Huduma za kufanyiwa mchakato wa hati, kufanyiwa uthamini (Valuation) na masuala yote ya ardhi

Mkuu,hujanambia gharama ya kupima
Gharama ya kupima mkuu haiko fixed..Inategemeana na baadhi ya mambo.Nitumie PM kiwanja kilipo na ukubwa wake then ntakupa makadirio ya bajeti ya kupima
 
Wewe mleta mada taaluma yetu yas Ardhi na Uthamini huruhusiwi kujitangaza hivi. Unaonekana kanjanja au hujui ninni maana ya taaluma yetu na miiko yake. Ni unprofessional so futa huu ujinga. Uzuri umeweka namba yako ntakufuatilia VRB nikuone na nikufunze maana ya taaluma yetu. Pole

Hasira za nini ndugu?
Kujitangaza katika misingi ipi?
Makampuni mbalimbali yanayofanya kazi za kupima na kupanga miji yanajitangaza.

Andika kwenye Google search kampuni za kupima ardhi Tanzania au Dar es salaam. Je walioko kwenye mtandao si matangazo hayo? Wamemwandikia nani huko?
Chuo cha ardhi Morogoro kipo kwenye mtandao na moja ya kazi kinachoonyesha kufanya ni kupima ardhi na mipango miji. Je hao hawajatangaza?

Kama mnang'ang'ana na sheria na policy kandamizi/kama zipo, ndo maana kazi hizi zinashindwa kufanikishwa.

Uhitaji wa watu kufanya matumizi kwenye ardhi uko juu sana. Nyinyi mmejifungia kwenye maofisi bila kuwafikia wananchi kutatua matatizo yao na kuwapa elimu ya jinsi ya kufanikisha matumuzi sahihi ya ardhi.

Hapa tu umeona uhitaji wa watu na shida zilivyo, ingekuwa vyema kuwa na ushauri chanya wa jinsi ya kulifanya kuliko kuwa just negative. Suggest: wananchi wafikiweje? Au tahadhali ya utambuzi wa watendaji wanaofanya hii kazi watambuliweje/hakiki kabla ya kuwapa kazi?

Hakuna field ambayo ilikuwa ina msimamo mkali kuhusu kujitangaza kama afya, lakini juzi operation imefanyika na matangazo kedekede. Hospitali zinajitangaza na huduma wanazotoa.

Kuna ya kubaki nayo ofisini kwenu lakini ni vyema mtambuliwe uwepo wenu na mnayoyafanya. Mambo hubadilika, badilikeni mwendane na hali ya ulimwengu kwa vitu chanya.

Pia, hata kama mwenzako kuna vitu hajavizingatia, ni bora kuwa na lugha rafiki ya jinsi ya kurekebisha mambo au mfuate binafsi. Tuwe kwenye maadili hata unapomrekebisha mwenzako, professionalism izingatiwe.
20220701_184541.png
 
Kwa wakazi wa Dar ambao wanahitaji huduma zinazohusu ardhi au ushauri kuhusiana na maswala ya ardhi/majengo msisite kunitafuta.

Ninatoa huduma zifuatazo

-Kufatilia zoezi la utoaji wa hatimiliki mpaka inapotoka.

-Kufanya uthamini (Valuation),hii ni kwa wale wanaotaka kuhamisha umiliki wa ardhi,kukopa bank kwa kutumia dhamana ya nyumba na mengineyo

-Kupima viwanja (Survey)

-Ushauri wa masuala ardhi

Tuwasiliane PM
PM ndio wapi mkuu?
 
Hasira za nini ndugu?
Kujitangaza katika misingi ipi?
Makampuni mbalimbali yanayofanya kazi za kupima na kupanga miji yanajitangaza.

Andika kwenye Google search kampuni za kupima ardhi Tanzania au Dar es salaam. Je walioko kwenye mtandao si matangazo hayo? Wamemwandikia nani huko?
Chuo cha ardhi Morogoro kipo kwenye mtandao na moja ya kazi kinachoonyesha kufanya ni kupima ardhi na mipango miji. Je hao hawajatangaza?

Kama mnang'ang'ana na sheria na policy kandamizi/kama zipo, ndo maana kazi hizi zinashindwa kufanikishwa.

Uhitaji wa watu kufanya matumizi kwenye ardhi uko juu sana. Nyinyi mmejifungia kwenye maofisi bila kuwafikia wananchi kutatua matatizo yao na kuwapa elimu ya jinsi ya kufanikisha matumuzi sahihi ya ardhi.

