Hujafa hujaumbika: Msanii Justin Bieber apatwa na ugonjwa wa facial paralysis

Hujafa hujaumbika: Msanii Justin Bieber apatwa na ugonjwa wa facial paralysis

Moja kwa Moja..

Msanii maarufu Justin Bieber ameshea video kwenye account yake ya instagram akieleza hali hiyo iliyompata inayosababishwa na virus aitwae 'Varicella zoster' ambao hushambulia nerves za sikio na uso.

Kutokana na ugonjwa huo Justin Bieber upande mmoja wa uso hawezi kutabasamu na macho yanashindwa kupepesa tena. Hali hiyo imesababisha shows zake zilizopangwa kufanyia siku za karibuni kufutwa vile vile amesisitiza kuwataka watu wamuombee kwa Mwenyezi Mungu arejee Ktk hali yake ya kawaida.

View attachment 2258852

Enzi za ujana na uzima
View attachment 2258855

Hali mpya
View attachment 2258856

Huyo anaelekea kupooza
 
Huyo anaelekea kupooza
Hiyo mbaya sana ,labda kwa vile ana mkwanja mkubwa anaweza kupatiwa huduma za kiwango na haraka na Mungu kumsaidia apone vinginevyo hali itakuwa mbayazaidi maana sura haiwezi kutabasamu tena..
 
"Kila siku imekuwa bora zaidi na Ktk maumivu yote haya nimepata faraja Ktk yule aliyeniumba na anayenifahamu"

" Ninakumbushwa kuwa anajua mambo yangu mimi yote. Anajua mabaya yangu yote ambayo sitaki mtu yeyote ayajue na wakati wote ananikaribisha Ktk mikono yake ya upendo"

" Mtazamo huu umenipa amani wakati wa thoruba la kutisha ninalo likabili"Ameaandika Justin Bieber
 
Back
Top Bottom