Huenda sababu ya Rais Samia kukaa kimya ni hii hapa!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Tofauti na watu wengine Raisi Samia akiongea lolote kuhusu mkataba wa DP world litamfikia mkuu wa wa Dubai. Sasa tatizo ni nini?

1. Kwanza akisema mazuri tu itakuwa vigumu kwenda kwao tena na kurekebisha mkataba
2. Akisema mabaya ya mkataba wazi wazi watajitoa kwenye mkataba mzima kitu ambacho hawezi kufanya.

Hivyo marekebisho yatafanya na watu wa chini yake. Dubai wana utamaduni wa kifalme na huu utamaduni unawafanya wamweke Raisi wetu kwenye level ya juu kama ufalme wao.

Hivyo ndiyo maana Rais Samia kafugwa mdomo maana akisema lolote ni tatizo.
 
Hakuna anayekataa uwekezaji bali ni aina ya makubaliano kuhusiana na huo uwekezaji
nguvu kubwa inayotumika ni kutaka kuua dhana ya uwekezaji kwenye vichwa vya watanzania jambo ambalo si sawa
 
Nimesoma vizuri mkataba nimkataba mbovu kuwahiii kutokeaa katika history ya nchiii hiii
 
Takataka. Hajakaa kimya on a purely bona fide basis. Kwani yeye ni nani? Mungu wa Watanzania wote hadi kimya chake kiwe chanzo cha tafsiri tofauti na mbalimbali? Kuna pesa ndefu imetembea na CCM watanufaika 2024-2025 kwenye chaguzi .
 
kwa nini mnakubali kudanganyika kirahisi namna hii.
hivi mnafikiri ccm hawana nia njema kwa taifa sijui akili naziweka wapi kwa kweli
Kwani wewe hauoni tunavyodaiwa mabilioni ya fedha kwa kuingia mikataba kibubusa??
 
nguvu kubwa inayotumika ni kutaka kuua dhana ya uwekezaji kwenye vichwa vya watanzania jambo ambalo si sawa
Umeambiwa hakuna mtanzania anayekataa uwekezaji. Tatizo ni aina ya mkataba na mapungufu yake, au wewe huoni mapungufu?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…