Hujuma kubwa dhidi ya reli mpya ya SGR inayofanywa na wanaccm na ndilo chimbuko la kukataa katiba mpya.

naunga mkono hoja ila sahihisho, reli ya nachingwea-mtwara haikua kusafirisha mkonge bali ni mradi mkubwa wa karanga ambapo waingereza waliuanzisha baada ya kuona kuna uhaba na upungufu mkubwa wa mafuta ya kupikia kwenye soko la dunia, mradi iliitwa groundnut scheme …
Sawa, mradi mwingine wa karanga ulikuwa Singida na reli ilitoka Dodoma.
 
Wanasema treni inabeba mabehewa machache ndio mana imefeli Kua suluhisho.
Kwahiyo malori hayakwepeki.
Si kweli, turnround ya sgr kati ya Dar na Kwala ni kubwa maradufu kUK liko lori, treni moja inachukua zaidi ya makontena arobaini na kuyafikisha chini ya nusu saa.
 
Ni mjinga tu ndiye anadhani reli hujengwa kwa lengo la kubeba abiria bila kujua abiria ni ziada tu, kutokana na lengo la kubeba mizigo ndiyo sababu reli huanzia bandarini na siyo kati ya mji na mji.
Gentleman,
kama ilivyo kwingineko duniani, Tanzania ina treni za mizigo na abiria, vitu ambavyo vinafanya kazi kwa ufanisi kila siku.

hakuna haja ya upotoshaji wala mihemko kwenye uendeshaji wa treni za mizigo na abiria Tanzania.
Kazi inaendelea vizuri sana 🐒
 
Mizigo iko wapi wakati yote inachukuliwa bandarini kwa kutumia malori badala ya kuyachukulia Kwala ambako serikali imegharas mia ujenzi kwa kutumia pesa nyingi. Wee panya hili jambo si la ushabiki wa vyama ni jambo lenye madhara kwa taifa kuliko lile la mabasi, sijui unatetea nini wakati serikali inakosa mapato.
 
Utawala wa hayati Magufuli uliona tatizo la gharama za matengenezo ya barabara zinazoelekea bandarini, hivyo rais Magufuli akaamua kujenga bandari kavu mkoa wa pwani eneo la Kwala, na ili itumike ikaamuliwa iunganishwe na reli ya sgr. Uwepo wa reli hiyo ungeiingizia mapato serikali ambayo yangetumika kuiendeleza reli hiyo kwenda bara na nchi jirani, lakini wahujumu wakabuni njia ya kujitajirisha kwa kununua ghafla malori mengi ili wasafirishe mizigo kwenda bara na kuipiga teke bandari kavu ya Kwala! Uamuzi unaotekelezwa na viongozi wa juu wa CCM ambao ni walinzi wa uchumi wa nchi huku wakijua reli bila kubeba mizigo inakuwa haina faida kwani hakuna nchi inajenga reli kwa ajili ya kusafirisha abiria na ili lengo liende kwa mafanikio wakazuia upatikanaji wa katiba mpya ambayo huenda ingewabana.
Wachumi wote wanajua bila mizigo reli inakufa kama ilivyotokea kwa reli ya TAZARA ambyo imejikuta ikikosa mizigo na kuambulia abiria ambao hawasaidii upunguzaji gharama za uendeshaji. Tujikumbushe reli ya Mtwara kwenda Nachingwea ambayo baada ya mradi wa mkonge kukwama ikabidi kuing'oa. Viongozi wamekua wakituhadaa kwa kujikita kupigia chapuo muda mfupi abiria wanaotumia kusafiri kati ya miji bila kujua nauli zitapanda mara dufu kufidia gharama za uendeshaji kutokana na mizigo mingi kubebwa na malori ambayo yanatuingizia gharama za matengenezo ya barabara kila mwaka huku wamiliki wakitajirika bila gharama! Ni raha iliyoje.
Duuh Mtwara nachingea kulikuwa na reli?
 
Mizigo iko wapi wakati yote inachukuliwa bandarini kwa kutumia malori badala ya kuyachukulia Kwala ambako serikali imegharas mia ujenzi kwa kutumia pesa nyingi. Wee panya hili jambo si la ushabiki wa vyama ni jambo lenye madhara kwa taifa kuliko lile la mabasi, sijui unatetea nini wakati serikali inakosa mapato.
Serikali haiwezi kukosa mapato hatakama unakwepa kulipa kodi gentleman.
Na usafirishaji wa mizigo kutumia reli hauna madhara yoyote ispokua faida tu.
Na hakuna haja ya mihemko kwenye ukweli huu ya kwamba, usafirishaji wa mizigo na abiria kutumia reli, unachochea ukuaji wa uchumi wa taifa letu 🐒
 
Bandari ya Kwala haina mizigo sasa kodi itapata toka kwa nani! Imejengwa kwa gharama na sasa haitumiki, sijui wewe unamtetea nani.
 
mizigo na abiria wa kusafirishwa kwa njia ya reli wapo wakutosha kuongeza pato la taifa na kusisimua uchumi wa taifa.

serikali sikivu ya CCM hashinikizwi na yeyote kutumia rasilimali zake gentleman 🐒
 
"mizigo na abiria wa kusafirishwa kwa njia ya reli wapo wakutosha", kwenda Kwala? Naona nawasiliana na kichaa.
 
Kuna kitu bado watu hawajaeleweshwa...

Treni ya Kwenda Kwala ni MGR.. na trip Moja inabeba kontena 27... Yaani uwezo wa kubeba zaidi ya hapo haupo
Wameshauri baadhi ya vipande vya chuma (mataruma ) yabadilishwe ili kuhimili mzigo mkubwa..