Hapa tu umeona uhitaji wa watu na shida zilivyo, ingekuwa vyema kuwa na ushauri chanya wa jinsi ya kulifanya kuliko kuwa just negative. Suggest: wananchi wafikiweje? Au tahadhali ya utambuzi wa watendaji wanaofanya hii kazi watambuliweje/hakiki kabla ya kuwapa kazi?

Hakuna field ambayo ilikuwa ina msimamo mkali kuhusu kujitangaza kama afya, lakini juzi operation imefanyika na matangazo kedekede. Hospitali zinajitangaza na huduma wanazotoa.

Kuna ya kubaki nayo ofisini kwenu lakini ni vyema mtambuliwe uwepo wenu na mnayoyafanya. Mambo hubadilika, badilikeni mwendane na hali ya ulimwengu kwa vitu chanya.

Pia, hata kama mwenzako kuna vitu hajavizingatia, ni bora kuwa na lugha rafiki ya jinsi ya kurekebisha mambo au mfuate binafsi. Tuwe kwenye maadili hata unapomrekebisha mwenzako professionalism izingatiwe.View attachment 2279816
Ubarikiwe mkuu kwa kuliona hilo na kulifafanua vyema
 
Wewe mleta mada taaluma yetu yas Ardhi na Uthamini huruhusiwi kujitangaza hivi. Unaonekana kanjanja au hujui ninni maana ya taaluma yetu na miiko yake. Ni unprofessional so futa huu ujinga. Uzuri umeweka namba yako ntakufuatilia VRB nikuone na nikufunze maana ya taaluma yetu. Pole
Taaluma yako wewe na nani, acha kunyanyua mabega wewe
 
Wewe mleta mada taaluma yetu yas Ardhi na Uthamini huruhusiwi kujitangaza hivi. Unaonekana kanjanja au hujui ninni maana ya taaluma yetu na miiko yake. Ni unprofessional so futa huu ujinga. Uzuri umeweka namba yako ntakufuatilia VRB nikuone na nikufunze maana ya taaluma yetu. Pole
ACHA vitisho, kama lengo ni kumshauri ungemfuata inbox 📥 ukamshauri
 
Kwa ambae hukuona hili bango na unauhitaji wa msaada wa masuala ya ardhi usisite kunicheki.
 
Faida ya kuwa na hati

a) Zawadi pekee unayoweza kuipatia ardhi yako ni ulinzi, na ulinzi pekee ni kuitafutia hati. Hii ni kusema kuwa ardhi salama ni ardhi yenye hati. Hii ni faida kuu ya kwanza unayoweza kupata baada ya kuwa unamiliki hati.

b) Hati hupandisha thamani ya ardhi haraka mno. Hii ni faida nyingine kubwa.Unaweza kununua ardhi isiyo na hati kwa milioni mbili na ukaiuza milioni hata 20 baada ya kuitafutia hati.

Wanaofanya biashara za ardhi hutumia njia hii kujipatia faida kubwa.Hununua maeneo makubwa yasiyo na hati kwa bei ndogo huyapimisha,huyakatakata viwanja, na kuyatafutia hati halafu huyauza tena kwa bei kubwa zaidi. Ardhi yenye hati ina thamani kubwa mno.

c) Hati ya ardhi hutumika kama dhamana mahakamani .Unapokuwa na hati si tu unamiliki ardhi bali pia unamiliki mdhamini.Matatizo hutokea na wakati mwingine kufikishwa mahakamani ni jambo ambalo laweza kukutokea bila hata kutarajia wala kufikiri kama kuna siku utafika huko.Hatimiliki ni nyaraka inayoweza kukusaidia usiingie korokoroni .

Mara nyingi dhamana huwa inahitaji mali isiyohamishimika ambayo ni ardhi.Na kitu pekee kinachothibitisha kumiliki mali isiyohamishika ni hati. Kupitia hati unaweza kujidhamini mwenyewe au kumdhamini ndugu,jamaana rafiki.

d) Kupata mkopo ni faida nyingine ambayo sote twaijua. Zipo taasisi za fedha zinazokubali hata nyaraka nyingine ambazo sio hati lakini kwa mwenye hati anakuwa na uhakika zaidi ya kupata mkopo
 
Kwa wakazi wa Dar ambao wanahitaji huduma zinazohusu ardhi au ushauri kuhusiana na maswala ya ardhi/majengo msisite kunitafuta.

Ninatoa huduma zifuatazo

-Kufatilia zoezi la utoaji wa hatimiliki mpaka inapotoka.

