Tetesi: Huenda ni ujinga wangu ila huenda nikielimishwa nitaelewa

Tetesi: Huenda ni ujinga wangu ila huenda nikielimishwa nitaelewa

shirima Mathias

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2017
Posts
451
Reaction score
1,333
Hadi muda huu nakaribia miaka 60 sijui maana au sababu hasa ya kukimbiza mwenge. Jf ya wabobezi nisaidieni mwenge una tofauti gani na KIBATARI kikubwa?
IMG-20190816-WA0002.jpeg
 

Attachments

  • IMG-20190816-WA0002.jpeg
    IMG-20190816-WA0002.jpeg
    48.5 KB · Views: 28
Nakumbuka dada zangu waliniambia walikuwa wanachangishwa shilingi 20 ,20 za mafuta ya Mwenge.Nyerere alikuwa fisadi jamani.Kuwachangisha wananchi masikini mafuta ya mwenge hapana kabisa aisee.
 
Kibatari kikubwa kinatoa mwanga mkubwa ili mwenye kukitumia aweze kuona pasipo na chenga wakati Mwenge unalenga kuwafanya wafuasi wa CCM na serikali yake wawe wanawaza kama misukule au mazezeta!

Tofauti ay pili, ni kwamba kibatari kikubwa ni msaada kwa wanafunzi wanaoishi maeneo yasiyo na umeme hususani vijijini, wakati Mwenge unalenga kusambaza mimba za mapema vijijini ili CCM iendelee kupata wafuasi wengi zaidi ambao hawana shule kichwani.

Tofauti ya tatu ni kwamba, wakati kibatari kikubwa ni chanzo cha mapato kwa wafanyabiashara wauza mafuta ya taa, kwa upande wa pili, mwenge ni chanzo cha kwiba mapato ya wafanyabiashara wanazoibiwa kwa mtindo wa kuchangia mwenge.

Hizo ndio tofauti kuu tatu kati ya mwenge na kibatari kikubwa, kwahiyo usilinganishe kibatari na mambo ya kijinga tafadhali! Hata hawa wanaopanga mauaji ya Watanzania wenzao hivi sasa, na wenyewe wengine walisoma kwa vibatari vikubwa!
 
Nakumbuka dada zangu waliniambia walikuwa wanachangishwa shilingi 20 ,20 za mafuta ya Mwenge.Nyerere alikuwa fisadi jamani.Kuwachangisha wananchi masikini mafuta ya mwenge hapana kabisa aisee.

Kwamba Nyerere alikuwa fisadi???????

Okay, mwaka gani walichangishwa
 
Kwamba Nyerere alikuwa fisadi???????

Okay, mwaka gani walichangishwa
Nyerere alikuwa fisadi wa mawazo ,hata mimi nakumbuka kusema zidumu fikra za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.shule ya msingi miaka ya tisini na sita tuliimba Naapa Naahidi mbele ya chama ,mapinduzi nitakulinda mpaka kufa.Yaani walihakikisha wanafisadi mpaka akili za watoto shule za msingi.Yaani akija waziri siku hiyo hakuna masomo ni kuimba nyimbo za kusifia chama.
 
Hii dhana ya kishirikana kwamba Mwenge unawapumbaza watanzania naikataa kwa nguvu zote. Ila aina ya ulazimishaji watanzania kuuheshimu huo mwenge nayo pia sikubaliani nayo!!
Haijalishi kama ni ushirikina au vinginevyo, lakini ukweli ni kwamba, Mwenge umeficha siri mzito sana ambayo si ya kawaida! Just imagine Magu alivyoingia madarakani na mbwembwe za kubana matumizi! Kwanza akaanza kufuta sheria ya kupongezana kule bungeni, siku chache baadae akafuta sherehe za Uhuru! In no time, sherehe za Mwenge zikawadia na Magu akasanda!!!

Na kila sababu ya kuamini Magu haendelei kukimbiza mwenge kwa ridhaa yake, vinginevyo ingekuwa keshafuatilia mbali!
 
Nakumbuka dada zangu waliniambia walikuwa wanachangishwa shilingi 20 ,20 za mafuta ya Mwenge.Nyerere alikuwa fisadi jamani.Kuwachangisha wananchi masikini mafuta ya mwenge hapana kabisa aisee.
Mpaka sasa zinachangishwa kwa wananchi Wa kada mbalimbali....
 
Mwenge kwa nyakati hizi hauna faida,sana sana ni kichaka cha ngono na pombe!Nenda sehemu mwenge unapolala utaelewa nin namaanisha,ishakuwa laana tofauti na zamani!
 
Je, kuna nchi nyingine yoyote ulimwenguni ambayo huwa kinakombiza mwenge kama tunavyofanya hapa nchini!
 
Mwenge ni alama ya taifa, alama za taifa ni sacred symbols kwa maana kwamba zina maana fulani inayoishi kiroho. Hivyo kuiondoa si jambo rahisi ila inawezekana. Hata ukiacha kuukimbiza haiondoi maana yake kiroho, let's hope for that day to come
 
Mwenge uliasisiwa na Forojo Ganze si Mwl Nyerere
 
Back
Top Bottom