Huenda Mkoa wa Morogoro ukagawanywa na kuwa mikoa miwili; Morogoro na Kilombero

Huenda Mkoa wa Morogoro ukagawanywa na kuwa mikoa miwili; Morogoro na Kilombero

Duru toka Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa zinatabanaisha kuwa Mkoa wa Morogoro huenda ukagawanywa na kuwa mikoa miwili kwa maana ya Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Kilombero.

Inasemekana makao makuu ya mkoa mpya wa Kilombero yatakuwa IFAKARA MJINI na utakuwa na wilaya nne nazo ni Wilaya ya ULANGA, wilaya ya MBINGU, Wilaya ya MALINYI na Wilaya ya IFAKARA.

Mungu ibariki Tanzania na Timu ya Yanga.
Mkoa wa Morogoro kama kugawanyika ni kuzaa mkoa mpya wa KILOSA na makao makuu yake ni mjini Kilosa. Hivyo, mkoa wa Morogoro kiutawala unaweza kugawanyika katika wilaya za Morogoro, Kilombero, Ulanga, Malinyi na sehemu ya tarafa za Mvomero. Na mkoa mpya itapendeza jina la Kilosa; na ukaundwa na wilaya za Kilosa, Gairo sehemu za tarafa ya Mvomero na tarafa Mpwapwa au tarafa ya Mlali ya Kongwa kwa mkoa Dodoma. Kumbuka haya ni maoni tu !


Mipaka na ukubwa wa Mkoa ni eneo la kilometa za mraba 73,039. Eneo hili ni sawa na asilimia 7.7 ya eneo lote la Tanzania Bara, kati ya eneo hili Km2 2,240 ni eneo la maji. Mkoa umepakana na Mikoa ya Pwani na Lindi kwa upande wa Mashariki, Manyara na Tanga kwa upande wa Kaskazini na kwa upande wa Magharibi umepakana na Mikoa ya Dodoma na Iringa na Upande wa Kusini unapakana na Mkoa wa Ruvuma na Njombe. Tukumbuke kwamba Morogoro ni mkoa wa pili kwa ukubwa hapa nchini kwa sasa ukitanguliwa na Mkoa wa Tabora.
 
Duru toka Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa zinatabanaisha kuwa Mkoa wa Morogoro huenda ukagawanywa na kuwa mikoa miwili kwa maana ya Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Kilombero.

Inasemekana makao makuu ya mkoa mpya wa Kilombero yatakuwa IFAKARA MJINI na utakuwa na wilaya nne nazo ni Wilaya ya ULANGA, wilaya ya MBINGU, Wilaya ya MALINYI na Wilaya ya IFAKARA.

Mungu ibariki Tanzania na Timu ya Yanga.
Ni jambao jema kwa maendeleo ya nchi.
 
Mkoa wa Morogoro una ukubwa wa eneo 70,624 km za mraba.

Netherlans ina ukubwa wa 41,543 km² na Belgium ina ukubwa wa 30,689 km². Kwa mantiki Morogoro ni kama nchi mbili za Ulaya.

Mwaka 2019 Netherlands iliuza nje (exports) mafuta ya mawese yenye thamani ya US$1 billion sawa ni Tril2.3 za TZS.

Wakati "mabeberu" wanazalisha kwa tija sehemu ndogo sana ya ardhi waliyonayo kwa kuongeza thamani ya kile kinachozalishwa na ku-export na kupata Dola (fedha ya kigeni); sisi kuna watu wanawaza kugawa mikoa, ofcourse kuzalisha ajira mpya kama itatokea za
RC
RAS
RSO
RPC
Mkuu wa PCCB
karibia wote hawa wanatumia V8 iwe ni GX, VX, GXR; well kuna ulazima kuwatuza viongozi wetu kwa kazi ngumu wanazofanya; kwa ku-import toyota au Nissan patrol na kuwapelekea wajapan dola;

Ni lini sisi Tanzania tutafikiria kwa mkakati ili kuongeza uzalishaji kwa consumable products ili ku-cut down imports ya what we are consuming locally?
Nimetoka Zambia kama majuma 4 yaliyopita, nikitembelea supermarkets hapakuwa na korosho kabisa; na mwenyeji wangu niliekuwa naongea nae akaniambia wana tamani kupata korosho za kula ila hamna; sisi tuko busy ku-export raw cashews kwenda vietnam.
Wakati huo bank ya uwekezaji imebakiza 88% ya fedha ambazo ilitakiwa zikopeshwe kwa miradi ya maendeleo ya Tanzania ikiwamo kuanzisha viwanda.
Ukifika bank ya uwekezaji wanataka Collateral yenye thamani ya 125% ya mkopo unaokopa 😳😳😳;

Kuna wakati tuna watu kwenye authirities hawako serious ya inclusive and suitable community economic development; wako tayari kufanya maigizo mbele ya kamera kuonekana wanafanya kazi ili wasitumbuliwe na #1, wakati ndani ya mioyo yao, wana IQ ndogo sana (japo wa vyeti vya ufaulu in the name of qualification) ya nini tufanye ili kupigana na maadui umasikni.

Tutafika 2025, Rais mpya atakuja na kampeni yet, kuna basics za kuondoa umasikini with right strategy.

Heri ya mwaka mpya; bado nawaza, inakuwaje nchi ndogo kama Malysia ambayo ilikuja Tanzania kuchukua mbegu za Mawese, leo ni 2nd in the volume of global export, ila sisi tunashangaa.
Japo majibu baadhi yetu twajua na nini kifanyike twajua, ila wenye mamlaka ya kusaidiana nasi nini tufanye ni kama hawajui nini cha kufanya, baadhi ukiwafuata wanajifanya wanajua na hicho wanachodhani wanajua huoni kikifanyiwa kazi;

Mungu isaidie Tanzania. ina all ita takes kuwa nchi yenye zaidi ya kiwango cha uchumi wa kipato cha kati, ila wale wenye mamlaka ni kama hawako tayari, simply "wao" wana qualifications ambazo zimetundikwa kwenye nyumba zao kwa kumbukizi ya majoho walioyovaa wakati wana gradute miaka ya late '70 early '80; ila in less than 40 years toka wamalize vyuo hawana solution ya nini kifanyike; wao wana-enjoy maisha ya V-8 wanawajuza vijana graduates kama wao, oyaa "nendeni mkajiajiri"

Shalom
 
Back
Top Bottom