Udini ,idini idini,idini,
Ukabils ukabila ukabila,.
Kuchanganya dini na siasa ndiko huku .
Ni wazi kabisa kuwa Gwajima bado ni askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima.
Wakati huo huo anagombea kupitia Chama cha Maponduzi.
Ama kwa hakika kama kuna watu wa vyama vingine ndani ya kanisa lake hawana tena askofu bali wao ni wapinzani wa askofu huyo mzinzi na mnafiki.
Alipaswa kuachana na uaskofu kama alivyofanya Dr. Slaa na kuingia kwenye siasa.
Endapo nchi yetu ingekua na mgombea Huru au mgombea binafsi basi angeweza kugombea. Lakini kugombea kupitia Chama wakati Chama hicho kiko wazi kabisa kuwa kina uadui mkubwa na chuki kubwa kwa wapinzani au watu wa vyama vingine kufikia hatua ya kutoa wito Mara kwa Mara bungeni na nje ya bunge kuwa wapinzani wauawe basi hakika Gwajima ni mchungaji aliyekimbia kondoo wake baada ya kuona mbwa mwitu au serikali imewasakama kondoo wake.
Akina Sylvester Gwamanya ni watu wa TISS miaka mingi ndio maana hatuwashangai.
Matapeli wote wamekimbilia CCM baada ya kuwadanganya watu na kujipatia fedha kama walivyo wasanii wengi waliojihusisha na biashara za madawa na Leo ndio wapiga debe wa CCM.
Nchi imevamiwa na wahuni na wananufaika mana watu wema wengi ni waoga sana. Waovu wengi wanajiunga na wakubwa ili mambo yao yaende kimya kimya.
Mtumishi wa Mungu wa kweli kama amebarikiwa kupata Mali na uwezo wa kuisaidia jamii sio lazima jamii imbebe kwa kutumia kodi zake kama ilivyombeba kwenye sadaka. Mbunge kwa mwezi mmoja analipwa zaidi ya mil. 12. Kwa wakati huu wa awamu hii yenye mateso makubwa kwa wafanyakazi ,hizo ni fedha nyingi sana. Na ni fedha zinazoweza kumbeba akakopa zaidi ya mil. 700 mpaka bil. 1.
Sasa tujiulize ni mtumishi gani wa Mungu anayeshindwa kujitolea kuwatumikia wananchi bila kutegemea fadhila kutoka kwa maskini.?
Hawa ndio kama kunawale waliokaa karne zilizopita na kubadili vifungu vya biblia ili waitumie kuwatawala watu na kuwafanya watumwa wao.
Ninapootafakari mambo kama haya naamini kuwa Uislam umefanikiwa sana kwa kulinda Dini ya haki isichafuliwe na watu wanaotaka kuweka maslahi yao binafsi.
Eti kamati ya kuhamasisha Amani iwepo kwa wezi wa CCM na dhulma itendeke ili CCM ishinde hawaoni kuwa Gwajima anachanganya dini na siasa. Hawaoni kabisa !
Eti kuna watu wanahamasisha amani utafikiri Tanzania hakuna amani. Hizo kamati zinatakiwa huko Congo sio hapa . Hapa sisi tuna amani Tangu mkoloni alipoitawala Tanzania na kuweka mipaka hatujawahi kupigana wenyewe kwa wenyewe. Amkeni acheni kupumbazwa na waroho na walafi waliolewa pesa sasa wamatafuta kuitwa waheshimiwa.
Wanajua wazi kuwa roho za watanzania hazina amani kwa sababu hawatendewi haki.
Tatizo la watanzania ni dhulma tupu.
Amani tunayo!!