Huko serikalini Kuna nini, ni fedheha mwalimu kusikia mtoto uliyemfundisha anakwiba Mali za umma!!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

I declare interest, Mimi ni mwalimu wa watoto. Sasa Huwa tunakaa tunajiuliza, walimu Hasa tunakosea wapi?

Tuseme kwamba labda Kuna watoto wengine hawapiti mikononi mwetu, hili Si Kweli,

Mbona huku darasani tunawafundisha msiibe, tunawafundisha msizini, Kila mtu awe na mke wake mwenyewe muda ukifika, tunawakataza pombe, madhara ya pombe tunawaonyesha wazi, tunajitahidi sana kuwaelekeza Maadili na kumcha na kuhofu Mungu, Uadilifu nk nk

Na mara nyingi mpatapo fursa za KAZI mbalimbali au fursa katika siasa Huwa mnatujia, tunawaombea na kuwakumbusha kutenda HAKI, kuchukia RUSHWA na UOVU, kutunza raslimali za nchi Ili tupige hatua kimaendeleo nk nk.

Nini Hasa Huwa kinatokea mkiingia huko serikalini?

Unasikia mtoto yule yule uliyemfundisha amehusishwa na ubadhirifu wa Mali za umma, mtoto yule yule utasikia Eti ameficha bilioni 7 nyumbani, kazitoa wapi?

Mtoto uliyemfundisha anapata KAZI, mwaka mmoja tu tayari ana nyumba na gari, unajiuliza Kwa mshahara upi?

Hata Hawa wezi wa kura, wamepita kwenye Sunday schools na madarasa!!

Fanyeni mnayofanya ila mjue walimu wenu hatufurahishwi na vitendo vyenu vya uasi Kwa kutofuata mafundisho na maelekezo yetu.

Mungu anawaona.

Karibuni🙏
 
Sio wote mwalimu wengine ni mikopo inatubeba assume nalipwa million moja na laki saba.. Je Niki toa laki saba kila mwezi sipati million 60??za kuvimba na kagari.. Ila si semi kwamba waizi hakuna wapo karibu kila Taasisi na hasa top management
 
Nini Hasa Huwa kinatokea mkiingia huko serikalini?
Nakubaliana na mshangao wako maana mimi pia niliwahi kuwa mwalimu. Walimu tuko sawa kwenye mafundisho yetu ya kuwataka wanafunzi wetu wawe waadilifu, kwa hilo walimu hatuna makosa.
Kinachotokea kwa wanafunzi wetu ni kwamba, huwa wakipata kazi wanaingia kwenye system ya maisha ambayo uadilifu siyo kitu cha maana sana. Wizi, ubabaishaji, ubadhirifu, ezembe ndiyo zimekuwa nguzo za maadili ya utendaji kazi huko serikalini na kwenye anga zake. Kila mtumishi anatafuta njia za kuiba. Hiyo ndiyo culture ya utumishi wa umma sasa hivi. Akija mtumishi 'anayejifanya' kuwa mwadilifu atachekwa, atabezwa, kudharauliwa, kuitwa mnoko, na hata kutafutiwa njia za kufukuzwa kazi. Kwa hiyo inabidi aingie kwenye hiyo culture ili awe relevant ktk mazingira aliyomo. Wezi ndiyo wanapendwa zaidi kuliko waadilifu!
 
Sasa mwalimu,

Aina Gani ya mafunzo yasaidie wanafunzi wetu wasibadikishwe na mfumo ovu?

Ingawa waadilifu wapo japo Si wengi.
 
Mwalimu aliyemfundisha Mwigu, Makamba mdogo, nape, sijui Huwa anajivunia au anajilaumu🤔
 
Aliyemfundisha Bashungwa Abarikiwe, kijana ni mwadilifu.
 
Sasa mwamimu,

Anina Gani ya mafunzo yasaidie wanafunzi wetu wasibadikishwe na mfumo ovu?

Ingawa waadilifu wapo japo Si wengi.
Ni kweli waadilifu wapo, japo ni wachache.
Sidhani kama kuna "mafundisho" yanaweza kubadilisha huo utamaduni wa ufisadi. Kinachoeeza kubadilisha ni usimamizi imara wa sheria ambazo zitawafanya hao wezi wapate consequences za matendo yao. Mtumishi akikutwa na 7 billion ameficha nyumbani kwake na hana maelezo sahihi ya alivyozipata, ananyongwa hadharani na pesa na mali zake zinataifishwa, wengine watajifunza na kuacha au kufanya kwa kificho.
 
Ukisikia aliyekuwa mwanafunzi wako amenyongwa Kwa ufisadi,

Utajisikiaje kama mwalimu?
 
Mwl K Majaliwa, unaliongeleaje hili🤔
 
Ukisikia aliyekuwa mwanafunzi wako amenyongwa Kwa ufisadi,

Utajisikiaje kama mwalimu?
Nitasikitika; halafu nitasema sheria imechukua mkondo wake.
Kwenye nchi za wenzetu ambako ufisadi haupo au upo kidogo sana, wako serious sana na usimamizi wa sheria.
Bila kubadilika na kuondoa huu utamaduni wa bora liende tusitarajie mabadiliko yoyote.
 
Nakubaliana na mshangao wako maana mimi pia niliwahi kuwa mwalimu. Walimu tuko sawa kwenye mafundisho yetu ya kuwataka wanafunzi wetu wawe waadilifu, kwa hilo walimu hatuna makosa.
Kinachotokea kwa wanafunzi wetu ni kwamba, huwa wakipata kazi wanaingia kwenye system ya maisha ambayo uadilifu siyo kitu cha maana sana. Wizi, ubabaishaji, ubadhirifu, ezembe ndiyo zimekuwa nguzo za maadili ya utendaji kazi huko serikalini na kwenye anga zake. Kila mtumishi anatafuta njia za kuiba. Hiyo ndiyo culture ya utumishi wa umma sasa hivi. Akija mtumishi 'anayejifanya' kuwa mwadilifu atachekwa, atabezwa, kudharauliwa, kuitwa mnoko, na hata kutafutiwa njia za kufukuzwa kazi. Kwa hiyo inabidi aingie kwenye hiyo culture ili awe relevant ktk mazingira aliyomo. Wezi ndiyo wanapendwa zaidi kuliko waadilifu!
Mzazi pia ni mwalimu kwa mwanae, sasa unategemea mtoto wa MADELU aweje baadae?
 
Back
Top Bottom