-Kufanya uthamini (Valuation),hii ni kwa wale wanaotaka kuhamisha umiliki wa ardhi,kukopa bank kwa kutumia dhamana ya nyumba na mengineyo

-Kupima viwanja (Survey)

-Ushauri wa masuala ardhi

Tuwasiliane PM au 0765 49 45 48
Kwanza niwapongeze kwa kitu huduma mnayofanya. Mna nafasi kubwa sana ya kufanikiwa na kujitanua iwapo mtazingatia huduma bora na za uhakika. Kwa exeperience yangu ya Tanzania ni kwamba sehemu/kampuni/watu wote wanaohusika na kutoa huduma wamejijengea utamaduni wa kutanguliza tamaa mbele na kutokuwa waaminifu. Naomba niwape ushauri ufuatao:
1: Ongezeni (hama hamna) huduma ya kusaidia wateja kuhakiki viwanja wanavyotaka kununua kama ni halali au vina mgogoro. Hili ni jambo gumu kidogo lakini mkitengeneza network nzuri na mamlaka husika mnaweza kuwa na taarifa sahihi, hivyo kwa mfano mtu anapotaka kununua kiwanja, atumie huduma yenu ya kitengo cha upelelezi kujua kama kiwanja husika kina uhalali.
2. Pamoja na hili nawashauri pia jaribu kufanya huduma zenu ziwa za kuaminika na customer care iwe nzuri. Tanzania sehemu nyingi za huduma wanatoa kauli mbovu na wanatanguliza tamaa mbele.
 
Shukrani sana mkuu kwa kongole ulizotupatia na pia kwa ushauri wako safi.Tutazingatia yote

Kuhusu kutanguliza tamaa mbele kwa upande wetu haina nafasi kwani msingi wa kazi nyingi ni connection.Utapata kazi nyingine iwapo utamfanyia mtu kazi yake vyema na kwa uaminifu kwani atakutangaza kwa wengine.

Suala la kuhakiki kabla ya kununua eneo,hii ni rahisi sana inatakiwa uende kwenye ofisi za ardhi za halmashauri husika.Ukifika hapo omba kufanya kitu kinaitwa "OFFICIAL SEARCH" utapewa control number ulipie kiasi kidogo.Kwa kufanya hivyo utapata kujua uhalali wa umiliki wa eneo husika na pia kama kuna migogoro,mazuio au kama eneo limechukuliwa mkopo.

Ushauri au jambo lolote linalotatiza kuhusu mambo ya ardhi kwetu ni bure kabisa.Utasikilizwa jambo lako na tutakusaidia kadri tunavyoweza.
 
This is nothing but an act of selfishness and greed. Hakuna ubaya wow one wa mtu mwingine kutuelimisha na huenda siku za usoni tukafanya biashara, hiyo VRB unategemea tungeijua vipi?

Na pia sasa tupo kwenye uchumi wa huduma kuwafuata wateja hivyo so dhambi akifanya hivyo.
Hawa ndio hawapendi raia wajue taratibu za maswala tofauti tofauti ili wawapige hela. Sasa ukiuliza hata shida ipo wapi haeleweki amekuja tu kung'aka.
 
Nani anahaki ya kumiliki hati?

a) Mtanzania,aidha mwanamme au mwanamke mwenye uraia halali wa Tanzania.

b) Kikundi cha watu ambao ni raia wa Tanzania walio katika umoja wa kisheria,wabia au washirika.

Ifahamike kwamba mtu ambaye sio raia wa Tanzania, au kikundi cha watu au mtu ambaye ana shirika lenye hisa,ambao wengi wa wanahisa wake sio Watanzania hawana haki ya moja kwa moja ya kumiliki ardhi nchini na kupewa hakimiliki ya ardhi isipokuwa tu kama watapewa ardhi hiyo kama wawekezaji.

Ili kupata hati kwa maeneo ya mijini eneo linapaswa liwe limekidhi vigezo vifuatavyo

a) Eneo husika lazima liwe limetangazwa kuendelezwa kimipango miji(planning areas).

b) Eneo liwe limeandaliwa michoro ya mipango miji na kusajiliwa wizarani.

c) Eneo liwe limepimwa kwa kufuata mchoro wa mpango mji uliopo na kupata usajili kwa ramani hiyo ya upimaji wizarani.
 
Mkuu naomba utupe process zako zote kuanzia mwanzo hadi mwisho ili mtu akikufuata awe anajua procedure zote.Mfano mm kuna shamba langu nataka nilitafutie hati km heka kadhaa na nimeona eneo lipo humu kwenye hyo attachment yako.Ninaanzia au ww utaanzia wapi had kuishia wapi mpaka nipate hati yangu na gharama zinaweza kuwa kias gani?Nenda kwa mfano tu ili niweze kujua naimudu au vp?
 
Okay sawa,hilo shamba lako limepimwa?
 
Back
Top Bottom