Siamini kama Magori ni pandikizi la Yanga. Lakini naamini Magori anapenda sana mpira na anaipenda sana Simba lakini mpira haujui na hata wachezaji wazuri wenye viwango hajui kabisa. Na hata sajili zake anaangalia zaidi takwimu za mchezaji na clip kuliko kumuona mchezaji halisi. Mfano mmoja tu Doumbia kwao alifunga magoli mengi sana kwao lakini karibia yote yalikuwa ya penati na vichwa tena free header. Mtu yoyote anayeujuwa mpira hata angeangalia tu clip za Doumbia kabla hajamuona uwanjani katu abadani hawezi kumsajili.
Mchezaji kama huyo unamleta kwenye ligi ambayo mabeki hata wa timu ndogo hawakupi hiyo nafasi ya kuruka mwenyewe ufunge. Na hata kuruka kwenyewe tu shida maana jana kuna krosi mbili kashindwa kabisa hata kuruka afunge. Lile umbo lake halina faida yoyote. Na kwa hili Simba wasione aibu wakubali tu hasara wamtoe kwa mkopo wasajili mshambuliaji mwingine.
Na kitendo cha MO kuendelea kumkumbatia Magori ndio anguko lake linakuja muda si mrefu maana wanasimba washaanza kuwachoka tajiri na chawa wake. Kwa aliye karibu na Mo amshtue kuwa aidha amtose au waende wote.