Mkoa wa Morogoro una ukubwa wa eneo 70,624 km za mraba.
Netherlans ina ukubwa wa 41,543 km² na Belgium ina ukubwa wa 30,689 km². Kwa mantiki Morogoro ni kama nchi mbili za Ulaya.
Mwaka 2019 Netherlands iliuza nje (exports) mafuta ya mawese yenye thamani ya US$1 billion sawa ni Tril2.3 za TZS.
Wakati "mabeberu" wanazalisha kwa tija sehemu ndogo sana ya ardhi waliyonayo kwa kuongeza thamani ya kile kinachozalishwa na ku-export na kupata Dola (fedha ya kigeni); sisi kuna watu wanawaza kugawa mikoa, ofcourse kuzalisha ajira mpya kama itatokea za
RC
RAS
RSO
RPC
Mkuu wa PCCB
karibia wote hawa wanatumia V8 iwe ni GX, VX, GXR; well kuna ulazima kuwatuza viongozi wetu kwa kazi ngumu wanazofanya; kwa ku-import toyota au Nissan patrol na kuwapelekea wajapan dola;
Ni lini sisi Tanzania tutafikiria kwa mkakati ili kuongeza uzalishaji kwa consumable products ili ku-cut down imports ya what we are consuming locally?
Nimetoka Zambia kama majuma 4 yaliyopita, nikitembelea supermarkets hapakuwa na korosho kabisa; na mwenyeji wangu niliekuwa naongea nae akaniambia wana tamani kupata korosho za kula ila hamna; sisi tuko busy ku-export raw cashews kwenda vietnam.
Wakati huo bank ya uwekezaji imebakiza 88% ya fedha ambazo ilitakiwa zikopeshwe kwa miradi ya maendeleo ya Tanzania ikiwamo kuanzisha viwanda.
Ukifika bank ya uwekezaji wanataka Collateral yenye thamani ya 125% ya mkopo unaokopa 😳😳😳;
Kuna wakati tuna watu kwenye authirities hawako serious ya inclusive and suitable community economic development; wako tayari kufanya maigizo mbele ya kamera kuonekana wanafanya kazi ili wasitumbuliwe na #1, wakati ndani ya mioyo yao, wana IQ ndogo sana (japo wa vyeti vya ufaulu in the name of qualification) ya nini tufanye ili kupigana na maadui umasikni.
Tutafika 2025, Rais mpya atakuja na kampeni yet, kuna basics za kuondoa umasikini with right strategy.
Heri ya mwaka mpya; bado nawaza, inakuwaje nchi ndogo kama Malysia ambayo ilikuja Tanzania kuchukua mbegu za Mawese, leo ni 2nd in the volume of global export, ila sisi tunashangaa.
Japo majibu baadhi yetu twajua na nini kifanyike twajua, ila wenye mamlaka ya kusaidiana nasi nini tufanye ni kama hawajui nini cha kufanya, baadhi ukiwafuata wanajifanya wanajua na hicho wanachodhani wanajua huoni kikifanyiwa kazi;
Mungu isaidie Tanzania. ina all ita takes kuwa nchi yenye zaidi ya kiwango cha uchumi wa kipato cha kati, ila wale wenye mamlaka ni kama hawako tayari, simply "wao" wana qualifications ambazo zimetundikwa kwenye nyumba zao kwa kumbukizi ya majoho walioyovaa wakati wana gradute miaka ya late '70 early '80; ila in less than 40 years toka wamalize vyuo hawana solution ya nini kifanyike; wao wana-enjoy maisha ya V-8 wanawajuza vijana graduates kama wao, oyaa "nendeni mkajiajiri"
Shalom