Huenda huyu mtangazaji wa E. FM Maulid Kitenge kapata shavu sehemu nyingine

Huenda huyu mtangazaji wa E. FM Maulid Kitenge kapata shavu sehemu nyingine

Mtangazaji maarufu wa Habari za Michezo, Maulid Kitenge, ameweka wazi kuwa ameondoka Radio EFM na sasa amehamia rasmi katika kituo cha Wasafi FM kinachomilikiwa na Mwanamuziki Diamond Platnumz.Kitenge ameondoka na watangazaji wenzake wawili ambao ni Yusuph Mkule na Mwanaidi Suleiman,Pia kwenye jopo lao amemuongeza mchambuzi maarufu wa mchezo nchini Eddo Kumwembe,ambapo watakuwa wakiendesha kipindi cha sport Arena kila siku kuanzia jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 5.Kadhalika atakuwa akichambua magazeti saa moja asubuhi kama alivyokuwa akifanya Efm kwenye kipindi cha joto la asubuhi.Tayari Efm imekwisha mtambulisha Elizabeth Michael (Lulu) kwenye kipindi cha joto la asubuhi kujaza nafasi ilioachwa na Kitenge.Kitenge alipoulizwa juu ya kuondoka kwake Efm amesema ameondoka kwa amani kabisa,,na wala hakukua na mtafaruku wowote.
 
Mkuu sio swala la kusadikika tayar huyo nguri wa kutangaza habari za michezo nchini ameshatua wasafi fm 88.9 kwa taarifa yenu sio yeye tu wako watangazaji wenzake wa3 wametinga wasafi, utashindana na mwenye hera wewe u muweze??
5d46a8b9a8474321a6528dadf9aa1c38.jpeg
Screenshot_20191017-193333_Chrome.jpeg
Screenshot_20191017-193326_Chrome.jpeg
Screenshot_20191017-193316_Chrome.jpeg
 
Mkuu uko vizur nakuelewaga sana watu wanataka maslahi sio jina la kituo au mazoea no najua baada ya mwezi mmoja tu tayar washapata jina na redio itakimbiza sana maulidi na wenzake nawakubali sana kwa show
Mikataba ya siku hizi imekuwa na mbwembwe kibao, ukikaa sehemu watu wanakupa tu mshahara hawana mbwembwe nyingine na siku upate kuna mtu anakupa mke, kiwanja+ gari lazima usaliti kundi na kwenda sehemu nono.

Wasafi inaweza kuleta ushindani wa masilahi kwenye media.
 
Biashara ya radio ngumu sana. Ndio maana Abdallah Majura kaamua kumuuzia Mwamposa. Yaani siku hizi wanafanya kusajili kwa mbwembwe na si kuajiri.
Kuna radio hapa hapa dar huwa nakaa miezi hadi mitatu sijasikiliza, na wanatumia gharama kuendesha ujue.
 
Leo katika kipindi chao cha tunanyambua na kunyumbulisha nimesikia watangazaji wenzake akina Gerald Hando na Musa Kipanya

Wakisema kuwa jana yake usiku walipewa taarifa kuwa katika kipindi cha asubuhi magazeti kinachotangazwa na huyu mtangazaji mashughuri mwenye shughuli yake kwa mbwembwe za kuvutiwa wasikilizaji bwana Maulid Kitenge kuwa hatokuwepo na mbadala wake atasoma magazeti mtangazaji mpya ambae ni Elizabeth Michael maarufu kwa jina la LULU kuwa yeye ndie amesoma siku ya leo.

Huenda huyu ndugu yetu bwana Kitenge kapata shavu sehemu au kahamishwa kitengo?

Mwenye kujua zaidi atuletee mrejesho.

Nimewasilisha.


Yuko central alishikwa ugoni jana kule Tabata.
 
Back
Top Bottom