LIMBOMAMBOMA
JF-Expert Member
- Oct 3, 2017
- 10,482
- 14,007
Kiukweli mama akiendelea na ndugai, atamvuruga Sana...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sema mnaona hafai kwa vile haafiki upuuzi wa chadema kuwaonea akina HalimaNimeona niliandike hili sasa hapa JF na kwa uwazi ili kutoa angalizo mapema kwa mwelekeo wa siasa za Tanzania huko tuendako.
Watanzania kwa sasa wametega macho na masikio kuona ni namna gani Rais mpya wa Tanzania, mama Samia Suluhu anaweza kuivusha Tanzania inayopitia kwenye mikwamo mikubwa wa kiuchumi, kidiplomasia na kisiasa iliyotengenezwa na mtangulizi wake.
Mama Samia bila woga na kificho aliweka wazi kabisa kuwa haridhishwi na mwenendo wa utendaji wa bunge la sasa, na kwa maneno yake ililiita bunge letu ni Dhaifu (halina afya) na limejaa wacheza ngoma (linadamka). Wachambuzi wanasema kauli ile ililenga zaidi kiti cha spika. Watu waliopo karibu na Spika Ndugai wanadai kuwa kauli ile ulimuudhi na kumkasirisha spika Ndugai, na ipo siku atatapika nyongo.
Sasa ngoja tuweke ukweli hapa, na tuuseme jinsi ulivyo kama unavyonong'onwa nyuma ya pazia.
Wachambuzi kadhaa wanasema huenda miongoni mwa watu wa juu kabisa ambao hawakutaka au hawakufurahi kuona mama Samia Suluhu anaupata urais wa Tanzania walikuwa Dkt. Bashiru Ally na Spika Ndugai (Hakuna uthibitisho kamili mpaka sasa, ila huko mbele ya safari ukweli mwingi utaibuliwa).
Viongozi hao wanadaiwa kufanya mawasiliano na mipango ya chini kwa chini kuratibu mkakati wa kisiasa ili kumkwamisha mama Samia kupata nafasi ya kuwa urais wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwa amefariki dunia huku umma wa watanzania ukiwa bado umefichwa. Lolote lingeweza kutokea.
Kwa sasa mama Samia anapambana kwa hali na mali kuwavuta wawekezaji na wahisani (mabeberu!) ili wamwage pesa zao hapa Tanzania ili kunusuru athari za mdororo wa kiuchumi kwa Tanzania. Na moja ya kikwazo kikuu anachokumbana nacho ni sharti la wahisani kuona mihimili mikuu ya bunge na mahakama ikiwa huru zaidi kujiendesha. Habari zisizo rasmi zinadai tayari hoja ya kuwatema wabunge wa Covid 19 iko mezani kwa mama Samia.
Alichokifanya Nape ilikuwa ni kuamsha agenda kimakusudi (Pre empty) na anachokifanya Ndugai ni kutaka kupimana ubavu na mama Samia kwa mtindo huo huo. Inadaiwa mjadala ndani vikao vya juu vya CCM ulifikia hatua ya kuona kuendelea kuwakumbatia wabunge wa Covid 19 hakuna faida tena kwa sasa, kwa kuwa mazingira ya kisiasa yameshabadilika na kunachafua vibaya taswira ya utawala mpya wa mama Samia.
Ukiacha zile taarifa za uwepo wa mkakati wa kichini chini na kimakusudi uliolenga kutumia bunge na wabunge kujenga hoja ya kutokuwa na imani na Rais ili achunguzwe na kicha kuwekwa pembeni (jambo ambalo kikatiba linawezekana kwa 100%), kuna mambo mengine kadhaa yanaelezwa kuendelea kufanyika ili kumkwamisha mama Samia.
Moja ya mkakati usio rasmi unaoendelea kwa sasa miongoni mwa wabunge kadhaa ndani ya CCM ni kuhakikisha kiti cha spika ajae kinakaliwa na mwanamke (Dr. Tulia?) ikiwa Spika Ndugai ataendelea kukwamisha harakati zozote za utendaji wa mama Samia. Tayari Spika Ndugai anajua wazi hatakiwi kwenye hicho kiti na utawala wa mama Samia na ili kujipanga vyema kulinda himaya hiyo ameanza mkakati wa kutaka kuonyesha anawajali sana wabunge wanawake.
Muda ni mwalimu mzuri kwenye kila jambo. Tusubiri, tujipe muda na tutazame yatakayojiri.
