Tetesi: Huenda ni ujinga wangu ila huenda nikielimishwa nitaelewa

Tetesi: Huenda ni ujinga wangu ila huenda nikielimishwa nitaelewa

Nyerere alikuwa fisadi wa mawazo ,hata mimi nakumbuka kusema zidumu fikra za mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.shule ya msingi miaka ya tisini na sita tuliimba Naapa Naahidi mbele ya chama ,mapinduzi nitakulinda mpaka kufa.Yaani walihakikisha wanafisadi mpaka akili za watoto shule za msingi.Yaani akija waziri siku hiyo hakuna masomo ni kuimba nyimbo za kusifia chama.
Hiyo kiapo cha uzalendo inatofauti gani na hii ideology mpya ya uzalendo ya wanaMATAGA wa leo?
 
Mbio za mwenge zinaweza kuwa na gharama kubwa lakini kuna ujumbe wa mshikamano na utaifa nyuma ya ukimbizaji wake.

Mataifa mengi ya Afrika yamekuwa yakiingia katika vita za wenyewe kwa wenyewe, chanzo ni uwepo wa nchi yenye bendera lakini inayokosa utaifa ndani yake.

Ukiishi na wanigeria utaugundua mara moja ukosefu huo wa utaifa, utawasikia wakijitambulisha kimakabila na kikanda tofauti na sisi tunapokuwa huko nje, tunajitambulisha kama watanzania kwanza.

Inakuwa rahisi kwa mchagga kwenda kuoa mgoni wakati nchi ikiwa na utaifa mkubwa. Inakuwa rahisi kwa mmakonde kwenda kuoa mhaya, wote wawili wanatambua maana ya utaifa.

RIP Julius Nyerere hakufanikiwa kwenye uchumi lakini atadumu daima katika nafsi za watu kwa kuweza kuujenga utanzania, na mbio za mwenge ni njia mojawapo zinazofanikisha kuulinda utaifa wetu.
 
Back
Top Bottom