Juzi Tanga zimeshushwa mataruma mengi kwa ajili ya njia ya Kaskazini ili reli ibebe mzigo mwingi kwa wakati mmoja

Bandari ya Dar inashusha kontena 4,000 kwa siku... Sasa hiyo reli hata ikienda trip 20 kwa siku ni kazi Bure...

Kinachotakiwa labda ijengwe reli Mpya kabisa...ya Kwenda Kwala...

..hicho unachokisema kilitakiwa kushughulikiwa ktk hatua za awali za ujenzi wa bandari kavu ya Kwala.
 
Wakati wa uongozi wa Jiwe hawakuliwaza hili... Wao walikwenda kujenga tuu...wakasema reli ipo...

Watu wa kushauri kwamba reli hii mataruma yake hayahimili uzito mkubwa walikuwa wamelala
 
..mradi wa umeme wa rufiji nao hadithi ni hiyohiyo.

..wameongeza uzalishaji wa umeme lakini miundombinu ya kusambaza ni chakavu.
 
Tujikumbushe reli ya Mtwara kwenda Nachingwea ambayo baada ya mradi wa mkonge kukwama ikabidi kuing'oa
Marekebisho kidogo.
Reli ya Mtwara hadi Nachingwea ilikuwa kwa ajili ya mradi wa kilimo cha karanga siyo mkonge.
Mkonge ulilimwa Mtwara yenyewe hasa maeneo ya Mikindani ambako karibu na bandari haikuhitaji reli.
 
Kuna kitu bado watu hawajaeleweshwa...

Treni ya Kwenda Kwala ni MGR.. na trip Moja inabeba kontena 27... Yaani uwezo wa kubeba zaidi ya hapo haupo
Wameshauri baadhi ya vipande vya chuma (mataruma ) yabadilishwe ili kuhimili mzigo mkubwa..

Juzi Tanga zimeshushwa mataruma mengi kwa ajili ya njia ya Kaskazini ili reli ibebe mzigo mwingi kwa wakati mmoja

Bandari ya Dar inashusha kontena 4,000 kwa siku... Sasa hiyo reli hata ikienda trip 20 kwa siku ni kazi Bure...

Kinachotakiwa labda ijengwe reli Mpya kabisa...ya Kwenda Kwala...
Wewe hujafika Kwala Kuna kitu unapotosha kidogo..
Reli zote mbili ya SGR na MGR zimepita hapo Kwala.
Tena karibu na geti la kuingia bandari kavu mita 20 hadi 60 tu.
Kati ya reli moja na nyingine zimeacha umbali wa mita hazizidi 60 pia.
Reli ya MGR imeshaingia hadi ndani ya bandari kavu hiyo nimeona kwa macho toka mara ya mwisho nimepita hapo. Ilikuwa bado SGR kuingia ndani ya bandari kavu. Kwa hivyo inahitajika kipande kisichofika 1km kutoka SGR kuiingiza ndani ya bandari kavu.
Makusanyo ya bandari a Dar ya mwezi mmoja tu wkiamua wanajenga hicho kipande na chenji inabaki. Kifupi hawataki kufanya hivyo.
 
Aione JokaKuu
 
Mbona juzi wametoa taarifa vizuri kuwa Kontena 54% zinabaki Tz
Kati ya hizo 54% Asilimia 90 zinabaki Dsm
Sasa ulitaka mzigo wa Dsm upelekwe Kwala?
TAZARA haikufa sababu ya kukosa mizigo bali uendeshaji mbovu
 
Wewe hujafika Kwala Kuna kitu unapotosha kidogo..
Reli zote mbili ya SGR na MGR zimepita hapo Kwala.
Tena karibu na geti la kuingia bandari kavu mita 20 hadi 60 tu.
Kati ya reli moja na nyingine zimeacha umbali wa mita hazizidi 60 pia.
Reli ya MGR imeshaingia hadi ndani ya bandari kavu hiyo nimeona kwa macho toka mara ya mwisho nimepita hapo. Ilikuwa bado SGR kuingia ndani ya bandari kavu. Kwa hivyo inahitajika kipande kisichofika 1km kutoka SGR kuiingiza ndani ya bandari kavu.
Makusanyo ya bandari a Dar ya mwezi mmoja tu wkiamua wanajenga hicho kipande na chenji inabaki. Kifupi hawataki kufanya hivyo.
Ngoja nikueleweshe...

MGR ndio kipaombele kwa Kwala, Bandari ya Dar inapakua kontena 4,000 mpaka 5,000 kwa siku... TRC wakitumia SGR Ina maana safari za abiria Kwenda Dodoma ziwe mbili kwa siku ?

Kipande Cha kutoka Bandarini Kwenda Kwala kitakuwa busy masaa 24.. na patahitajika treni mahususi za mizigo kama mbili..uwezo wa kuchukua kontena kama 80 hivi kwa mara moja

Kumbuka tuna single lane reli ya SGR japo Kuna section chache za kupishana....

Hapa Serikali Cha kufanya ni kuongeza line Mpya SGR Kwenda Kwala...au SGR ifanye kazi usiku ..Tena kuanzia saa 5 ...baada ya treni ya mwisho..na bado mzigo hautamalizwa kutolewa bandarini

Kule Bahi Kuna Bandari kavu inajengwa... Na hili suala la namna ya kupeleka mzigo wa kutosha na njia bora ...wapo wanapiga mahesabu
 
Nimeridhika na ufafanuzi wako.
 
Back
Top Bottom