Kusema kweli bora huyu Tulia kuliko huyu mtu ndugai. Ni mswahili kuliko waswahili wenyewe. Anapenda mipasho na umbea kuliko chochote.Mihemko ndio imemtawala kuliko sheria!Moja ya mkakati usio rasmi unaoendelea kwa sasa miongoni mwa wabunge kadhaa ndani ya CCM ni kuhakikisha kiti cha spika ajae kinakaliwa na mwanamke (Dr. Tulia?) ikiwa Spika Ndugai ataendelea kukwamisha harakati zozote za utendaji wa mama Samia. Tayari Spika Ndugai anajua wazi hatakiwi kwenye hicho kiti na utawala wa mama Samia na ili kujipanga vyema kulinda himaya hiyo ameanza mkakati wa kutaka kuonyesha anawajali sana wabunge wanawake.
Ngosha mbona unaandika kama unakimbizwa? tulia chini utafakari nini unataka kuandika badala ya kukurupuka kama uharo!Hamna lolote mnaagenda yenu ambayo mnaona haitimii akiwepo tatizo lenu mnataka kila mtu amuabudu samia. Huyo samia kaanza kwa kasi sana kumchafua magufuli kujifanya anatatua makosa kwenye mambo ya serikali kumbe kuna watu wake anawatafuta angekua na nia ya kweli mbona kina kingwangala bado wanadunda mtaani licha ya upumbavu alioufanya serikalini.
Basi Mungu atende haki haraka
Ulikuwa ni uharibifu mkuu badala ya uchaguzi mkuuWanapigwa katika kura?
Kura gani Tz kuna uchaguzi au uchafuzi
Unakera natamani nikutusi
Lema si wakuchukulia kimzaa mzaa hata kidogo - maono yake yanatisha sana.
Umeliweka vizuri sana, NDUGAI ndiye adui mkubwa wa Rais SSH. Na bahati mbaya muda unakwenda na anazidi kuharibuNimeona niliandike hili sasa hapa JF na kwa uwazi ili kutoa angalizo mapema kwa mwelekeo wa siasa za Tanzania huko tuendako.
Watanzania kwa sasa wametega macho na masikio kuona ni namna gani Rais mpya wa Tanzania, mama Samia Suluhu anaweza kuivusha Tanzania inayopitia kwenye mikwamo mikubwa wa kiuchumi, kidiplomasia na kisiasa iliyotengenezwa na mtangulizi wake.
Mama Samia bila woga na kificho aliweka wazi kabisa kuwa haridhishwi na mwenendo wa utendaji wa bunge la sasa, na kwa maneno yake ililiita bunge letu ni Dhaifu (halina afya) na limejaa wacheza ngoma (linadamka). Wachambuzi wanasema kauli ile ililenga zaidi kiti cha spika. Watu waliopo karibu na Spika Ndugai wanadai kuwa kauli ile ulimuudhi na kumkasirisha spika Ndugai, na ipo siku atatapika nyongo.
Sasa ngoja tuweke ukweli hapa, na tuuseme jinsi ulivyo kama unavyonong'onwa nyuma ya pazia.
Wachambuzi kadhaa wanasema huenda miongoni mwa watu wa juu kabisa ambao hawakutaka au hawakufurahi kuona mama Samia Suluhu anaupata urais wa Tanzania walikuwa Dkt. Bashiru Ally na Spika Ndugai (Hakuna uthibitisho kamili mpaka sasa, ila huko mbele ya safari ukweli mwingi utaibuliwa).
Viongozi hao wanadaiwa kufanya mawasiliano na mipango ya chini kwa chini kuratibu mkakati wa kisiasa ili kumkwamisha mama Samia kupata nafasi ya kuwa urais wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Magufuli kuwa amefariki dunia huku umma wa watanzania ukiwa bado umefichwa. Lolote lingeweza kutokea.
Kwa sasa mama Samia anapambana kwa hali na mali kuwavuta wawekezaji na wahisani (mabeberu!) ili wamwage pesa zao hapa Tanzania ili kunusuru athari za mdororo wa kiuchumi kwa Tanzania. Na moja ya kikwazo kikuu anachokumbana nacho ni sharti la wahisani kuona mihimili mikuu ya bunge na mahakama ikiwa huru zaidi kujiendesha. Habari zisizo rasmi zinadai tayari hoja ya kuwatema wabunge wa Covid 19 iko mezani kwa mama Samia.
Alichokifanya Nape ilikuwa ni kuamsha agenda kimakusudi (Pre empty) na anachokifanya Ndugai ni kutaka kupimana ubavu na mama Samia kwa mtindo huo huo. Inadaiwa mjadala ndani vikao vya juu vya CCM ulifikia hatua ya kuona kuendelea kuwakumbatia wabunge wa Covid 19 hakuna faida tena kwa sasa, kwa kuwa mazingira ya kisiasa yameshabadilika na kunachafua vibaya taswira ya utawala mpya wa mama Samia.
