Hujuma kwa mmiliki wa Bus la Hokas na kilio cha adha ya nauli kubwa kwa wananchi wa kata ya Loya, Uyui -Tabora

Hujuma kwa mmiliki wa Bus la Hokas na kilio cha adha ya nauli kubwa kwa wananchi wa kata ya Loya, Uyui -Tabora

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Sumatra-Tabora

Takribani miezi mitatu iliyopita Bus la Hokas lilianza safari zake za Loya kwenda Tabora na kuleta ushindani wa kibiashara KWA mmiliki wa Bus la Mama's one na kufikia hatua ya kushusha nauli kutoka 12000/= Hadi 8000,10000 na 7000/= wananchi walifurahia ushindani huo na kushuka kwa nauli.

Taarifa zilizonifikia ni kuwa hujuma zilianza KWA mmiliki wa Bus la Hokas na kufikia hatua ya kusitisha safari zake Hadi sasa.

Hujuma hizo zilifanywa na mmiliki wa Bus la Mama's akishirikiana na baadhi ya viongozi wa kata ya Loya na wale wa ngazi ya juu mkoani Tabora Hadi kupelekea hatua ya Bus la Hokas kusitisha safari zake!

Wananchi wa Loya wanalalamikia kupanda KWA nauli Hadi 14000/= na 16000/= kinyume na TARATIBU Baada ya Hokas kusitisha safari zake RASMI.

Niiombe mamlaka ya Sumatra -Tabora kulitazama upya swala hilo ambalo ni adha KWA wananchi wa Loya!
Taarifa zilizonifikia ni kwamba si mara ya kwanza kwa mmiliki wa mama's kushirikiana na viongozi hao Kuwahujumu washindani wa kibiashara wa Loya Tabora hata mwaka jana lilifanyika!!wanyetishaji wanasema mmiliki wa mama's hutoa rushwa KWA viongozi husika Ili kuwawekea vikwazo washindani wake wa kibiashara.

Muda umefika wa kukomesha Tabia hii iliyokita mizizi na kuwa Tatizo kwa wananchi.

Ikumbukwe Loya ni Moja ya kata ya kimkakati kiuchumi hasa kwa zao la mpunga na uvuvi wa samaki ambao umekuza ukusanyaji wa mapato wa serikali KILA mwaka na Sasa hivi kuna mfumuko wa uvuvi wa dagaa uliokusanya mamia ya watu kutoka mikoa mbali mbali nchini hapo kwenye Mbuga ya wembere.

Ni matumaini yangu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi Batilda Buriani na viongozi wa Tabora watatatua kadhia hii inayoendelea kwa wananchi hao.

Nimepewa ujumbe nimeufikisha wenye mamlaka chukueni hatua.

Asanteni KWA kusoma
 
Back
Top Bottom