Umeandika kisheria
Umeandika kisheria Feisal yupo sahihi, tuwekee hiyo sheria ila tu usiweke ile mistari minne inayodaiwa ipo kwenye mkataba wa Feisal maana ni kishekesho kuweka ile mistari kama utetezi. Mkuu ITR suala Morisson tuliposikia tu yule mwanasheria wa Yanga anasema walikata maandishi ya awali kwa peni na kusaini juu tulijua ni uhuni wa viongozi wa Yanga, hili ni tofauti kabisa. Mikataba ingekuwa inavunjwa hovyo hovyo hivyo bila upande wa pili kuridhia kusingekuwa na umuhimu wa kusaini mkataba na kungekuwa vurugu kubwa kwenye uhamisho wa wachezaji. Hivi wewe hujiulizi kwa nini Azam wanakana kuhusishwa huku Feisal akiwa ameingiza fedha acount ya Yanga toka tarehe 23? Feisal ameshaaga Yanga lakini Azam hawajathubutu siyo tu kumtangaza hata kukiri kumtaka tu.