Huko Kenya moto si wa kitoto

Huko Kenya moto si wa kitoto

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
William Ruto amemjibu Raila Odinga kuwa asithubutu kuingiza wananchi barabarani kwani Kenya inaongozwa kwa sheria sio maandamano.

Ikumbukwe kuwa Raila Odinga alihitisha maandamano ya kitaifa tarehe 20, jumatatu ijayo, sababu ikiwa ni ugumu wa maisha, kuporwa kwa kura wakati wa uchaguzi uliopita, na Ruto kutotimiza ahadi zake ndani ya siku 100 tangu aingie madarakani km alivyoahidi kwenye kampeni.

Sasa ngoja tusubiri km Ruto atawapiga waandamanaji hadi wachakae. AFRICA figisu za uchaguzi zitaendelea kutoa roho za watu. Pia wanasiasa wasiwe wana wachukulia wapiga kura km wajinga. Wanasiasa wamekuwa waongo sana ili tu wapewe kura, na wakishapewa wanaanza kunyanyua makwapa.

In fact, there are no real politicians in Africa but political mongers.

Jumatatu siyo mbali let's wait.
 
Hamna kitu Ruto atafanya maana Raila akiguswa tu nchi itawaka moto. Imagine katika kura million 14 wameachana kura laki 3 pekee meaning ni 50-50.

Kama alijiapisha kuwa Rais na hakufungwa Wala kupiga waandamanaji ndio sembuse sahivi?

Ukabila utawamaliza Kenya
 
Huku mmeambiwa kulalamika maisha magumu ni unafiki maana hata UK vitu vimepanda bei.

BTW: Kauli ya Ruto kwamba yeye siyo muumini wa Handshake imechangia pakubwa kuibua hiki kinachotokea.

Wapinzani wa kiafrika wanapenda tu recognition hizo za ugumu wa maisha ni porojo tu.
 
Hakuwahi kujiapisha kuwa rais wa Kenya, hicho kipengele alikikwepa kijanja.
 
Huku mmeambiwa kulalamika maisha magumu ni unafiki maana hata UK vitu vimepanda bei.

BTW: Kauli ya Ruto kwamba yeye siyo muumini wa Handshake imechangia pakubwa kuibua hiki kinachotokea.

Wapinzani wa kiafrika wanapenda tu recognition hizo za ugumu wa maisha ni porojo tu.

Handshake ya Raila na uhuru, Raila alilipwa kama Rais kwa kila kitu na alipewa privaleges zote kama Rais na alikua mshauri mkuu wa uhuru hadi Ruto akageuzwa kama secretary na matiangi akawa na nguvu sana juu ya Ruto, hivo alichofanya Ruto ni kisasi na Raila anapewa nguvu ya kuvuruga na uhuru ili Ruto aharibikiwe kabisa na kwa akili za wakenya wameshaingia box , maana Raila alianza maandamano karibu county zote alivomaliza sasa anataka afanye maandamano kitaifa ili aende hadi ikulu kumtoa ruto, Raila yuko more calculated kwenye hiyo move
 
Huu upuuzi unaitwaga maandamano kwa nchi za kiafrica unatuchelewesha sana. Eti unaandamana kisa unga umepanda bei. Huyo raila watoto wake wapo mamtoni kama wa Lissu anatumia maskini kufanya fujo.
Ruto tandika virungu vya ugoko hao tukupe manyota.
 
Kuandamana kwa nchi za Africa utaumia na utakufa na Hakuna atakaye kuhurumia Kama unawaamini wanasiasa wa Africa means bado haujajitambua ni ukosefu wa Akili na Maarifa kuandamana kwa ajili ya siasa
 
Huyu mzee odinga mpumbavu anataka kuleta machafuko nchi isitawalike ruto piga hao wasiotaka kutulia majumbani mwao.
 
Jakuwahi kujispisha kuwa rais wa Kenya, hicho kipengele alikikwepa kijanja.
Whatever the case lakini mkusanyiko ulikutana kwa kazi hiyo mbona hawakuwazuia? Kuna machafuko yalitokea?

Yule Odinga hata Moi alimshindwa ndio sembuse Ruto ambaye Odinga ndio alimpa uongozi ODM!!

Ajaribu kutoa pua yake jumatatu ndio ataelewa why Kenyatta alikubali yaishe. Odinga ana watu akiamua kulianzisha trust me nchi itaingia vitani
 
William Ruto amemjibu Raila Odinga kuwa asithubutu kuingiza wananchi barabarani kwani Kenya inaongozwa kwa sheria sio maandamano.

Ikumbukwe kuwa Raila Odinga alihitisha maandamano ya kitaifa tarehe 20, jumatatu ijayo, sababu ikiwa ni ugumu wa maisha, kuporwa kwa kura wakati wa uchaguzi uliopita, na Ruto kutotimiza ahadi zake ndani ya siku 100 tangu aingie madarakani km alivyoahidi kwenye kampeni.

Sasa ngoja tusubiri km Ruto atawapiga waandamanaji hadi wachakae. AFRICA figisu za uchaguzi zitaendelea kutoa roho za watu. Pia wanasiasa wasiwe wana wachukulia wapiga kura km wajinga. Wanasiasa wamekuwa waongo sana ili tu wapewe kura, na wakishapewa wanaanza kunyanyua makwapa.

In fact, there are no real politicians in Africa but political mongers.

Jumatatu siyo mbali let's wait.
Dawa ya maandamano ya kisiasa dhidi ya serikali ni vidonge viwili tu.

1. Kama hoja za mpinzani hazina mashiko na watu wanaelewa, muachie mpinzani afanye maandamano na kama watu ni werevu watampuuza, hatapata mass appeal.

2. Kama hoja za mpinzani zina mashiko, panga mazungumzo kuzi address na uondoe haja ya maandamano.

Zaidi.

1. Maandamano ya amani ni haki ya kikatiba.
2. Wahuni wakivunja sheria, sheria ichukue mkondo wake.
 
Naomba kuuliza...je legality ya matokeo ya uchaguzi ambayo imekuwa ikisemwa na kina Raila ikoje...ni kweli kura ziliibwa ama la..!! Tuanzie hapa twende mbele Sasa
 
Ktb ya kenya ingebainisha uwakilishi serekalini utegemee asilimia za kura alizo pata mgombea uraisi wa chama kwenye uchaguzi!
Kama alipata asilimia.50%, 30%, 10%.... apewe mkate serkalini kwa asilimia hizo alizo pata kwenye uchaguzi!
Wenzenu TZ tunaelekea huko kuondoa bugudha!
INSHAALLAH!
 
Back
Top Bottom