Huenda ukastaajabu. Lakini huu ulikuwa upande wa pili wa maisha yangu ndani ya JamiiForums

Huenda ukastaajabu. Lakini huu ulikuwa upande wa pili wa maisha yangu ndani ya JamiiForums

Umaskini wa nchi shida sio viongozi tu! Hata wananchi tuna pigo za ajabu sana
[emoji23][emoji23][emoji23] Hapa ningekuwa na ID zangu za kazi. Karan lutha angeanza kukupopoa. Halafu izo biz angeungana na wewe kujibu mashambulizi

Wamatukio angekuwa analiamsha tu pale anapoona kama mnaenda kujisahaulisha

Roselyn2 angewapatanisha PM, kisha muanze kumtongoza. Na kila mtu angesindikiza muamala, mmoja muamala sahihi, mwingine muamala wa mchongo
 
Habari za wakati huu wakuu,

Ni nusu mwaka sasa tokea kuwa "The Storyteller" aliyestahili tuzo humu jukwaani. Ni muda mrefu sana umepita tokea pale nilipoifahamu na kujiunga na jumuiya, japokuwa mlio wengi mtachungulia kwa profile ili kuona lile neno "joined Nov 2022", JF nimeifahamu kwa zaidi ya miaka kadhaa iliyopita

Mbali na ID ya Melki the Storyteller ,pia nina ID mama ambayo sitoiweka wazi kwa miaka hii, japokuwa ni ID kubwa na pendwa ambayo inatema madini yenye mantiki na yenye kukubalika. Katika ID hiyo nimeishi maisha yasiyo halisi kwa 100% na hakuna mtu anaweza / ataweza shitukia. Niwashukuru kwa kuniheshimisha kupitia hiyo ID

Je, The Storyteller wetu ana IDs nyingine za ziada mbali na hizo mbili tajwa hapo juu?

Jibu ni HAPANA. Lakini kwa kipindi cha nyuma nimewahi kuwa nazo kadhaa. Ndani ya JamiiForums nimeishi maisha ya uzee, ujana, usomi, ushamba, utoto, michezo, uganga, siasa n.k

Sometimes niliunda uzi na kuanza kuchangia mwenyewe huku nikibishana na kujitukana kwa ID hii na kusuluhisha kwa ID nyingine, lengo ni kusogeza uzi na kuufanya uzi kupamba moto

Niwaombe mniwie radhi kwa utoto nilioufanya kipindi cha nyuma, lakini sina budi kuuweka wazi siku ya leo

a) izo biz Hii ilikuwa ID yangu pendwa niliyoikubali kupita maelezo. Sikuwahi pitwa na tukio nisilielezee ndani ya ID hii. Nilifanikiwa kuunda nyuzi nyingi sana zenye mantiki na zisizo na mantiki ndani ya ID hii. Nikiachana na ID hii baada ya kuona wanachama wameanza kuignore post zangu na kudhani huenda zikawa ni chai, kitu ambacho sio kweli
View attachment 2618355
ID za karan lutha na wamatukio zilishika hatamu baada ya ID ya izo biz kususwa. Karan Lutha alitumika kuleta visa "serious" na hoja za msingi ambazo zilihitaji utatuzi makinifu ambazo kama zingewekwa kwenye ID ya izo biz zingekuwa ignored
View attachment 2618358
ID ya Wamatukio ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya Jokes na mikasa ya kuchekesha. Nahisi ni ID iliyokuwa pendwa kulinganishwa na izo biz ama karan lutha
View attachment 2618360
Tukiachilia mbali na IDs tajwa hapo juu, ID ya roselyn2 ilikuwa ni ID yangu pia. Hii niliitumia kwa ajili ya attention pamoja na changamsha kijiwe, japo kuna watu wachache walishtukia pasi na uhakikaView attachment 2618362
Baada ya kukomaa kifikra na kiakili, niliamua kuzichinjilia mbali ID hizi kwa namna ambayo ninaifahamu mimi i.e kwa IT ndogo niliyonayo kumkichwa

Nimeona ni vyema kuja kutubia makosa yangu hapa na kwa wakati huu. Kwa wale wote ambao niliwakwaza kupitia ID zangu, naombeni tusameheane na tuendeleze jukumu la kulijenga taifa

Narudi kwa ushuhuda zaidi...
Ulikuwa na muda wa kupoteza..
 
That’s not a Childish [emoji1578] it’s a seriously Mental Health Issue[emoji205]
[emoji23][emoji23] Hapa ningekuwa na ID zangu za kazi. Karan lutha angeanza kukupopoa. Halafu izo biz angeungana na wewe kujibu mashambulizi

Wamatukio angekuwa analiamsha tu pale anapoona kama mnaenda kujisahaulisha

Roselyn2 angewapatanisha PM, kisha muanze kumtongoza. Na kila mtu angesindikiza muamala, mmoja muamala sahihi, mwingine muamala wa mchongo
 
Wakati unatongozwa as rosy ulikua unajisikia[emoji23]
[emoji23][emoji23]Kuna Sister mmoja nilimuachia PM ili afanye yake, japo anadai zilimzidia. Zingine aliziweka Pending. Hata ID yangu ya izo biz imewahi kumtongoza roselyn2

Kazi yangu ilikuwa ni kuunda nyuzi tu, bila kusahau maneno kama "kweli tena.." na tu-emoji ili kuwaaminisha watu
 
Ndo maana huwa siwaamini sana hawa wanaoweka picha za mapaja, lips,vimdoli na videmu vya ki Asia kwenye I'd zao, wengi ni masela
Ukijichanganya na tamaa za kiwaki unatapeliwa chap tu.

Au ukibahatisha akawa dem wa kweli basi ile picha uliyojijengea kichwan kuwa atakua Dem wa dizain hii atakushangaza unaweza kukutana na mmama analingana na shangazi yako ila hapa jf ana behave kama kabinti kasiko na hatia
Eti kabinti kasiko na hatia[emoji23][emoji23] Nimecheka sana aisee
 
Only the fools will tell the truth [emoji1787] waiting for ignore from several members [emoji1787][emoji1787][emoji2506][emoji475][emoji473][emoji1733][emoji3104]
Kwa hiyo unaniweka kwenye ignore list mkuu? Licha ya madini ninayoyamwaga Jamii Check?
 
[emoji23][emoji23][emoji23]We acha tu mkuu! "No Woman, no cry". Hapo ndipo nilipoamini kwanini Adam alirubuniwa kula tunda akakubali. Wanaume tu wadhaifu, tujipige kifuani mara tatu na tuseme Mola atusaidie

Watu walipasuka asikwambie mtu! Full miamala, kama Zuwena vile
😂😂😂 jinga sana wewe
 
Back
Top Bottom