Huenda ukastaajabu. Lakini huu ulikuwa upande wa pili wa maisha yangu ndani ya JamiiForums

Huenda ukastaajabu. Lakini huu ulikuwa upande wa pili wa maisha yangu ndani ya JamiiForums

Naona unatoa ya moyoni
20220531_214454.jpg
 
Du! wana JF tutafika mbinguni tumechoka sana,kwahio unaanzisha mada,unabishana nayo kwa ID nyingine halafu mtu anakuunga mkono kumbe wewe unamchora tu

Halafu hii ya kujifanya mwanamke lengo inakuwa nini?
Attention seeking disorder.

Kuna mwingine yule jamaa wa matusi Gentamycine,pia Kuna mkulungwa/zee korofi.

Hawa watu wanasumbuliwa na;

1.Bipolar

2.Oestrogen homones (mwanaume aliyetimia hawezi kufanya huu upuuzi). Imagine mtu Kama Ushimen anauingia mkenge wa kutongoza I'd ya roselyn Kumbe Ni kijamaa kina makende.

3.Malezi mabovu..Mtu aliyelelewa vizuri na wazazi hawezi kuwatukana wenzie bila sababu za msingi Ili tu kuwasababishia ban Kama wafanyavyo hawa watu.

Utagundua watu wenye IDs nyingi ni watu wenye matusi Sana na hawana adabu Wala hekima kwa members wenzao.

Hawa watu wanatakiwa wachukuliwe hatua Kali sana maana mtu kuwa na IDs nyingi ana uwezekano mkubwa wa kuwatapeli watu humu ndani.
 
Du! wana JF tutafika mbinguni tumechoka sana,kwahio unaanzisha mada,unabishana nayo kwa ID nyingine halafu mtu anakuunga mkono kumbe wewe unamchora tu

Halafu hii ya kujifanya mwanamke lengo inakuwa nini?
Kulikuwa na shidano la member bora Jukwaa la Sports. Ndipo mtaalamu GENTAMYCINE akaibua ID zake zote mafichoni. Akajipigia kura kisha akashinda
 
[emoji23][emoji23][emoji23]We acha tu mkuu! "No Woman, no cry". Hapo ndipo nilipoamini kwanini Adam alirubuniwa kula tunda akakubali. Wanaume tu wadhaifu, tujipige kifuani mara tatu na tuseme Mola atusaidie

Watu walipasuka asikwambie mtu! Full miamala, kama Zuwena vile
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Habari za wakati huu wakuu,

Ni nusu mwaka sasa tokea kuwa "The Storyteller" aliyestahili tuzo humu jukwaani. Ni muda mrefu sana umepita tokea pale nilipoifahamu na kujiunga na jumuiya, japokuwa mlio wengi mtachungulia kwa profile ili kuona lile neno "joined Nov 2022", JF nimeifahamu kwa zaidi ya miaka kadhaa iliyopita

Mbali na ID ya Melki the Storyteller ,pia nina ID mama ambayo sitoiweka wazi kwa miaka hii, japokuwa ni ID kubwa na pendwa ambayo inatema madini yenye mantiki na yenye kukubalika. Katika ID hiyo nimeishi maisha yasiyo halisi kwa 100% na hakuna mtu anaweza / ataweza shitukia. Niwashukuru kwa kuniheshimisha kupitia hiyo ID

Je, The Storyteller wetu ana IDs nyingine za ziada mbali na hizo mbili tajwa hapo juu?

Jibu ni HAPANA. Lakini kwa kipindi cha nyuma nimewahi kuwa nazo kadhaa. Ndani ya JamiiForums nimeishi maisha ya uzee, ujana, usomi, ushamba, utoto, michezo, uganga, siasa n.k

Sometimes niliunda uzi na kuanza kuchangia mwenyewe huku nikibishana na kujitukana kwa ID hii na kusuluhisha kwa ID nyingine, lengo ni kusogeza uzi na kuufanya uzi kupamba moto

Niwaombe mniwie radhi kwa utoto nilioufanya kipindi cha nyuma, lakini sina budi kuuweka wazi siku ya leo

a) izo biz Hii ilikuwa ID yangu pendwa niliyoikubali kupita maelezo. Sikuwahi pitwa na tukio nisilielezee ndani ya ID hii. Nilifanikiwa kuunda nyuzi nyingi sana zenye mantiki na zisizo na mantiki ndani ya ID hii. Nikiachana na ID hii baada ya kuona wanachama wameanza kuignore post zangu na kudhani huenda zikawa ni chai, kitu ambacho sio kweli
View attachment 2618355
ID za karan lutha na wamatukio zilishika hatamu baada ya ID ya izo biz kususwa. Karan Lutha alitumika kuleta visa "serious" na hoja za msingi ambazo zilihitaji utatuzi makinifu ambazo kama zingewekwa kwenye ID ya izo biz zingekuwa ignored
View attachment 2618358
ID ya Wamatukio ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya Jokes na mikasa ya kuchekesha. Nahisi ni ID iliyokuwa pendwa kulinganishwa na izo biz ama karan lutha
View attachment 2618360
Tukiachilia mbali na IDs tajwa hapo juu, ID ya roselyn2 ilikuwa ni ID yangu pia. Hii niliitumia kwa ajili ya attention pamoja na changamsha kijiwe, japo kuna watu wachache walishtukia pasi na uhakikaView attachment 2618362
Baada ya kukomaa kifikra na kiakili, niliamua kuzichinjilia mbali ID hizi kwa namna ambayo ninaifahamu mimi i.e kwa IT ndogo niliyonayo kumkichwa

Nimeona ni vyema kuja kutubia makosa yangu hapa na kwa wakati huu. Kwa wale wote ambao niliwakwaza kupitia ID zangu, naombeni tusameheane na tuendeleze jukumu la kulijenga taifa

Narudi kwa ushuhuda zaidi...
Aiseee 😲
 
Sometimes niliunda uzi na kuanza kuchangia mwenyewe huku nikibishana na kujitukana kwa ID hii na kusuluhisha kwa ID nyingine, lengo ni kusogeza uzi na kuufanya uzi kupamba moto


[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom