Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Huenda haitazidi ijumaa ya kesho..
Akisubiri kubanduliwa na bunge bila kujiuzulu, basi atakua amejiondolea mwenyewe sifa na vigezo vya kikatiba kuwania nafasi za uongozi wa kisiasa wala, kushikilia nafasi yoyote ya utumishi wa umma nchini Kenya. Kwa lugha nyingine, atakua amajifungia maisha yake yote kutokujihusisha na siasa, lakini pia utumishi wa umma. Hiyo ni kwa mujibu wa katiba ya Kenya.
Hata hivyo,
Kutokana na uzito wa tuhuma zilizoibua sekeseke la musuada wa kubanduliwa kwake ofisini, kuna uwezekano mkubwa sana wa muungwana Rigath Gachagua, akapelekwa mahakamani moja kwa moja, iwe amejiuzulu kwa hiyari yake mwenyewe au asubiri kubanduliwa na bunge. Tuhuma zinazomkabili za kisheria, kikatiba, za kimaadili, uchochezi na zile za rushwa ni nzito mno, haziwezi kumuacha salama uraiani.
Kwa mipango ilivyo mpaka sasa, mabunge yote mawili lile la kitaifa na lile bunge la seneti wako tayari kuhakisha mwamba hachomoki kwa mujibu wa sheria na katiba ya Kenya, bali anakwenda jela 🐒
Mungu Ibariki Tanzania