Huenda David Zacharia Kafulila ndio mwanasiasa kijana toka CCM anayewasumbua zaidi Anti-Samia kwa hoja zenye data na misimamo thabiti isiyoyumba

Huenda David Zacharia Kafulila ndio mwanasiasa kijana toka CCM anayewasumbua zaidi Anti-Samia kwa hoja zenye data na misimamo thabiti isiyoyumba

Wasalaam JF,

Hoja thabiti za aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe David Zacharia Kafulila zimeendelea kugonga Vichwa vya wale wote wanaotamani kusikia na kuona Rais Samia Suluhu Hassan kashindwa kuliongoza Taifa hili na Sasa utafutwe mbadala,

Tofauti kabisa na wanasiasa wengi hapa nchini David Zacharia Kafulila mara zote amekuwa akijenga " HOJA ZAKE KWA EVIDENCE NA DATA " jambo ambalo limekuwa likiwaumiza zaidi Wapinzani wa Chama Cha Mapinduzi na wale Anti-Samia wote kwani mara zote hushindwa kuzijibu na kuishia kutukana na kukejeli,

Wapo wanaosema David Kafulila alishindwa kuiba na kuwekeza kama wenzake alipokuwa madarakani ndio sababu ya yeye Leo amegeuka " Chawa wa Mama "

Record zinaonesha Mhe David Zacharia Kafulila ndio kijana anayeichukia zaidi Rushwa hapa Tanzania na huenda ndio sababu ya yeye kuendelea kuwa mtu wa Maisha ya kawaida kabisa tofauti na vijana wengi wa Kitanzania kwani wengi wao mara tu wanapoteuliwa hukimbilia kuiba Mali za UMMA na kuonekana kuwa wao ni MASHUJAA kwani huonekana wakiogelea kwenye Ukwasi ndani ya muda mfupi baada tu ya " UTEUZI "

Lakini pia, Huenda hili linachagizwa zaidi na vita ya Urais ndani ya CCM inayoonekana kukolea kila uchapo huku Upande pia wa Upinzani wakiendelea kumtupia madongo Rais Samia ili aonekane hawezi kuongoza Ila wao ifikapo 2025 waweze kuchukua hili dola na wangetamani wasiwepo watu aina ya Kafulila wanaofuta hoja zao kwa data na ushahidi anuai,

Tunaomfuatilia huyu kijana vizuri na wenye kumbukumbu sahihi mtakubaliana na Mimi kuwa Mhe David Zacharia Kafulila tangu akiwa mbunge wa Kigoma Kaskazini baadae RAS Songwe na Juzi RC Simiyu wakati wote huu Kafulila amekuwa ni mtu wa kuiunga mkono Serikali kwa kuandika na kurekodi makala mbalimbali tofauti na mawazo ya wengi kuwa ni baada ya kufurushwa kwenye U-RC ndio ameanza kuandika haya,

Tafiti zisizo rasmi ila zinazoaminika zinaonesha kuwa Mhe David Zacharia Kafulila alimsemea zaidi Rais Samia Suluhu Hassan akiwa RC Simiyu Pengine kuliko RC yeyote hapa Tanzania kwa wakati ule na hii iwatafakarishe wale wote wanaosema anachokifanya Leo Kafulila ni kusaka UTEUZI,

Sisi kama vijana, Tunamengi ya kujifunza toka kwa Mhe David Zacharia Kafulila hasa la Kiongozi kuwa Mwadilifu na mwaminifu hasa kwa kuchukia zaidi Rushwa na Wala Rushwa hata kama kesho tutasalia masikini Ila historia itaishi na ipo siku itatoa hukumu dhidi yetu,

#TUACHE KUHIMIZA VIJANA WAIBE WAKIWA NA VYEO ILI KESHO WASICHEKWE NA KUKEJERIWA,

====
Post in thread 'Kafulila: Rais Samia Suluhu kusuka upya mfumo wa Elimu ya Tanzania ni zaidi ya Uamuzi muhimu wowote uliowahi kufanyika baada ya Uhuru' Kafulila: Rais Samia Suluhu kusuka upya mfumo wa Elimu ya Tanzania ni zaidi ya Uamuzi muhimu wowote uliowahi kufanyika baada ya Uhuru




====
ONA HIZI KEJELI KWA WAZALENDO
👇🏿👇🏿

Thread 'Kafulila acha kusifu na kuabudu zama zimebadilika, mvua zinanyesha kubali umepumzishwa, shika jembe ukalime' Kafulila acha kusifu na kuabudu zama zimebadilika, mvua zinanyesha kubali umepumzishwa, shika jembe ukalime


Thread 'Kafulila hukuwekeza kama wenzako akina Ally Happi utakuwa mpiga tarumbeta hadi lini? Unazeeka sasa!' Kafulila hukuwekeza kama wenzako akina Ally Happi utakuwa mpiga tarumbeta hadi lini? Unazeeka sasa!

Sawa kafulila, tafuta kazi ya kufanya. Uchawa sio mzuri.
 
Ni wapi Jamaa amesema anasaka UTEUZI?

Mwacheni mtu afanye anachokipenda nacho ni kumpigania Mama Samia Suluhu Hassan

Anakipigania cheo Wala sio Rais. Kumbuka maneno ya Rais wakati anamtumbua. Tena alitumbuliwa akiwa safarini Dodoma.
 
Mimi sio Kafulila Kaka, Ila Sipendi ujinga wa kuhamasisha watu kuiba wawapo na madaraka,

Kafulila imejishusha Sana. Kutoka mpinga ufisadi mpaka kuwa chawa wa RAIS. Pole Sana angalia ulipojikwaa. Unatetea mfumuko wa Bei na mikopo halafu unajiona upo sawa?. Endelea na uchawa.
 
Ila hoja za namba zinauhalisia zaidi ya bra bra zile

Tofautisha namba za makarasi na namba za uhalisia. Kuna data zingine za kupika. Juzi tu hapo bungeni kumetokea mabishano Kati ya Waziri wa Fedha na Spika wa Bunge kuhusu data. Kuna mbunge alipinga kuonesha data zinavyosema ni tofauti na jimboni kwake kulivyo.
 
Back
Top Bottom