Huenda hotuba hii ya Askofu Mwanamapinduzi ndio chanzo cha yeye kukamatwa na Polisi.
=======
Askofu Machumu: Chini ya Serikali ya mama Samia Suluhu Hassan, yeye ndio ameamua rasmi kuiuza Tanganyika, naomba iwe wazi hiyo. Yeye ameamua rasmi kuiuza Tanganyika kuanzia bandari zake, misitu, mapori yake tena ameuza kwa waarabu.
Kama wanadai nimesema uongo, watuambie ile mikataba waliofanya kule Dubai, mikataba 39 inahusu nini?
Tumewekewa mikataba miwili, mkataba wa kwanza, mkataba wa bandari. Ule mkataba wa bandari ukiusoma, unasema kwamba bandari zinakabidhiwa kwa waarabu mpaka shughuli za bandari zitakapoisha maana yake ni kwamba mpaka Yesu arudi.
Tunauliza, ni kwa shilingi ngapi hatuambiwi. Magufuli alipoingia madarakani alikuta mkataba mmoja wa kuuza bandari ya Bagamoyo. Bandari ile ilikuwa inakabidhiwa kwa wachina kwa miaka 99 ila watajenga wenyewe.
Akasema mkataba huu, mtu yeyote anayetaka kuingia mkataba huu lazima kwanza awe chizi na mwendawazimu.
Sasa mama Samia nitafutieni jina la kumpa maana kama ni uchizi ameshazidi hapo. Ameuza bandari sio moja, ameuza bandari 54 za Tanganyika za kwenye bahari mpaka maziwa, kwa miaka mingapi hatujui, kwa shilingi ngapi hatujui!
Mimi nawaambia ukweli, mama huyu tumalizane naye safari hii, tumalizanane naye Serikali za mtaa, msichague chama chake. Mkichagua CCM atapata nguvu ya kugombea, kama amewauza kwenye awamu yake ya kwanza, awamu ya pili atawafanyaje!
Pia soma:
Singida: Baba Askofu Machumu akamatwa kwa Uchochezi