Huko Kenya moto si wa kitoto


Na shida watu Wana Hali ngumu Kenya, hivyo itahamasisha maandamano.
 
Huyu mzee odinga mpumbavu anataka kuleta machafuko nchi isitawalike ruto piga hao wasiotaka kutulia majumbani mwao.

Akiwapiga ndio SULUHISHO?. Mtu amaebakia kuteua rafiki zake walioshindwa ubunge, usenator na ugavana kuwa CAS baadla ya kudeal na matatizo ya ugumu wa Maisha.
 
Ila tuwajulishe majirani wetu kwamba hapa kwetu kumejaa hakuna mahali pa kukimbilia, hivyo acheni hizo fujo.
 
Huu upuuzi unaitwaga maandamano kwa nchi za kiafrica unatuchelewesha sana. Eti unaandamana kisa unga umepanda bei. Huyo raila watoto wake wapo mamtoni kama wa Lissu anatumia maskini kufanya fujo.
Ruto tandika virungu vya ugoko hao tukupe manyota.

Mtoto gani wa Raila yupo nje? Halafu Kenya sio Tanzania am alone hata kudai mfumuko wa Bei upo juu ni kosa la kuitwa mnafiki. Yani mnaona maandamano ni fujo, kisa nyie mmeridhika na hali yenu. Kama umeshiba usiwasemee wenye njaa.
 
Lakini pia raia tusitumike kama kondomu kwa wanasiasa.
Yaani kupigania mtu awe madarakani kwa faida yake.
Waafrika wanasiasa karibia wote ni njaa njaa tu na kutaka sifu.
Utendaji Zero aliyepo na anayekuja wote sawa
 
Afrika hakuna wanasiasa bali kuna wachumia tumbo.

Tulikuwa tunasifu katiba yao...sasa ni wazi kwamba kwa mwafrika katiba ni maandishi tu haina tafsiri yoyote katika maisha halisi.

Katiba yao imewapa Uhuru wa kuandamana kudai gharama nafuu za Maisha. Huku kwetu Kuna mtu aliongea atafukuzwa kazi, huku hata kilo moja ya nyama iuzwe elfu ishirini wote tutajificha ndani na kulia kinafiki.

Kama wewe umeridhika na ugumu wa Maisha au umeshiba usiwahi kuwasemea wenye njaa.
 

Jibu murua mkuu
 
Mfumo wa uchaguzi na uongozi hauendani na hali halisi ya Afrika. Tanzania inatakiwa tuwe makini sana sana tukiandika katiba mpya ili tusifanye makosa. Kenya walitakiwa waondoe mfumo wa kumpa mtu mmoja madaraka makubwa.
 

Raila Hana njaa Kama unavyodhania. Kaangalie utajiri wake. Vimnofu Ruto anawapa rafiki zake akina Kidero na waruguru walioshindwa u haguzi.
 

Punguza uoga wa kitanzania. Ndio maana Kikwete anawatukana kwa kudai Kuna mfumuko wa Bei.
 

Hivi Makamu wa Rais yupo nje ya system, punguza uongo.
 
Kwakweli Raila alimwambia ruto huwezi tawala hii nchi nikiwa hai, kuna uwezekano ruto akatolewa madarakani pengine jeshi likaongoza nchi ili wakose wote...... Raila... wangemuacha tu kwa 5yrs ya urais...ili azeeke vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…