Huduma ya polisi ku-trace simu ni hisani, kiofisi au bure?

Ilinikuta mie mwaka juzi niliibiwa iPhone yangu nikareport nilijua wataitrace sababu niliactivate huduma ya "find my iPhone".

Jamaa ananiambia nimpe laki afanye hiyo kazi nikamwambia basi aache tu maana niliona atanibabaisha na mambo ya kitoto wakati unakuta alisomeshwa kozi ya wiki tu namna ya kutrace simu kimtandao Ila yeye anajiona Kama amekuwa IT guru.

Nilichofanya nikaanza kuitrace kwa laptop na jamaa wakajichanganya kutaka kuingiza password mpya ikaniletea namba ya jamaa ni Fundi Kariakoo.

Nikampigia nikamwambia naiona simu ipo hapo maeneo ya Tandamti street kwenye wauza simu na namba yako ninayo nikampiga biti jamaa akasema yeye ni Fundi ameletewa tu simu .

Nikapanga mtego tikakamata mwizi wangu kilaini sana dogo alikuja akijua simu imeshafunguliwa akaja tukamdaka kwakweli walinilipa gharama zangu na nusu ya pesa ya simu kwa usumbufu ndio tukamwachia dogo sio Fundi Ila Fundi polisi walimnywa hela mie nilikomaa na dogo.

Hakuna maajabu kwenye kutrace simu sema no muda tu inahitajika Ila polisi wamegeuza ni dili siku hizi na wanawajua wezi wa simu wakiiona wanaweza kukausha halafu anampigia ampe hela .

Polisi bana.
 
Hii inafanya watu wabuni mbinu halamu za kumaliza a na wezi!!!
 
Kwamba polisi hawana mawasiliano na polisi wenzao wa maeneo mengine hadi waende wao?

Hilo la kuipata simu na kuitumia wao au kuiuza hata mimi niliambiwa na polisi mwenzao. Kumbe ndio maana utawaona na simu kali kali kumbe wameiba.
 
Asante Afande
 
Hii kazi ingekua inafanywa na makampuni ya simu make wao ni rahisi sana au tcrc ili iwe rahisi. Ukishapoteza unaenda kuripoti polisi unapewa RB unaipeleka kwenye kampuni husika ingesaidia kuondoa huu uhuni wa polisi wetu
 
Yaani kufanya kazi na 4m four failure ni shida sana
 
Daaa kirahisiii ivyoooo tyuuuu?
 
Wapoo, semaaa ndo ivyooo
 
Uzuzu huu utatutoka lini ninyi working class?,wote humu tunaelewa in black &white kuwa jeshi letu la police hawana uwezo wa tracking simu iliyoibiwa/kupotea lakini bado tunao tu, service providers walitakiwa wawe na uwezo wa ku block simu zilizopotea/kuibiwa, na ku swap sim card inatakiwa uende kwa service provider wako na ID,na proof of address, na kumbuka watu au sehemu ulizowasiliana kwa kutumia simu yako(kama 5 hivi),tuna police hawawezi hata to take statements, to secure crime scene na sitoshangaa Ile gari iliyopata ajali na dereva kufariki pale korogwe bado ipo pale na jeshi letu limeshindwa kabisa kumtambua marehemu, tuna special unit moja tu ndani ya police wetu, kukimbizana na wapinzani wa kisiasa, na wasiojulikana tu
 
ASANTE STUDIO.

Hili tatizo lilinikuta asee ila nilishindwa niliwekeje ili nieleweke.
MAJIBU TAFADHALI
 
Kiukweli hii huduma ya kutrack simu iliyoibiwa police hawatendi haki, nilibiwa simu nikaripoti police, Toka mwezi wa Tano mwaka Jana 2021, mpaka leo, nilifatilia nikachoka, kwa Nini kisipelekwe sehemu nyingine
 
Nikiwa kitaa Brother akatoka job akaingia Gheto lake pale maeneo ya Mbezi akagundua kuwa kaibiwa vitu simu,TV,king'gamuzi pamoja na laptop akaenda Polisi kufungua kesi kweli kesi ikafunguliwa pale Gogoni .Game ikaanza Tukio likakaguliwe gari la Polisi Bovu tena halina wese hivyo gari hakuna Mzee Yule Mpelelezi akawsha gari yake tukaondoka akaingia sheli akaweka mafuta ya Tsh 15000/= tukafika Eneo la tukio akakagua Hilo Eneo Kisha akauliza stationary Ipo wapi akachukua form moja ya maelezo aliyokuja nayo akaenda kutoa photocopy Kama sita hivi yaani 1200/= Kisha akaanza kuandika maelezo ya majirani wa Eneo lilipo tukio Kisha akapiga picha jinsi Eneo la tukio lilivyo na akachorachora na kuchukua Alama vidole Kisha akasema kesho tuonane huko kituoni Kisha akaondoka kurudi kazini kwake. Siku iliyofuta akasema ameandika barua kwenda mitandao ya simu hivyo anapeleka barua huko mitandaoni akaingia garini kwake akaondoka kupeleka barua na baadae akarudi na kusema barua ameshapeleka na zimegongwa muhuri tukaziona akatueleza pia anaendelea na upelelezi wa kawaida na akigundua Nani kafanya majibu ya Mtandao hayatakuwa na Muhimu Sana Ila akishindwa huko atategemea Sana mtandaoni .Kiukweli ilipita miezi mitatu bila Majibu kutoka mtandaoni yule Mpelelezi akasema Kama unataka tufanikiwe hili Jambo tuwape pesa kidogo Watu wa Mtandao ili barua ijibiwe kweli tulutoa Mzee wiki tu Simu ikasomeka Mapinga Bagamoyo jamaa wakaenda akakamatwa aliyokuwa anaitumia naye akaeleza alikuipata ni Mbezi kauziwa na fundi kufika kwa fundi naye akamtaja kibaka aliyemuuzia naye kibaka baada kukamatwa akataja alipouza vitu vingine hivyo tukapata vyote . Hivyo kwakuwa sisi tulitaka vitu vyetu akasema subiri kesi iishe ndipo tukasubiri miezi Kama minne kesi ikaisha jamaa kafungwa tukapewa vitu vyetu.
Sasa najiuliza
1 Je kwanini Watu wa mitandao ya simu hawajibu barua kwa haraka mpaka wapewe hela?
2.Kwanini serikali isiwe na utaratibu wa kuwafikia wateja wa mitandao bila kulia Shida Mitandao ya simu?
4.Kwanini Kule Polisi inamlazimu Mpelelezi kutumia gharama zake kupeleleza kesi Kama pale nilipoona askari anatumia gari yake kukagua Eneo la tukio pia kupata stationary ?
5.Kama Mpelelezi hana gari hizo gharama za upelelezi anazibeba Nani maana kesi ni nyingi wapelelezi ni Wengi lakini Polisi gari moja Tena Bovu na halina mafuta?

Kiukweli nimewaza kwa Sauti nakumbuka hiyo Idara Mara ya Mwisho kupewa magari ni Enzi za Kikwete nimeshindwa hata kulalamika kwanini huwa wanachelewa kufika maeneo yatukio.

Kabla hatujawalaumu serikali ifanye mapinduzi ya kutosha panatia kinyaa hata viti vya kukaa Sisi tunaotaka huduma hakuna.
 
Hawa jamaa ukifika pale ukatoa details zako wanachukua, aafu ukishindwa kutoa Mchongo pesa wanaitrack wanaichukua wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…