Billy Kimber
Member
- May 20, 2022
- 89
- 207
- Thread starter
- #41
Hapa inategemeana kama eneo lako limepimwa au halijapimwa.Mkuu naomba utupe process zako zote kuanzia mwanzo hadi mwisho ili mtu akikufuata awe anajua procedure zote.Mfano mm kuna shamba langu nataka nilitafutie hati km heka kadhaa na nimeona eneo lipo humu kwenye hyo attachment yako.Ninaanzia au ww utaanzia wapi had kuishia wapi mpaka nipate hati yangu na gharama zinaweza kuwa kias gani?Nenda kwa mfano tu ili niweze kujua naimudu au vp?
a) Kama eneo halijapimwa inatakiwa lipimwe na kusajiriwa.Upimaji unaweza ukafanywa na kampuni binafsi au wapimaji wa halmashauri husika.
Baada ya kupimwa,kupitishwa na kusajiriwa hatua ya ufatiliaji hati inaweza kuendelea (nitaelezea chini hatua za kufuata)
b) Kama eneo lako limepimwa na kusajiriwa kinachofuata hapo ni kufatilia mchakato wa hati ambao unahusisha hatua zifuatazo
i)Kujaza Fomu ya maombi ya kupatiwa hati
ii) Uhakiki wa taarifa za kiwanja na muhusika.Hatua hii inajumuisha kufanyika kwa uhakiki wa kiwanja kinachoombewa hati kama kimepimwa na kusajiriwa lakini pia kuhakiki umiliki wa muombaji wa hati
iii)Hatua inayofuta ni kupewa gharama ambazo
utakiwa ulipie ili kufanikisha zoezi la kupata hati.Gharama hizo ni
Premium fee: Eneo la kwanja x Gharama ya kiwanja kwa mita mraba x 0.025
Registration Fee: Hii inatozwa 20% ya kodi ya ardhi ya mwaka
Survey Fees: Hii hutegemea na hamashauri husika
Certificate of Preparation
Deed Plan Fee
Stamp Duty
iv) Utatakiwa pia uwasilishe picha za pasipoti saizi za rangi za hivi karibuni.