Huenda leo ndiyo ukawa mwisho wa Mjadala wa Feitoto kwani anarejea rasmi Yanga SC

Huenda leo ndiyo ukawa mwisho wa Mjadala wa Feitoto kwani anarejea rasmi Yanga SC

Mama kapigiwa sana Simu (siyo za Vitisho) na Watu anaowaheshimu na wenye Nyadhifa zao na wale waliowahi kuwa nazo nchini (wenye Mapenzi mema) na Yanga SC ili amsihi Mwanae abadili Maamuzi na hatimaye Nguvu ya Mama kwa Mtoto imefanya Kazi.

Kuanzia leo Feitoto ataomba Radhi kwa Uongozi wa Yanga SC na atawaomba Radhi pia Wanachama kisha ataelekea Kambini Avic Town kuwaomba Radhi Wachezaji wenzake rasmi kurejea Kikosini.

Matajiri wa Yanga SC wamekubali Kumpa Feitoto Mshahara wa Tsh Milioni 15 na tayari wameshamnunulia Gari (japo siyo Range kama ambavyo Azam walimnunulia) na kaambiwa aseme anataka Nyumba wapi ili GSM wamalize Shughuli mapema.

Mama wa Kihistoria Kisiwani Zanzibar kwa Heshima aliyonayo Zanzibar na kwa wana Yanga SC nchini kamaliza rasmi huu Utata wote na sasa kuna 95% za Feitoto kurejea Yanga SC na Kuendelea kufumua Mashuti yake ya Kutukuka ambalo moja wapo hata Kipa wangu Aishi Manula alipishana nalo likiwa la Moto na lenye Kasi ya Kombora Vita.
Thumb up brother! Navutiwa sana na aina yako ya uandishi. Nadhani waweza kuwa mchambuzi bora wa soka la bongo.
Hamia huko uachane na siasa za soka. Naamini jukwaa hili la soka la bongo litapata mtu sahihi kama tunavyofurahia uwepo wa Mosdef kwenye forum ya Liverpool.
 
Kumbe kutikisa kiberiti ni afya
 
Kuna watu wajanja bwana!! Fei aliwashtukiza wananchi wakati wanajipanga kukutana na AZAM kwa Mkapa!! Hawakutaka tukutane nae kwenye mechi hiyo muhimu akitokea upande wa pili. Akili mu kichwa. AZAM huko ataenda tu si mechi imeshapita na wananchi tulishinda!!! Kongole viongozi wa wananchi!
 
Nchi hii kwenye muziki na mpira hakuna mwenye jeuri ya kuwavimbia wanasiasa wa chama tawala.

Mpka sasa swala la feisal kwenda azam haliwezekani labda wakati ujao.
Siyo mambo ya siasa mkuu, ni jambo la kisheria tu, Azam siyo wajinga kutomtangaza toka last week, wameona grounds za kisheria zipo against wao na mchezaji. Mchezaji kuondoka kwa kununua mkataba ni very complicated ,ingekuwa rahisi kihivyo wachezaji wangekuwa wananunua mikataba yao kila siku. Nashangaa watu wanasema mkataba wa Feisal unamruhusu kulipa Sh. 112 milioni na kuondoka, ni mkataba upi huo, kile kipage kimoja kinachosambaa mtandaoni ndiyo mkataba? Wakubwa walicho mwambia Feisal na mama yake ni kutulia ili kijana asije akapata matatizo ya kufungiwa na FIFA wakati yeye ndiyo sura nzuri ya soka la Zanzibar.
 
Mama kapigiwa sana Simu (siyo za Vitisho) na Watu anaowaheshimu na wenye Nyadhifa zao na wale waliowahi kuwa nazo nchini (wenye Mapenzi mema) na Yanga SC ili amsihi Mwanae abadili Maamuzi na hatimaye Nguvu ya Mama kwa Mtoto imefanya Kazi.

Kuanzia leo Feitoto ataomba Radhi kwa Uongozi wa Yanga SC na atawaomba Radhi pia Wanachama kisha ataelekea Kambini Avic Town kuwaomba Radhi Wachezaji wenzake rasmi kurejea Kikosini.

Matajiri wa Yanga SC wamekubali Kumpa Feitoto Mshahara wa Tsh Milioni 15 na tayari wameshamnunulia Gari (japo siyo Range kama ambavyo Azam walimnunulia) na kaambiwa aseme anataka Nyumba wapi ili GSM wamalize Shughuli mapema.

Mama wa Kihistoria Kisiwani Zanzibar kwa Heshima aliyonayo Zanzibar na kwa wana Yanga SC nchini kamaliza rasmi huu Utata wote na sasa kuna 95% za Feitoto kurejea Yanga SC na Kuendelea kufumua Mashuti yake ya Kutukuka ambalo moja wapo hata Kipa wangu Aishi Manula alipishana nalo likiwa la Moto na lenye Kasi ya Kombora Vita.
Merry Christmas Genta
 
Back
Top Bottom