Huenda leo ndiyo ukawa mwisho wa Mjadala wa Feitoto kwani anarejea rasmi Yanga SC

Huenda leo ndiyo ukawa mwisho wa Mjadala wa Feitoto kwani anarejea rasmi Yanga SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mama kapigiwa sana Simu (siyo za Vitisho) na Watu anaowaheshimu na wenye Nyadhifa zao na wale waliowahi kuwa nazo nchini (wenye Mapenzi mema) na Yanga SC ili amsihi Mwanae abadili Maamuzi na hatimaye Nguvu ya Mama kwa Mtoto imefanya Kazi.

Kuanzia leo Feitoto ataomba Radhi kwa Uongozi wa Yanga SC na atawaomba Radhi pia Wanachama kisha ataelekea Kambini Avic Town kuwaomba Radhi Wachezaji wenzake rasmi kurejea Kikosini.

Matajiri wa Yanga SC wamekubali Kumpa Feitoto Mshahara wa Tsh Milioni 15 na tayari wameshamnunulia Gari (japo siyo Range kama ambavyo Azam walimnunulia) na kaambiwa aseme anataka Nyumba wapi ili GSM wamalize Shughuli mapema.

Mama wa Kihistoria Kisiwani Zanzibar kwa Heshima aliyonayo Zanzibar na kwa wana Yanga SC nchini kamaliza rasmi huu Utata wote na sasa kuna 95% za Feitoto kurejea Yanga SC na Kuendelea kufumua Mashuti yake ya Kutukuka ambalo moja wapo hata Kipa wangu Aishi Manula alipishana nalo likiwa la Moto na lenye Kasi ya Kombora Vita.
 
Aaah!labda Fei huyu sio mzanzibari maana kwa msimamo wanaongoza, maswali ya kujiuliza unaachaje ofa iliyonona kisa eti kuna kasimu kamepigwa? aaah hadithi za sungura kambeba tembo, imeisha hiyo
 
Aaah!labda Fei huyu sio mzanzibari maana kwa msimamo wanaongoza,maswali ya kujiuliza unaachaje ofa iliyonona kisa eti kuna kasimu kamepigwa?aaah hadithi za sungura kambeba tembo,imeisha hiyo
Nchi hii kwenye muziki na mpira hakuna mwenye jeuri ya kuwavimbia wanasiasa wa chama tawala.

Mpka sasa swala la feisal kwenda azam haliwezekani labda wakati ujao.
 
Nchi hii kwenye muziki na mpira hakuna mwenye jeuri ya kuwavimbia wanasiasa wa chama tawala.

Mpaka sasa swala la Feisal kwenda azam haliwezekani labda wakati ujao.
Sahihi. Na hata Azam wanalikua wameingia mkenge ni vile basi tu...
 
Matajiri wa Yanga SC wamekubali Kumpa Feitoto Mshahara wa Tsh Milioni 15 na tayari wameshamnunulia Gari (japo siyo Range kama ambavyo Azam walimnunulia) na kaambiwa aseme anataka Nyumba wapi ili GSM wamalize Shughuli mapema.
Mkataba huu mpya utakuwa unaisha lini?
Signing fee kachukua sh ngapi?

Kwa kiwango ambacho anacheza fei toto sa hivi alistahili kulipwa 20m kama mshahara kwa mwezi, signing fee 400m. Na hapo angetakiwa kuongeza miaka miwili tuu kwenye mkataba ambao unaisha hiyo may 30 2024.

Na bado gari zero km na nyumba juu(japo ni vizuri zaidi gharama za nyumba na gari zingekuwa zinajumuishwa kwenye signing fee au mshahara) mchezaji apewe pesa yake ye mwenyewe ajinunulie gar anayotaka na kutafuta nyumba anayotaka.
 
utaratibu upi umevunjwa,kwamba FEI hana haki ya kuvunja mkataba mpaka klabu iridhike,akili ndogo inaweza kuwa hivyo
Hajavunja mkataba ila amenunua mkataba wake 😀😀
 
Back
Top Bottom