Huenda huyu mtangazaji wa E. FM Maulid Kitenge kapata shavu sehemu nyingine

Mtangazaji maarufu wa Habari za Michezo, Maulid Kitenge, ameweka wazi kuwa ameondoka Radio EFM na sasa amehamia rasmi katika kituo cha Wasafi FM kinachomilikiwa na Mwanamuziki Diamond Platnumz.Kitenge ameondoka na watangazaji wenzake wawili ambao ni Yusuph Mkule na Mwanaidi Suleiman,Pia kwenye jopo lao amemuongeza mchambuzi maarufu wa mchezo nchini Eddo Kumwembe,ambapo watakuwa wakiendesha kipindi cha sport Arena kila siku kuanzia jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 5.Kadhalika atakuwa akichambua magazeti saa moja asubuhi kama alivyokuwa akifanya Efm kwenye kipindi cha joto la asubuhi.Tayari Efm imekwisha mtambulisha Elizabeth Michael (Lulu) kwenye kipindi cha joto la asubuhi kujaza nafasi ilioachwa na Kitenge.Kitenge alipoulizwa juu ya kuondoka kwake Efm amesema ameondoka kwa amani kabisa,,na wala hakukua na mtafaruku wowote.
 
Mkuu sio swala la kusadikika tayar huyo nguri wa kutangaza habari za michezo nchini ameshatua wasafi fm 88.9 kwa taarifa yenu sio yeye tu wako watangazaji wenzake wa3 wametinga wasafi, utashindana na mwenye hera wewe u muweze??
 
Tatizo wao wanawasikikiza watangazaji wa kipindi husika yaani hawana ubunifu
Hawa wasafi fm hawawezi buni kitu cha tofauti naona wanafanya kama efm sports hq.
 
Mkuu uko vizur nakuelewaga sana watu wanataka maslahi sio jina la kituo au mazoea no najua baada ya mwezi mmoja tu tayar washapata jina na redio itakimbiza sana maulidi na wenzake nawakubali sana kwa show
 
Biashara ya radio ngumu sana. Ndio maana Abdallah Majura kaamua kumuuzia Mwamposa. Yaani siku hizi wanafanya kusajili kwa mbwembwe na si kuajiri.
Kuna radio hapa hapa dar huwa nakaa miezi hadi mitatu sijasikiliza, na wanatumia gharama kuendesha ujue.
 


Yuko central alishikwa ugoni jana kule Tabata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…