Huduma ya RITA inatia mashaka, nawashauri wajitathimini

Nataka nifuatilie Cheti cha Kifo cha mdogo wangu,sijui hata nianzie wapi[emoji134]ningepata mfanyakazi wa RITA akanisaidia kwa uharaka kisha nikampoza ningefurahi sana,tafadhali Matapeli msidhani hii ni fursa ya kunipigia,ooohh
Omba online tu!! Tena simple kama unakibali cha Mazishi tu
 
Kuna kaukweli niliwahi kumsindikiza jirani yangu, aisee alizungushwa hadi sio poa na kuna muhudumu mmoja hivi ana majibu ya nyodo
 
Taasisi nyingi za kiserikali zinafanya kazi kwa mazoea na kivivu sana. Huduma zinazotoka ni bora liende.

Niliwai enda taasisi fulani kufata fomu fulani unaambia fomu huwa inatolewa mwisho saa 4. Utasema baada ya saa 4 iyo fomu inakua sio part ya ofisi
Tabu kwelikweli
 
Kila mtu akague Vyeti vyake kwa makini majina ya mama na baba na tarehe kama viko sahihi shukuru Mungu
 
Kuna kaukweli niliwahi kumsindikiza jirani yangu, aisee alizungushwa hadi sio poa na kuna muhudumu mmoja hivi ana majibu ya nyodo
Huyo lazima atakuwa wakike mimi nimemkariri mpaka sura na kuna mshikaji wangu hivyo hivyo alizinguliwa na muhudumu huyo.
 
Kuna kaukweli niliwahi kumsindikiza jirani yangu, aisee alizungushwa hadi sio poa na kuna muhudumu mmoja hivi ana majibu ya nyodo
Ndio maana mimi nilitumia njia ya mchongo kupata cheti cha kuzaliwa sikupenda kuzungushwa na kunyenyekea kama unaomba uhai ,nilimpa mtu tangazo pamoja na misimbazi kadhaa wiki tu kila kitu tayari hakuna matata.
 
Unavyoona hii njia ni suluhisho?
 
kumbe unafahamu milolongo yao
 
Unavyoona hii njia ni suluhisho?
Hapana ,ila niliokoa muda tu na kuzungushana na sikufanya janja janja sababu kiambatanisho cha kupata cheti nilikuwa nacho .
 
Walikosea jina la mwanangu Sina haja hata kurudi Tena nikifikiria usumbufu hi nchi ya kipumbavu sana
 
Back
Top Bottom