Huyo jamaa hajui hesabu. Analinganisha bei ya data badala ya kulinganisha vipato vya watu kutoka hayo mataifa. Kuna kitwa kinaitwa "purchasing power parity" ndio kinaamua kama bei iko juu au chini. Ni sawa na embe kuuzwa dolar 2 Marekani ambayo ni roughly TZS 4,600. So kw marekani kununua embe kwa dolar mbili ni very cheap lakini kwa Tanzania ni ghali sana. Kwa hiyo gb 1 ikiuzwa dolar 2 kwa itaonekana ghali kwa Tanzania lakini kwa Marekani itaonekana very cheap. Huyu mleta mada inaonekana anatoka familia ya Magufuli hivyo kwao hawana shida ya hela
Yaani wewe mkuu ni wale watu ambao wanaongea maneno mengi ili kuwatoa watu wenye hoja ya msingi relini. Ila hapa andika umenoa. Hata uje na maneno mengi ukidhani utanichanganya na kunitoa relini andika maumivu. Nilishadeal na watu dizaini yako wengi sana. Hapa nilipo nina mchepuko wangu ana tabia kama yako, akifanya kosa atajifanya kuwa yeye ndio victim, kwanza ataanza kujilalamisha eti simpendi, pili ukianza kumuuliza maswali anaanza kuongea maneno mengi ya kujifanya yeye ndio mhanga ili akutoe kwenye reli. So huwa namsikilizaaa, akimaliza namwambia hunitoi kwenye reli, jibu swali langu. Kwa nini umefanya a,bc?
Sasa nirudi kwako. Umeuliza maswali mengi kwa kudhani utanifanya nishindwe kusimamia hoja yangu. Hayo maswali ni brah brah tu, point inabaki data kuwa juu inategemea na kipato cha wanunuzi. Swala la makampuni kuuziwa hizo data sijui na billgate or whoever ni irrelevant. Hiyo miuondo mbinu ya mawasiliano kama minara haiishi wala kuharibika kisa watu wanatumia data. Hayo maminara ya simu yakishasimikwa haijalishi watu wengi wanatumia data au hawatumii yataendelea kuwepo hadi yatakapochakaa menyewe due to depreciation au kuzeeka, au kuoza kwa kunyeshewa na mvua ila si kwamba watu wanapopiga simu au kutumia data.
Halafu haya makampuni ya simu hayanunui data kama unavodai wewe. Sisi wateja ndio tunaonunua data, wao (kampuni za simu) wanapata commision kutokana na sisi kutumia internet, kwa hiyo kadri wanavyotupiga sisi kwenye data ndio wanavyopata commision kubwa kutoka kwa hao wa kina Billgate na hao wakina Markzuburg.
Kwa kuhitimisha, jikite kwenye hoja uliyoileta mwenyewe. Bei ya data kuwa kubwa haipimwi kwa bei ya data kati inchi na nchi bali inapimwa kwa uwezo wa watu wa kununua data.