Ukiacha zile taarifa za uwepo wa mkakati wa kichini chini na kimakusudi uliolenga kutumia bunge na wabunge kujenga hoja ya kutokuwa na imani na Rais ili achunguzwe na kicha kuwekwa pembeni (jambo ambalo kikatiba linawezekana kwa 100%), kuna mambo mengine kadhaa yanaelezwa kuendelea kufanyika ili kumkwamisha mama Samia.
Moja ya mkakati usio rasmi unaoendelea kwa sasa miongoni mwa wabunge kadhaa ndani ya CCM ni kuhakikisha kiti cha spika ajae kinakaliwa na mwanamke (Dr. Tulia?) ikiwa Spika Ndugai ataendelea kukwamisha harakati zozote za utendaji wa mama Samia. Tayari Spika Ndugai anajua wazi hatakiwi kwenye hicho kiti na utawala wa mama Samia na ili kujipanga vyema kulinda himaya hiyo ameanza mkakati wa kutaka kuonyesha anawajali sana wabunge wanawake.
Muda ni mwalimu mzuri kwenye kila jambo. Tusubiri, tujipe muda na tutazame yatakayojiri.
Uzuri Madam President ni very smart upstairs sina shaka amekwisha realise kwamba Mh. Ndugai mwisho wa siku ata end up being a liability kwenye Administration ya Madam President - kila mtanzania mwenye akili timamu anaona kwamba Current administration Ikulu na Mh. Ndugai don't seem to run in sync!!Ndugai ni adui wa taifa
Spika ambaye atakuwa na uwezo na weledi mkubwa wa kuchambanua mambo ya ki-leo kwa uhakika ni Mh. Zungu nawambieni - jamaa huyu ana vast handon experience ya mambo mengi Duniani - personally nilianza kunchukulia seriously wakati alipo fanya analysis ya jinsi makampuni makubwa ya cellphone networks yanavyo tuibia kiufundi kwa kukwepa kodi na makato mengine muhimu, kaenda mbali zaidi kwa kupendekeza mpaka aina ya electronic systems za kubaini jinsi wanavyo tuibia ikiwemo na upigaji simu kwenda nje ya nchi. System ilinunuliwa na kuwa installed inasaidia sana ku-generate revenue za kufa mtu, what did Mh. Zungu get in return hakuwahi hata kuteuliwa kwenye Board ya TCRA wanateuliwa watu mediocre kwa kujuana,wanapeana ulaji tu, mtu ungetegemea Mh. Zungu angepewa hata u Board Chairman wa TCRA kutokana na ubunifu wake,lakini wapi bwana!! Aliteuliwa Uwaziri briefly halafu akaondolewa fasta - Miaka ya hivi karibuni Taifa letu limeingiliwa na kasumba ya kusujudu PhD holders sijui kwa nini? Mambo haya hayapo huko Ulaya wala Marekani - chunguza list ya mawaziri na viongozi wakubwa kwenye mataifa hayo yaliyo endelea - hawana kasumba ya ajabu anayo anza kujengeka hapa kwetu - sijasema mtu kujiongeza kielumu ni dhambi - ninacho sema wasirundikwe Serijakini na mashirika ya UMMA waende kufubdisha vyuoni huko ndiko wana hitajika zaidi - wenzetu Ulaya na Marekani kundi hilo wengi wao ni ma academician - sio wana siasa wala nini sijui!!Dr Tulia ? Sidhani. Amebebwa mno mpaka hapo na mwendazake. Binafsi simuoni kama ni type inayoendana na Mama Samia.....kama ana lengo la kutengeneza "team yake".
G Lema sio nabii na wala hana uwezo wa kiroho wa kutoa unabii. Masharti ya unabii hayatokani na vitu vinavyozungumzwa ila ni mambo ambayo hayajui na wala hujawahi kuyafikiria kamba yatatokea ndio hufunuliwa na kuyatamka bayana.Lema si nabii ila anajua kilicho nyuma ya unabii Wake na si mambo ya kufurahia kwa vile mtu humpendi maana unabii huo waweza geuka ukamtokea unayempenda
Ngosha mbona unaandika kama unakimbizwa? tulia chini utafakari nini unataka kuandika badala ya kukurupuka kama uharo!
Kumbeee wewe jamaa ni nabiiMama Samia bila woga na kificho aliweka wazi kabisa kuwa haridhishwi na mwenendo wa utendaji wa bunge la sasa, na kwa maneno yake ililiita bunge letu ni Dhaifu (halina afya) na limejaa wacheza ngoma (linadamka). Wachambuzi wanasema kauli ile ililenga zaidi kiti cha spika. Watu waliopo karibu na Spika Ndugai wanadai kuwa kauli ile ulimuudhi na kumkasirisha spika Ndugai, na ipo siku atatapika nyongo.