace bure tusaidie wenzako maana Kuna kipindi waliniibia simu nikakumbuka gharama nikaghahiri hata kufungua kesi
 
konstebo anamiliki kitochi ama tecno ,uniforms ana mwaka wa nne hajapata mgawo, apate Iphone macho matatu arudishe? thubutuuuu hiyo simu haya RPC wake hana , hapo mkizungumzia uzalendo siwaelewi kabisaaaaa, kiufupi makaro njaa sana ndio maana wana hasira tu akiona hata mtu anaendesha kigari chake amazing anauuuuuna.
 
Dah! inahuzunisha sana na inatia aibu kama mimi ningelikuwa polisi basi huu uzi na maoni yake yangefanya niachane na hiyo kazi.
 
Yaani inchi hii ni aibu kujitapa mbele za watu kwamba Mimi ni mtanzania..

Yaani muda wote watu wanawaza kuiba ,,
Sasa Jambo kama hilo la kutrack simu pia police wapewe pesa?

Hivi jukumu la police ni nn?
 
Kuna hii huduma ya ku trace simu hutolewa na polisi wapelelezi. Kama umepoteza simu au unamtafuta mtu fulani namba yake inakiwa traced kujua yupo wapi.

Utaratibu wa utoaji wa hii huduma umekaa kiwizi wizi sana. Hakuna utaratibu rasmi wa kiserikali. Ni kama mradi wa mtu binafsi au wa serikali iliyoparanganyika.

Yaani mnamalizana wewe na askari, hakuna invoice/bill wala EFD. Bei maelewano.

Nawataka jeshi la polisi na wizara ya mapolisi wanijibu kupitia vyombo mbalimbali vya habari;

1. Hii huduma ni bure? Kutokana na kwamba victim amepeleka jambo polisi apate msaada.

2. Hii huduma ni utashi wa polisi mpelelezi? Mnaelewana tu bei na kupeana pesa vichochoroni?

3. Wekeni wazi taratibu wa kupata hii huduma.

Haya maswali yajibiwe ndani ya masaa 72
Hata ukiripoti Polisi hamna wanachofanya, nadhani kitengo cha cyber crime wako bize kutafuta matumizi mabaya ya marumizi ya mtandao ili washitakiwe.
 
Dah! inahuzunisha sana na inatia aibu kama mimi ningelikuwa polisi basi huu uzi na maoni yake yangefanya niachane na hiyo kazi.
Lakini hawa watu wasomi wetu wanaokaa kila mara wanawalalamikia Polisi na kudai kuwa Polisi hawajasoma, wao ndiyo wamesoma; je wao huko maofisini kwao kweli wanafanya inavyotakiwa kufanyika? Mbona kila mahali ni shida tupu? Yupi sasa ni bora kati yao na Polisi? Mimi naona bora Polisi kuliko mtu anayejidai msomi halafu bado anafanya mazito kuzidi hata wale anaowalalamikia
 
Yaani inchi hii ni aibu kujitapa mbele za watu kwamba Mimi ni mtanzania..

Yaani muda wote watu wanawaza kuiba ,,
Sasa Jambo kama hilo la kutrack simu pia police wapewe pesa?

Hivi jukumu la police ni nn?
Kama kweli tuhuma hizi ni za kweli kwamba Polisi wanaiba, basi uwezekano mkubwa ni kwamba tuliowafundisha ni sisi raia; wanajaribu nao kuiga namna sisi raia tulivyo ili nao waweze kuafana na sisi. Hii nchi viongozi wetu kila siku wanalalamika hatufanyi kama wanavyotuelekeza, lakini bado kila Mtanzania naye pia analalamika; sasa unajiuliza maswali kwamba hawa viongozi wetu wanaotulalamikia kila siku, wanaongoza watu kutoka Kenya au Malawi na si Tanzania?
 
Hata ukiripoti Polisi hamna wanachofanya, nadhani kitengo cha cyber crime wako bize kutafuta matumizi mabaya ya marumizi ya mtandao ili washitakiwe.
CYBER CRIME ni kitengo kizito mno na kinachoshughulika na maswala nyeti mno ya nchi, watu wanasota kwa kusomea, na hivyo hakiwezi kujikita kwenye kushughulika na maswala haya madogo madogo ya PILFERAGE za smartphones za watu mitaani
 
Kama kweli tuhuma hizi ni za kweli kwamba Polisi wanaiba, basi uwezekano mkubwa ni kwamba tuliowafundisha ni sisi raia; wanajaribu nao kuiga namna sisi raia tulivyo ili nao waweze kuafana na sisi. Hii nchi viongozi wetu kila siku wanalalamika hatufanyi kama wanavyotuelekeza, lakini bado kila Mtanzania naye pia analalamika; sasa unajiuliza maswali kwamba hawa viongozi wetu wanaotulalamikia kila siku, wanaongoza watu kutoka Kenya au Malawi na si Tanzania?
Kuna mazingira ya kulazimishwa utoe rushwa,

Maana kama una mkono mfupi husaidiwi ,
unadhani nini kitatokea?
 
Siku moja nilienda kituo Cha polisi kumcheki jamaa yangu (ambaye ni polisi pia), kwa muda niliokaa pale niligundua raia wanaonewa saaana na polisi.

Yani mtu anajazwa mteru Kama kapindua nchi vile akija kurudishwa road tayari ashapigwa kiasi kadhaa Cha pesa. Nilicheka sana na kuonea watu huruma.
 
Lakini hawa watu wasomi wetu wanaokaa kila mara wanawalalamikia Polisi na kudai kuwa Polisi hawajasoma, wao ndiyo wamesoma; je wao huko maofisini kwao kweli wanafanya inavyotakiwa kufanyika? Mbona kila mahali ni shida tupu? Yupi sasa ni bora kati yao na Polisi? Mimi naona bora Polisi kuliko mtu anayejidai msomi halafu bado anafanya mazito kuzidi hata wale anaowalalamikia
hii nayo ni kweli
 
Back
Top Bottom