Johnson Yesaya
Member
- Jan 1, 2013
- 21
- 31
1. 0 UTANGULIZI.Habari zenu watanzania na wananchi wenzangu wa nchi yetu pendwa ya Tanzania? Nawasalimu nikiwa na furaha kubwa sana na nikiwa na lengo la kuchangia mawazo yangu kwaajili ya kuboresha zaidi huduma za serikali dhidi ya wananchi wa Tanzania ambao ndio sisi (Mimi na Wewe). Wengi tunafahamu kwamba, sisi kama wananchi wa Tanzania, tunahitaji huduma mbalimbali kutoka serikalini. Huduma tunazohitaji zaweza kuwa Maji, Umeme au Nishati Zingine, Elimu, Barabara, Vituo vya afya, Usalama (Polisi na Jeshi), miundo mbinu mingine kama reli, viwanja vya ndege n.k Hivyo vyote ni muhimu, lakini mimi nahitaji kujielekeza zaidi katika huduma kama Huduma za Usajili na Utambuzi kwa mfano Usajili wa vyeti vya kuzaliwa, ndoa na vifo; Usajili wa vyeti vya umiliki wa ardhi na mali; Usajili wa vitambulisho vya taifa; Usajili wa biashara na kampuni; Leseni na vibali vya biashara au leseni za udereva na leseni zote zingine; Usajili wa ardhi na utoaji wa hati miliki na vibali vingine pamoja na barua za serikali za mitaa n.k.
Mimi nadhani huduma kama hizi, hazina haja ya mwananchi kuacha shughuli au biashara yake na kwenda kupanga foleni katika ofisi ya umma kwa muda mrefu na wakati mwingine kwa siku kadhaa. Serikali itengeneze mfumo mzuri zaidi au iboreshe huu uliopo (e-goverment) ili uweze kufanya kazi vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Mifumo mingi ya Tehama/Mtandao ya serikali ni ya kusuasua sana japokuwa kuna baadhi ambayo inafanya kazi vizuri lakini si kwa kiwango kile ambacho tunatamani Tanzania ya baadae ifike.
2.0 MAANA YA TEHEMA/MTANDAO NA HISTORIA YA MATUMIZI YAKE TANZANIA
Tehama, ambayo ni ufupisho wa, "Teknolojia ya Habari na Mawasiliano". Inajumuisha matumizi ya vifaa vya elektroniki na programu za kompyuta kwa lengo la kusambaza na kuhifadhi taarifa. Teknolojia hii inajumuisha kompyuta, simu za mkononi, mitandao ya kompyuta, intaneti, programu za kompyuta, na mifumo mingine ya mawasiliano. Mtandao, kwa upande mwingine, ni mfumo wa kompyuta unaounganisha vifaa mbalimbali kwa kutumia mawasiliano ya elektroniki.
Tanzania ilianza kujitayarisha kuingia katika matumizi ya utoaji wa huduma za kiserikali mtandaoni mwaka 2012 wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya nne ya Dkt Jakaya Mrisho Kikwete. Lakini mfumo huo ulianza kufanya kazi rasmi miaka ya 2015 wakati wa serikali ya awamu ya Tano ya Marehemu Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kutungwa sheria kadhaa kama sheria ya makosa ya mtandao ya 2015 na sheria ya serikali mtandao ambazo zililenga kuulinda na kuuwezesha mfumo huo kufanya kazi hasa kudhibiti uhalifu mtandaoni na kulinda taarifa binafsi za watu.

