Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
KUSITISHA UTOAJI HUDUMA YA UVUSHAJI KWA KIVUKO MV. KIGAMBONI
Kivuko MV. KIGAMBONI kinasimama kutoa huduma kwa ajili ya kwenda kufanyiwa ukarabati mkubwa ili kitakaporejea kiweze kutoa huduma kikiwa katika hali ya ubora na usalama.
TEMESA inawashauri abiria hasa wenye magari kwa sasa, kutumia njia mbadala ya Daraja la Mwalimu Nyerere ili kuepusha msongamano katika eneo la kivuko mpaka pale kivuko MV. KIGAMBONI kitakaporejea.
Aidha, shughuli za uvushaji katika eneo hilo, zitaendelea kutolewa kama kawaida kwa kutumia kivuko MV.KAZI pamoja na Sea Taxi.
TEMESA inawaomba radhi abiria wote kutokana na usumbufu watakaoupata wakati wote ambapo kivuko MV. KIGAMBONI hakitakuwepo na inawakumbusha kuendelea kufuata maelekezo ya mabaharia wakati wanapotumia vivuko ili kuendelea kuwa salama.
Imetolewa na Kitengo cha Masoko na Uhusiano
TEMESA
06/06/2024
PIA SOMA
- Abiria tunaovuka Kivuko cha Kigamboni leo ni kero tupu, kivuko kimoja tu ndio kinafanya kazi
- Changamoto ya Vivuko Kigamboni kwa sasa kunafanya kazi kivuko kimoja tu
- Vivuko vimekuwa kero, wanatoa taarifa za ghafla kuwa hamna huduma
- Huduma za Vivuko Kigamboni janga linaloenda kusababisha maafa nchini
- Huduma za Uvushaji wa MV Kigamboni zasitishwa