Huduma ya RITA inatia mashaka, nawashauri wajitathimini

Huduma ya RITA inatia mashaka, nawashauri wajitathimini

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Nina mashaka makubwa sana na uwezo wa watendaji RITA hususani kitengo cha usajili wa vizazi na vifo!

Ukichunguza kwa makini vyeti 8 kati ya 10 vilivyotolewa na RITA lazima utakuta dosari au changamoto!

Miongoni mwa dosari hizo ni kama zifuatazo!
1. Mteja anaweza kuwa anaitwa ABDALLA lakini cheti usishangae wakakitoa kikisomeka ABDULLA
2. Mteja anaweza kuwa amezaliwa 1969 lakini usishangae cheti wakakitoa kinasomeka 1996
3. Mteja anaweza kuwa anaitwa KHANIFA lakini usishangae kabisa kukuta wametoa cheti kinachosomeka HANIFA
4. Vyeti vingi wasipokosea jina la mtoto basi watakosea jina la wazazi iwe either baba au mama kisarufi, kiufupi ukichukua cheti RITA ukakiangalia kwa makini hukosi kasoro!

Ukiwauliza kwanini mnakosea watakujibu wao wanazingatia viambatanisho! Lakini hata pale mteja atathibitisha viambatanisho kuwa sahihi lakini bado hukosea vilevile

Hiii inatia sana mashaka uwezo wa watoa huduma hao huenda utaratibu wao wa ajira Rita hauna viwango stahiki!

Taasisi nyeti kama RITA Haikupaswa kabisa kuwa hivi karne 21

Kwa makosa wanayoyafanya kwenye Vyeti ingekuwa oparesheni ya afya ya mwili basi 80% ya wateja wao wangekuwa na vilema kwa makosa wanayoyafanya RITA.

Nashindwa kuelewa kwanini wameshindwa hata kuweka CUSTOMER PREVIEW ili mteja athibitishe taarifa kabla hawaja PRINT CHETI.

Mbali na cheti,
kwanza ukitaka kujua huduma ni mbovu hata ukifika ofisi zao pale jengo la RITA TOWER DSM utaona walivyo too disorganized (very local)

Mtakumbuka Kwa wale mliofika kwenye maonesho pale sabasaba mtakubaliana na Mimi kuwa wale wahudumu pale walionyesha kuwa na uelewa mdogo sana kichwani (dizaini kama RITA wanaajili vishoia kwenye idara kwenye baadhi ya idara)

Hata banda lao kwenye maonesho ya sabasaba lilitoa ujumbe wa huduma mbovu, "Lilikuwa banda bovu kuliko mabanda yote pale sabasaba!

Siamini hata kama RITA Wana mkurugenzi maana mambo yao yapo vululuvululu tu bora liende!

Inje ya huduma Jengo la RITA TOWER ni zuri sana na refu lakini pia inashangaza sana katika LIFT 4 zilizopo lakini inashangaza zinazofanya kazi pale ni mbili tu!

Hivyo siyo ajabu kabisa kwenye jengo la RITA mteja akasubiri LIFT kwa nusu saa!

Kiufupi huduma iliyopo sasa ukitaka kwenda RITA AGANA NA NYONGA! ile panda shuka ya ngazi kwa miguu.
 
Nataka nifuatilie Cheti cha Kifo cha mdogo wangu,sijui hata nianzie wapi[emoji134]ningepata mfanyakazi wa RITA akanisaidia kwa uharaka kisha nikampoza ningefurahi sana,tafadhali Matapeli msidhani hii ni fursa ya kunipigia,ooohh
 
Taasisi zote za serikali kwenye kuandika taarifa za mtu lazima watakosea....
Hata uwaachie taarifa zako siku ukienda chukua kitambulisho au cheti nk,dosari lazima itakuwepo
Wanauzembe fulani na kufanya kazi kwa mazoea
Mpe taarifa zako mzungu sasa hutaona kasoro

Ova
 
Wanaajili watu wasiyo sahihi
 
Nataka nifuatilie Cheti cha Kifo cha mdogo wangu,sijui hata nianzie wapi[emoji134]ningepata mfanyakazi wa RITA akanisaidia kwa uharaka kisha nikampoza ningefurahi sana,tafadhali Matapeli msidhani hii ni fursa ya kunipigia,ooohh
Bahati yako tumestaafu hizo shuguli za madokoma,ningekula hela yako kma upepo(joke)

We nenda Rita si una kibali cha mazishi,na taarifa za marehemu
Huna haja ya kumpoza mtu,we ikingia
Hapo kifua mbele tu

Ova
 
Taasisi nyingi za kiserikali zinafanya kazi kwa mazoea na kivivu sana. Huduma zinazotoka ni bora liende.

Niliwai enda taasisi fulani kufata fomu fulani unaambia fomu huwa inatolewa mwisho saa 4. Utasema baada ya saa 4 iyo fomu inakua sio part ya ofisi
 
Nataka nifuatilie Cheti cha Kifo cha mdogo wangu,sijui hata nianzie wapi[emoji134]ningepata mfanyakazi wa RITA akanisaidia kwa uharaka kisha nikampoza ningefurahi sana,tafadhali Matapeli msidhani hii ni fursa ya kunipigia,ooohh
Kupata utapata shida usahihi wa taarifa ndo majanga
 
Apply online wewe,huko tulishatoka mda mrefu
Death Certificate inaombwa online au??mimi nataka mtu wa ndani RITA nimpe majina ashughulikie fasta kesho nikachukue nimpoze ya Wine,habari za nenda rudi kesho au keshokutwa sijui hakuna network sina muda kabisa
 
Nataka nifuatilie Cheti cha Kifo cha mdogo wangu,sijui hata nianzie wapi[emoji134]ningepata mfanyakazi wa RITA akanisaidia kwa uharaka kisha nikampoza ningefurahi sana,tafadhali Matapeli msidhani hii ni fursa ya kunipigia,ooohh
Nenda halmashauri mtafute muhasibu wa halmashauri Ela ya soda ten tu unskipata siku hio hio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati yako tumestaafu hizo shuguli za madokoma,ningekula hela yako kma upepo(joke)

We nenda Rita si una kibali cha mazishi,na taarifa za marehemu
Huna haja ya kumpoza mtu,we ikingia
Hapo kifua mbele tu

Ova
Mtu alifia kijijini huko hakuna hata Dispensary wala Ofisi ya Serikali ya Kijiji hiko kibali cha Mazishi kitatoka wapi!!!kuhifadhi mwili tu usiharibike inabidi mtandaze chumvi chini na majani kwa juu kisha mnaulaza mwili
 
Taasisi zote za serikali kwenye kuandika taarifa za mtu lazima watakosea....
Hata uwaachie taarifa zako siku ukienda chukua kitambulisho au cheti nk,dosari lazima itakuwepo
Wanauzembe fulani na kufanya kazi kwa mazoea
Mpe taarifa zako mzungu sasa hutaona kasoro

Ova
Na sana sana ni wadada ndio wenye changamoto kubwa ukimkuta asubuhi ofisini kachoka hata kabla ya kuanza kazi mara kuchat mara kubinua midomo yani tabu tupu na anajua Huna cha kumfanya kama ajila keshapata tena Serikalini
 
Back
Top Bottom