Chanzo : e-goverment
Mpaka sasa mfumo huu upo lakini kuna udhaifu mkubwa na miundo mbinu yake haikidhi uhitaji wa watumiaji wake hasa watanzania wengi ambao sio wataalamu sana wa TEHAMA.
3.0 MATATIZO YALIYOPO KWA SASA KATIKA MFUMO WA SERIKALI MTANDAO ULIOPO.
Mifumo hii ina matatizo katika ufanyaji kazi wake, haieleweki, inachukua muda mrefu kufunguka na inakuwa na hitilafu mara kwa mara na kuathiri huduma kwa mwananchi na kwa kiasi fulani kuathiri pato la serikali na
watu binafsi. Mfano wa mfumo ulioleta shida hivi karibuni ni mfumo wa ajira wa jeshi la polisi. Jeshi la polisi lilitangaza ajira na kuruhusu vijana wa kitanzania kuomba ajira kupitia mfumo wa ajira <ajira.tpf.go.tz>. Lakini waombaji wakakumbana na tatizo kubwa ambapo mfumo ulishindwa kupokea maombi na waombaji wengine wakadai kuwa mfumo hautambui namba zao za NIDA n.k. Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ikalazimika kuongeza muda wa maombi mpaka tarehe 26 mwezi huu wa tano.
Chanzo : Jamii Forums.
Lakini ushahidi mwingine wa matatizo ya mifumo iliyopo ni kupitia ripoti ya CAG ya mwaka 22/23 ambapo ripoti hiyo ilibainisha kuwa mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya uvuvi ulikuwa ukitoza ada ya leseni ya asilimia 50 kwa leseni mpya kwa kuzichukulia kama leseni za zamani zinazohuishwa badala ya ada halisi ya leseni mpya. Hii inaathiri mapato kwa serikali.
Chanzo: Jamii Forums
4.0 VYANZO VYA MATATIZO KATIKA MFUMO / MAMBO YA KUREKEBISHA
Mifumo ya Tehama ya serikali ya Tanzania inakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo zinafanya iwe mizito kufunguka, kutopatikana, na kusumbua watumiaji. Sababu moja kubwa ya tatizo hili ni miundombinu duni ya teknolojia. Kwa mfano, matumizi ya "shared servers" au tunza data za kuchangia ambapo huduma nyingi za serikali zinategemea seva moja, husababisha mzigo mkubwa na kusababisha mifumo kufanya kazi polepole au kutopatikana kabisa wakati watumiaji wengi wanapokuwa wanautumia mfumo huo. Pia, "bandwidth" ambao ni uwezo wa mfumo kuruhusu kiwango kikubwa cha taarifa kuwasilishwa na kuweza kuchakatwa bila shida yoyote. Mifumo mingi ya serikali (nadhani kwa kuwa sipo kwenye mifumo hiyo), ina bandwidth ndogo hivyo inapopata watumiaji wengi kwa wakati fulani hushindwa kufanya kazi.
Sababu nyingine ni ukosefu wa uwekezaji wa kutosha katika teknolojia za kisasa na matengenezo ya mifumo iliyopo. Mifumo mingi ya Tehama inayotumiwa na serikali inaweza kuwa ya zamani na haiwezi kuhimili idadi kubwa ya watumiaji au kiasi kikubwa cha data.
Ili kuondoa tatizo hii, serikali inapaswa kuwekeza zaidi katika matumizi ya seva zinazojitegemea (dedicated servers) badala ya seva za pamoja (shared servers) ili kupunguza mzigo na kuboresha utendaji wa mifumo. Pia kuna haja ya kuongeza upana wa mtandao (bandwidth) ili kuhakikisha mifumo inaweza kuhudumia watumiaji wengi kwa wakati mmoja bila matatizo. Pia, serikali inapaswa kuwekeza katika teknolojia za kisasa na kuhakikisha mifumo ya Tehama inaboreshwa na kufanyiwa matengenezo mara kwa mara.

5.0 HITIMISHO / FAIDA ZA MATUMIZI YA TEHAMA KATIKA KUTOA HUDUMA ZA KISERIKALI
Faida ya kwanza ni kupunguza rushwa, ulazima wa kwenda katika ofisi za umma na kukutana kwa watu ni chanzo cha watumishi wa umma kupata sababu za kuomba rushwa. Watu wakiweza kujihudumia wenyewe kupitia mifumo, rushwa itapungua kwa kiasi kikubwa. Faida ya pili ni kupunguza matumizi ya serikali katika uendeshaji wa ofisi zake. Serikali haitahitaji kukodi au kujenga majengo makubwa kuweka samani kwaajili ya wageni katika ofisi, hii itaokoa fedha nyingi ambazo zitaelekezwa katika maendeleo ya wananchi. Faida ya tatu ni kupunguza lugha mbaya na kero wanazopata wananchi kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma na pia hivyo hivyo kupunguza lugha mbaya ambazo watumishi wa umma wanaweza kuzipata kutoka kwa baadhi ya wananchi.
Kwa kumalizia, niseme ninaipenda sana Tanzania na ninataka iwe bora zaidi kuliko sasa.

Upvote
4