Huenda huyu akawa ni mtu hatari Zaidi kwa Upinzani wa Tanzania

Huenda huyu akawa ni mtu hatari Zaidi kwa Upinzani wa Tanzania

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029
Aina ya Siasa anayofanya Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka ni kete muhimu sana kwa CCM na anguko la Upinzani Tanzania

====

HEBU ANGALIA SHAKA AKISHIRIKI NA WANAWAKE WA MTWARA WALIOMPA TUZO MAALUMU RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Wanawake mkoani Mtwara wamemkabidhi tuzo maalumu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wa kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo hususan mkoani humo.

IMG-20220608-WA0037.jpg

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema tuzo hiyo itamtia moyo na kumpa ari Rais Samia kuendelea kuwatumikia Watanzania.
IMG-20220608-WA0033.jpg

"Kitendo cha kumpatia tuzo mnamtia moyo, mnapa ari ya kuwatumikia Watanzania, pia mnamtia ari ya kutimiza malengo yenu akinamama katika mambo muhimu na ya msingi kama ambavyo nimeshasema.
IMG-20220608-WA0031.jpg

"Mwito wangu kwenu msisite, msiishie hapa endeleeni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu, kila mmoja kwa imani yake Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya njema ili aweze kututumikia Watanzania," amesema.
IMG-20220608-WA0036.jpg

Akiendelea kuzungumza zaidi kuhusu tuzo hiyo, Shaka amesema aliyoyafanya Rais Samia wanawake wanayajua hata ukiwaamsha usingizini wanakwambia ameifungua Mtwara.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hiyo, kwa niaba ya wanawake hao Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Mtwara Zuhura Farid amesema wanawake wa Mtwara kwa niaba ya wanawake wengine wote wanampongeza Rais Samia kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya.
IMG-20220608-WA0033.jpg

"Hivyo tunaomba tukukabidhi zawadi hii kwa heshima na taadhima tunaomba umfikishie zawadi hii mama na umwambie asichelewe kufika Mtwara aje atuone kinamamma," amesema.


=======

HEBU ANGALIA SHAKA ALIVYOIWAKILISHA CCM KUIAGA TIMU YETU YA TEMBO WARRIORS

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ashiriki hafla ya kuiaga timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu Tembo warriors inayoelekea nchini Poland barani Ulaya kwa maandalizi ya kuelekea mashindano ya dunia yatakayofanyika nchini Uturuki, 2022.
IMG-20220608-WA0010.jpg

Hafla hiyo ilifanyika usiku wa tarehe 06 Juni, 2022 katika ukumbi wa hotel ya Regency Park, Dar es Salaam ambapo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini.

IMG-20220608-WA0013.jpg
 
Aina ya Siasa anayofanya Katibu wa NEC itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka ni kete muhimu sana kwa CCM na anguko la Upinzani Tanzania,
ukumbi wa hotel ya Regency Park, Dar es Salaam ambapo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo nchini.
Shaka namkubali Sana.
 
Kama kuna kitu mi sielewi mtanisaidia wadau. Hivi bado marufuku ya wapinzani kufanya siasa bado ipo? Maana namwina Shaka tu, wa upinzani siwaoni wala kuwasikia.
 
Huyu jamaa anajua sana Siasa aise,

..hali ngumu ya maisha na uchumi ndio tishio la Ccm kwa sasa hivi.

..Ccm wanakosea kuamini kwamba wapinzani ni watu hatari kwa chama chao.

..Kitu ambacho ni hatari kwa Ccm ni wananchi kuamini kwamba chama hicho kimekosa mbinu za kutatua changamoto za maisha na kiuchumi zinazowakabili.
 
Mhh wapi alikuwa Nape kidogo niliona anawezakujenga hoja na kujibu hoja wakati yu katibu wa itikadi na uenezi. Huyu hafiki hata robo.
 
Huyo yupo serikalini ndio maana unamuona wa maana lakini mwambie aje huku CHADEMA hata siku Moja hawezi kumudu. He has state resources and security.
 
Back
Top Bottom