A
Anonymous
Guest
Natumia nafasi hii kutoa mrejesho wa hoja iliyowasilishwa jukwaani kuhusu kero zilizokuwa zikijitokeza kufuatia kusitishwa kwa huduma za vyoo katika Kituo cha Mwendokasi Kivukoni.
Baada ya zoezi la ukarabati, nimebaini kuwa huduma zimerejea katika hali nzuri. Miundombinu imekarabatiwa, na kwa sasa maji yanapatikana tofauti na ilivyokuwa awali.
Huduma hizo zilikuwa zimesitishwa kwa takribani mwaka mmoja kutokana na changamoto ya ukosefu wa maji katika vyoo hivyo.
Kusitishwa kwa huduma hizo kulisababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa kituo hicho.
Baadhi walilazimika kujisaidia katika maeneo yasiyo rasmi, ikiwemo kwenye korido zilizo karibu na vyoo, huku wengine wakilazimika kutoka nje ya kituo na kufuata huduma ya choo katika Soko la Samaki lililopo umbali kidogo kutoka kituoni.
Hatua ya kufanya maboresho ilikuja baada ya hoja ya mdau kuripotiwa, ambapo matengenezo yalianza kufanyika. Kwa sasa, hata miundombinu ya maji imeboreshwa na hali ya huduma imeimarika.
Nawapongeza wahusika kwa kuchukua hatua, ingawa zimekuja kwa kuchelewa. Hata hivyo, nitoe wito kwao kuhakikisha kuna usimamizi madhubuti, hususan katika suala la upatikanaji wa maji, ili kuzuia kujirudia kwa changamoto zilizokuwa zikijitokeza mara kwa mara hapo awali.
Pia soma:
~ Abiria Mwendokasi-Kivukoni walazimika kutumia korido kujisaidia haja ndogo kutokana na vyoo kutofanya kazi
~ Vyoo Kituo cha Mwendokasi Kivukoni vyaanza kukarabatiwa baada ya kuripotiwa kusitisha huduma kwa kipindi kirefu